du hata kuielewa hiyo issue yenyewe nimeshindwa!
Hapa pagumu.......
juzi nlikuwa na bosi wangu wa kampuni fulan.
alinionyesha sijui niseme mchezo au kitugan.kuna karata kwenye hiyo gemu(acha nitumie gemu)halafu kuna maneno yanatokea kukukaribisha kwenye hiyo chezo linaitwa magic world halafu zile karata zinatawanyika moja baada ya nyingine.
halafu nikaambiwa nichague karata 1na nisiseme ipi wala kugusa iwe siri yangu moyoni nikafanya hivyo halafu next step ikatokea picha ikionyesha upande mmoja sura ya mzungu jina la kwanza ivon sms pemben ikadisplay tazama jicho la huyo mtu (yote kwenye cm na ww mtu halis)badae maneno yakatokea ninajua nn umefikiria na kadi ulochagua mwisho ile kadi ambayo uliweka moyon inatoka kwenye orodha.nikastaajabu ila nkarudia tena kwa kuhis huenda ni system inayofanya kadi unayotazama ndo umechagua nkapiga kengeza naangalia kulia kumbe nimechagua kadi ya kushoto ikatoka ile ile nlowaza moyoni.
jaman nafikiria cpati jibu kuna technologia inayoweza kuvumbua hisia za mwanadamu kama hii???
great thinkers karibun kwa mawazo yenu.
Hiyo ni gemu ya siku nyingi. Kuna mchezo unaitwa "Magic cat", ambao kuna picha ya paka, na chini yake zipo karata saba. unatakiwa uiangalie kwa makini karata moja kati ya hizo saba, na baadaye, ile karata uliyoingalia inatoweka. Inadaiwa huyo paka anasoma hisia zako. Bado siri hiyo sijaitambua sana ila ni ka gemu ka siku nyingi.
Hiyo ni gemu ya siku nyingi. Kuna mchezo unaitwa "Magic cat", ambao kuna picha ya paka, na chini yake zipo karata saba. unatakiwa uiangalie kwa makini karata moja kati ya hizo saba, na baadaye, ile karata uliyoingalia inatoweka. Inadaiwa huyo paka anasoma hisia zako. Bado siri hiyo sijaitambua sana ila ni ka gemu ka siku nyingi.
iko hv, zile karata za mwanzo zote anazokwambia uchague hazipo tena anapo onesha mara ya pili so hata kama moyoni utachagua karata zote zile basi akija kukuonesha mbele hutoziona karata zako zote.. Mfano anweka 9kisu, 9jembe, 4 kopa, 4 mavi, 2kisu na 2 mavi then ww utachagua moja na kuconcentrate na hio tu then atakwambia ashaijua karata yako thn atakuonesha 9kopa, 9mavi, 4kisu, 4jembe, 2kopa na 2 jembe, ww utadhani iliokuwa haipo ni ile yako tu ulichagua moyoni kumbe zile zote zinazooneshwa mwanzo hazijirudii, namba ni zile zile rangi zile zile bt sio zenyewe coz kama mwanzo aliweka 4kisu huku mbele anaweka 4kopa, mwenye swali aulize
hahaha hiyo hata mimi ipo kwenye cm yangu, ila nimeuelewa huo mchezo,
ni hivi kuwa makini unapochagua hiyo karata, na ukiletewa baadae utagundua zipo tofauti, yaani karata ulizoletewa mwanzo zinabadilishwa zote na unaletewa nyingine kwahiyo ile ulochagua mwanzo haitakuja. Nadhani mtakua mmenielewa.
Hamna chochote hapo FIX tupu. Ngoja nikuelekeze ugundue child trick inayotumika hapo.
Hicho kipicha cha mtu na jicho ni geresha ili tu uone na kudhani kuna kitu kisicho cha kawaida. Kwa kifupi iko hivi
Chukulia mfano seti ya kwanza ni
K-Kopa, 7-Mavi, 4-Shupaza na 2-Kisu. Wanavyokwambia uchague moja, akili yako hubakia kwenye hiyo moja uliyoichagua wewe. Sasa wanachofanya, ni kuzibadili zote kwa mfananio wa rangi kwa mpangilio ule ule.
K-Kisu, 7-Shupaza, 4-Mavi na 2-Kopa. Sasa kama wewe ulichagua 4-Shupaza kwenye seti ile ulioambiwa uchague, unapowekewa hii seti ya pili hutagundua kuwa seti nzima imebadilika. Wewe utaona tu ile 4-Shupaza haipo basi unadhani wameijua karata yako wakati si kweli.
Wewe angalia kwa makini utagundua karata zote zimebadilishwa na wala sio moja