Jamal Malinzi. Rais wa TFF

Makau Js

Member
May 25, 2017
93
233
NIMEMUONA raisi wa TFF NDUGU Jamali Malinzi akikosea Mlango wa Karandinga. Imenigusa sana. sizungumzii tuhuma zinazomkabili. Nawaza katika muktadha wa kiutu na kujifunza.

Hakukosea mlango wa kuingia katika karandinga kwa sababu haujui. La hasha. Ni mawazo na namna alivyo sasa. Wiki kadhaa nyuma alikuwa miongoni mwa binadamu wenye mafanikio na hadhi katika jamii. Kazini alienda kwa gari la thamani lenye kiyoyozi na alirudishwa nyumbani kuungana na familia yake kwa unyenyekevu. Leo ana amrishwa, anashurutishwa. Hana cha kufanya ila kutii.

Katika maisha kuna ajali nyingi sana. Unaweza kunusurika katika magari, ndege, meli na pikiki ila ukanasa katika tuhuma fulani. Nayo hiyo ni ajali.

Malinzi hana amri tena, hana uhuru tena. Kichwa chake hakiwezi kuwa sawa. Bila shaka alipotea mlango kwa sababu mwili ulikuwa pale ila akili ilikuwa sehemu nyingi ikijiuliza bila kupata majibu. Leo mimi niko hapa? Nachanganyika na hawa? Siwezi kuamua lolote ila kutii amri? Mbona dunia inanisaliti kwa kiwango hiki?
 
Sheria bwana haina cha mwendo wa polpole wakasi au unatembeaje polisi fanyeni kazi zenu
 
b0edda76ec8cfea270cf26ebce8a0b96.jpg
de14ec262bceff0788cbaa33cc07955b.jpg
6c93dd176f0db5baf8adc6421f621f7c.jpg
 
Aise kila nikiangalia ile video nacheka tu......by the way mleta uzi mbona umeongea kama wewe ndio malinzi au tuje tukupige p.a huko jela kama umeingia na simu....

Anyway ndio wajifunze hata hawa kina shoza kuna siku watakua behind bars
 
Kwa jinsi raia wa nchi hii walivo masikini' nikisikia jitu limehusika na ufisadi roho inaniuma sn na ndio maana kwenye hili watz tuache ushabiki hakuna mbadala wa magu.
 
Dini iliyo safi, isiyo na uchafu mbele za Mungu Baba, ndio hii: kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu.
 
Saa hizi kashalala mchongoma shwaini yule. Lazima apange foleni sambamba na vibaka wa kuku
 
Alafu eti kuna mwanaCCM anajiona yuko salama milele kwa kuonea wenzake.
Hivi macho huna hata hisia pia huna? Hakuna wana ccm alie salama kwa ufisadi? Hii awamu ya kufanya kazi na kubadilisha mitazamo mliozoea. Uwe ccm chadema cuf utanyooka tu.
 
Back
Top Bottom