Jalada kesi ya mauaji, laibwa ofisi ya RCO Kilimanjaro

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limeingia katika kashfa nzito likituhumiwa kuiba jalada la kesi ya mauaji ya meneja wa baa maarufu mjini Msohi ya Mo-Town,James John Massawe aliyeuawa kikatiri juni 9 mwaka 2009 katika kijiji cha Kindi Kibosho Moshi Vijijini.

Watuhumiwa wa mauaji hayo ni wafanyabiashara wanne ndugu,John Joseph Kisoka kwa jina la utani anaitwa 'magazeti'Deo Joseph Kisoka,Lucas Joseph Kisoka na Mussa Joseph Kisoka ambao wanamiliki vitega uchumi kadhaa katika jiji la miamba ya mawe la Mwanza Rock city'.

Ndani ya jalada hilo ambalo lilikuwa katika hatua za mwisho kupelekwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali kwa ajili ya kuandaliwa mashitaka dhidi ya watuhumiwa ,kulikuwa na maelezo ya mashahidi muhimu wanane lakini maelezo ya mashahidi sita yametopea pamoja na ripoti ya uchunguzi ya mwili wa marehemu.

Mauaji yalivyokuwa

Juni 9,2009 asubuhi marehemu alipigiwa simu na wauaji wakidai kuwa kaka yake marehemu aliyekuwa akijulikana kwa jina la 'kichwa' amegongwa gari na amekufa na marehemu alipotoka nje ya baa ili akimbilie eneo la tukio,alijikuta akidakwa na wauaji hao na kuingizwa ndani ya gari lao na kukimbia nalo hadi eneo la Kindi Kibosho ambako wanaishi na kumfungia ndani na kuanza kumpa kipigo cha kila aina.

Walikuwa wakimshinikiza awataje watu waliohusika na mauaji ya mama yao mzazi,Martha Kisoka ambaye alikuwa ameuawa wiki mbili zilizopita na watu walioaminika kuwa ni majambazi na licha ya marehemu kudai hawajui wauaji hao,aliendelea kupewa kipigo ambacho kilimfanya alegee na hatimaye kukata roho.

Baada ya mauaji hayo watuhumiwa hao walikimbilia nje ya nchi na kurejea mwaka jana kwa mbwembwe ambako walichinja mbuzi baada ya vijana wawili waliohusishwa na mauaji hayo licha ya kutokuwa wahusika wa kweli kuachiliwa huru na mahakama kuu.

Kupotea kwa jarada hilo ndani ya ofisi ya mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa(RCO) ni kielelezo cha nguvu ya fedha waliyonayo watuhumiwa hao ambayo imewapofusha macho polisi na kuamua kudhulumu haki ya mtu.

Maswali ya kujiuliza

Nani aliyekuwa mpelelezi wa kesi hiyo?

Nani alikuwa akitunza majalada likiwamo hilo?

Nani alikuwa akifanya mawasiliano na watuhumiwa?

Nani anawalinda watuhumiwa?

RCO atakwepaje kuwajibishwa kutokana na jalada hilo kupotelea mikononi mwake?



 
Yaani mpaka mnaandika haya RCO bado hajatiwa ndani? Kwa mtazamo wangu huyo ni shahidi namba wani.
 
Mh makubwa haya...lakini damu ya mtu italipiza tu kisasi hata faili likiibiwa tena hao walioiba faili wamejiongeza tu kwenye list ya watu watakaopokea adhabu toka kwa Mungu
 
Hiyo kesi toka mwanzo nlijua itaishi tu mana jamaa alikua rafiki n manumba so istoshe ushahidi ulikua mkubwa sana kuwatia hatiani
 
Ila damu ya mtu haipoteagi bure!! Lazima itawarudia wauajii...so sad
 
baada ya police kupoteza imani kwa utendaji wao...

nini kitafuata ?.
au ni heri kuchukua sheria mkononi..!!
 
rco bado yupo kazini ! sijasikia hakiwajibishwa...

maana kashindwa kazi aliyopewa.

alafu rais anachekacheka tu..
 
Jamaa walijificha Miaka 3 na walihonga zaidi YA milioni 600 kuanzia DPP

Maisha ya kujificha ni gharama makofia n deo wanaishi mombasa 2010 nlikua mwz luka alikamatwa akapelekwa moshi kusomewa case cjui iliishia wapi
 
Back
Top Bottom