Jamal Malinzi: Natukanwa sana JamiiForums, Facebook na redio mbali mbali

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
51,974
114,283
Katika hali ya kusikitisha kabisa rais wa TFF ametumia nafasi yake kuongea na media kujibu watu tunaomkosoa.

Malinzi ameweka wazi kuwa anatukanwa JF(Jukwa la Sports).

Sisi wanamichezo wa JF tumekuwa tukimpa changamoto mbalimbali Malinzi, kama member wa JF tumekuwa tukimwita kujibu maswali magumu ya member pasipo kutokea.

Malinzi amekimbia uzi wake alioanzisha mwenyewe akitaka kupata maoni toka kwa wadau.

Malinzi tumekuwa tukimhoji juu ya mashaka ya ajira za wahaya pale TFF, ambao waliajiriwa kipindi chake.

Pia ameshutumiwa kutaratibu upangaji wa matokeo ya Polisi Tabora na Geita Mining.

Vilevile tulitaka msimamo wake juu ya viwanja vilivyoporwa na CCM, ahadi yake ya soka la vijana. Pamoja na kuboronga kwa Taifa Stars. Je haya ni matusi?

Ninampa 24hrs atuombe radhi members wa Jukwaa la Sports.

========

JAMALI MALINZI AKIJIBU SHUTUMA ZA UPANGAJI MATOKEO,
LIGI DARAJA LA KWANZA

 
Ajiulize kwa nini Anatukanwa?? Huko kote kwenye social networks na media wanamuonea wivu??
Issue ni kuhusika kwenye sakata la upangaji matokeo!! Asitutolee mapovu!! Ajibu tuhuma
Kwa nini mechi haikurekodiwa kama walivyokubaliana?
Akubali TCRA wapitie mawasiliano yake ya simu!
Taarifa ya kamisaa inasemaje? Kuhusu kipa we Geita kutoka uwanjani na kurudi bila kuadhibiwa!
Dakika kipindi cha pili zilichezwa ngapi?
 
Hivi uchaguzi wa TFF unafanyika lini? maana huyu Malinzi aliendana na kasi ya JK kila kitu kipo ovyo ndani ya TFF


Hawa wakina Malinzi wote wako kwenye michezo kimaslahi zaidi na sio kuendeleza michezo. Kaka yake Dioniz ni mwenyekiti wa baraza la michezo hivyo wanamipango yao ya kutumia michezo kwa maslahi yao!! Kule Gymkhana club Dioniz alikuwa Mwenyekiti kwa muda mrefu sijui kama anaendelea; club ile ilididimia sana na members wengi waliondoka kwasababu ya uongozi wa hovyo!! Msitegemee maendeleo ya soccer mkiwa na Jamal Malinzi kwani kasi yake ilikuwa ya MSOGA!!! Kutafuta $$$$$$$$$ basi.
 
Siyo kosa lake jamani si mnajua kwenye soka kaja kutafuta pesa baada ya kuona kule kwenye u-agent biashara ilikuwa ngumu.
 
"Hakuna mtu alietukanwa Nchi hii kama mimi lakin hata mshipa wa Shingo haukunistuka, Namshangaa Mkurugenzi wa Tanesco kukondeshwa na vimaneno vya kufurahisha baraza"-Dr.Jakaya kikwete kwny uzinduzi wa Mitambo ya Gesi Mtwara.August 2015.
Malinzi asihuzunike ajikaze kiume, aliwahi kumpelekea Lowasaa kumuonesha Mipango mkakati yake akidhani angepata Ukikwete!
 
Back
Top Bottom