Jakaya kikwete Will Retire as a "Statesman" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jakaya kikwete Will Retire as a "Statesman"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Feb 5, 2012.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Katika kitabu cha Mandela, Long Walk to freedom anasema kila binadamu ana madhaifu yake na mazuri yake. Tangia JK achaguliwe hasa kipindi cha pili amekuwa anaandamwa sana na ukosoaji ambapo waweza kuwa wa haki au si wa haki. Amekuwa anashutumiwa kwa kushindwa kuonyesha leadership na kuwa dhaifu kutoa maamuzi, rushwa katika serikali yake, kushindwa ku handle uchumi nk. Hata hivyo nina hakina JK atastaafu vizuri sana na ataheshimika sana baadae ila anatakiwa afanye mambo fulani madogo sana.

  (i) Aendelee kusimamia vizuri mchakato wa katiba na awe strong mbele ya wana ccm extremists. Kama akiendeleza ushirikiano na chadema na taasisi nyingine hadi mwisho na katiba mpya ya watu ikapatikana najua atakuwa amefunika mabaya yote anayolaumiwa nayo
  (ii) Ahakikishe uchaguzi ujao unakuwa wa huru na haki ndani ya ccm na nje ya ccm. Atajijengea heshima kubwa asipotumia nguvu kuingilia mchakato wa urais ndani ya chama chake na pia mgombea wa ccm dhidi ya upinzani. Ikitokea ameteuliwa Lowassa, sitta, magufuli nk amwachie agombee na ikitokea ameshinda Dr Slaa amwachie aongoze. Akifanya hayo atakuwa baba ya taifa.

  Hata kama akituachia uchumi mbaya kitu ambacho ni dhahiri, akifanya haya bado ataheshimika sana kwani uchumi utarekebishwa tu na yeye kwa sasa hataweza kurekebisha uchumi ila afanye haya ambayo hayahitaji kufikiri sana wala jitihada kubwa lakini yatakuwa na heshima sana kwake. Namshauri Rais wangu mpendwa ajikite kufanya mambo haya ya kuleta demokrasia tu ili aache legacy maana kiukweli sioni ni kitu gani zaidi anaweza kufanya akumbukwe kwa muda uliobaki. mungu mbariki Jk!
   
 2. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Atahukumiwa kwa matendo yake yote kama mazuri watamshukuru na kama mabaya atawajibika. Kufanya mema hakumfanyi awe safi hata kwa mabaya aliyofanya. Labda aweza samehewa lakini siyo kusafishwa
   
Loading...