Jakaya Kikwete arusha dongo la kizamani huko Mbeya... soma ucheke!

Kwali JK ataweza kumnadi mgombea wa urais ajaye kwa ahadi zile zile 78 alizotupa mwaka 2010!!!kwelii???ile reli ya umeme hadi Kigoma na Mwanza??zile meli kila ziwa,na viwanja ndege kila mkoa kuboreshwa kuwa vya kisasa??miradi ya maji,afya na elimu??barabara zote alizoahidi??yangu macho... Nasubiri kwenye ki box cha kupigia kura nitaamua mwenyewe
 
Jk kweli hana adabu kwa wageni yan ana lalamika hadi wageni wanajua wapinzani wanamsumbua!
Kweli udhaifu haufichiki!
 
naomba tukumbushane zile ahadi zote ili tuzidadavue utekelezwaji wake katika maeneo husika
 
Ni chadema ndio, kwani sugu akiwa bungeni aliwatangazia serikali kuwa, iwapo hawataunda tume/kamati ya kuchunguza zile vurugu za mbeya, basi atawahamasisha vijana/watu wa mbeya kususia kuwapokea viongozi wa serikali.
 
Sasa hapa apongezwe nani kati ya J.K,ccm au wafadhili? Pia atuelezee mali ambazo wahisani wanapewa kwa mlango wa nyuma.There is no free lunch in America!
 
Kikwete is the second smart president after Nyerere. You know why? This is the only URT President who has led this country without its first founder and yet goes well! Kikwete truly deserves some hands!

mmmh! We still have a long way to go! Kama ndo mawazo yetu haya
 
Nimesoma ila sijaona maneno ya kunichekesha, zaidi ya Rais kuongea ukweli.
 
Wamemkunukuu vibaya rais wetu? Rais hawezi kutoa hoja nyepesi na zilizokaa kimipasho hivyo. It is un-presidential!.

Upinzani hawakusanyi kodi, hawapokee misaada kwa niaba ya nchi kama ambavyo EU wame-fund huo mradi wa maji huko Mbeya. Kupatikana kwa maji infact inaweza kuwa sifa kwa upinzani maana kama sio wao hata huo mradi usingekamilika. Ufuatiliaji wa upinzani na ukaribu wao na wananchi ndio unaifanya serikali na CCM yake kukumbuka shuka alfajiri!

Hata hivyo ahadi za rais ni nyingi na sidhani kwa muda uliobakia anaweza kuzitimiza zote, na hapo bado ilani ya chama.

Nadhani na wewe umemuelewa vibaya Rais, alichosema Wapinzani wanashindwa KUHAMASISHA MAENDELEO. Sijaona sehemu aliyosema wapinzani wameshindwa KULETA MAENDELEO.
 
aliahidi meli ktk kila dimbwi la maji likiwemo la mtaani kwe2 mbona hatuzioni? wa2 wanakufa kwa kusafiria meli mbovu hallafu wengine mnasifu,hii nchi cjui imerogwa! TANZANIA ZAIDI YA UIJUAVYO
 
Nimesoma ila sijaona maneno ya kunichekesha, zaidi ya Rais kuongea ukweli.
hamna ukweli hapo huo mradi ulianza zamani na ni mpango wa EU kuwezesha majiji kupitia program yao na si kwasababu mtyu fulani kaomba,hata kabla ya uchaguzi huo mradi ulikuwa umeaanza,tuchape kazi tuache siasa za kujisifu zisizo na maana,hatujafika kabisa ndo tunachechemea,kiukweli mbeya kikwete hukubariki kabisa na 2015 huwezi kuongea chochote kule.tuache siasa tujenge taifa.
 
Muulizeni mbona alikuja kimyakimya mbeya anajua hatakiwi kabisa mkoani hapa.Halafu watu aliowahutubia waliletwa na malori kutoka maeneo ya nje ya jiji kama chunya na vijijini.
 
Mradi wa maji tena jijini tangia uhuru hadi leo miaka 50 bado ni miradi kama ya kujenga mahema ya makuti katika ufukwe wenye jua, mvua na upepo mkali......!
Akili ndogo katika kichwa kikubwa!
 
Nimejaribu kuipitia hii thread zaidi ya mara kumi lakini sijaona sehemu ya kuchekesha nilichobahatika kukiona ni rais Kikwete kaongea ukweli mtupu.
 
Kuna vyama kana kwamba anaongelea nchi nyingine. Huyu ndo rais anajidai watoto wote ni wake inakuwaje anashindwa kutoa ushauri kwa hao watoto wake wengine walio watukutu kama CDM, CUF, TLP NCCR n.k
 
Wamemkunukuu vibaya rais wetu? Rais hawezi kutoa hoja nyepesi na zilizokaa kimipasho hivyo. It is un-presidential!.

Upinzani hawakusanyi kodi, hawapokee misaada kwa niaba ya nchi kama ambavyo EU wame-fund huo mradi wa maji huko Mbeya. Kupatikana kwa maji infact inaweza kuwa sifa kwa upinzani maana kama sio wao hata huo mradi usingekamilika. Ufuatiliaji wa upinzani na ukaribu wao na wananchi ndio unaifanya serikali na CCM yake kukumbuka shuka alfajiri!

Hata hivyo ahadi za rais ni nyingi na sidhani kwa muda uliobakia anaweza kuzitimiza zote, na hapo bado ilani ya chama.

Mkuu usiwe bingwa wa kukosoa kila jambo ebu msome vizuri rais JK...

Rais amezindua mradi uliojengwa kwa gharama ya Sh79 bilioni, wenye uwezo wa kuzalisha lita za ujazo milioni 51 kwa siku mradi huo utawahudumia zaidi ya watu 381,000 na utadumu hadi mwaka 2017.

Mradi huo una uwezo wa kuzalisha maji mengi kuliko uwezo wa matumizi ya wakazi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake, mahitaji ya sasa ni lita za ujazo 38 milioni kwa siku...wewe endelea kupinga kila kitu.
 
Mimi napenda Watanzania tuwe watu wa kuona mambo kwa chanya,

Hapa mimi kwenye huu mradi wa maji Mbeya napenda kuipongeza Serikali ya Mheshimiwa Kikwete kwa kufanikisha hili,maana nia kubwa ni kuleta maendeleo,na pia kama CHADEMA wamesaidia huu mradi ukatekelezwa ni jambo jema,kwa sababu kuwa chama cha upinzani sio ugomvi ni ili kuleta ufanisi katika kuwaletea wananchi maendeleo,na sio magomvi.Watanzania tuepuke kujenga mbegu ya chuki kwenye jamii ya Watanzania.Mabadiliko katika nchi yetu yatakuja na sio lazima tumwage damu.Tufanye siasa za Kistaarabu.Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom