Mwekezaji na mmiliki wa Jamaa Bakery, John Alfred Kyenkungu, sasa ameleta huduma za mikate na vyakula mbalimbali jijini Arusha.
Kenkungu aliyeanzisha biashara hiyo miaka 32 iliyopita, ameeleza safari ya mafanikio yake akishirikiana na maduka ya Nakumat Supermarket kabla haijafungwa.
Your browser is not able to display this video.
Sasa Kenkungu amefungua upya biashara yake hiyo jijini Arusha akilenga kuteka soko la utalii kwa kuuza mikate fresh inayookwa kila siku, pizza, sandwich, spaghetti, chipsi, chapati hadi mandazi, kuna ladha mbalimbali za kujivinjari nazo.
Mdau wa utalii Arusha, Benny Mayunga, ameipongeza bakery hiyo baada ya kuonja baadhi ya vyakula na kuvutiwa na ubora na namna vinavyoandaliwa.