Kama unasoma ili uendeleze shughuli zako au uongeze uelewa wa ulimwengu nenda haraka ila kama unasoma ili upate ajira baadae hapo hujajua unachokitaka.
Elimu ni muhimu sana sema wabongo hawataki kuamini, endapo una shughuli ya kufanya unaamini hiyo ada haitakupiga chenga nenda. Uzuri muda ni mfupi wa kusoma ni kitendo cha kuwa serious na masomo basi.
Na usisome vitu vigumu kama Physics sijui Mathematics actually elimu ya bongo kwa sayansi ni kupotezeana sana muda na kujaribujaribu vitu vingi bila concentration ya vitu vichache muhimu, mwishowe unatoka ukiwa master of none. Labda kama wewe ni technician ila kama ni mjasiriamali soma masomo ya sanaa na biashara.
Nimesoma upuuzi mwingi kwenye sayansi na sijawahi kuutumia na sitokaa niutumie. Tofauti na watu wanavyodhani, nchi haina wajasiriamali hii labda ina watu wengi wanaodhani ni wajasiriamali. Ila sasa tumefundishwa hadi Extraction of Aluminium wakati hakuna ore yake Tanzania sasa sijui walijua tutahamia Urusi, Reproduction in flowering plants na matakataka kibao. Najutia muda wangu niliotumia kujifunza sehemu za uzazi za ua la tulip. Pumbaf mliotunga syllabus