Jakaya Kikwete arusha dongo la kizamani huko Mbeya... soma ucheke! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jakaya Kikwete arusha dongo la kizamani huko Mbeya... soma ucheke!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Jul 22, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  RAIS Kikwete amezindua mradi mkubwa wa maji wa Uwanja mpya wa Ndege wa Swaya mkoani Mbeya, huku akivirushia madongo kwa vyama vya upinzani kuwa vinafikiria kuanzisha ugomvi kila siku badala ya kuhamasisha maendeleo.

  Rais Kikwete alisema atahakikisha anatekeleza ahadi zake zote alizoahidi wakati wa kampeni mwaka 2010 na kuhoji vyama vya upinzani vitawaeleza nini wananchi wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015.

  Akizungumza na wananchi wa Mbeya kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uzinduzi wa mradi mkubwa wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira uliopo Swaya, Rais Kikwete alisema kuna vyama vya siasa vya upinzani vinafikiria kuanzisha ugomvi. Ingawa Rais Kikwete hakutaja jina la chama, lakini ni dhahiri kwamba alikuwa akikilenga chama kikuu cha upinzani nchini cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho ndani na nje ya Bunge kimejikuta kwenye mvutano na serikali kwenye masuala kadhaa yanayohusu maslahi ya taifa.

  "Wengine wanatafuta ugomvi kila siku badala ya kuhamasisha maendeleo tuone mwaka 2015 watawaeleza nini wananchi, sisi chama chetu kinawahudumia wananchi wakati wengine wanawazuia wasiende kwenye miradi ya maendeleo, ikifanikiwa wao wanakuwa wa kwanza kuhitaji huduma wakati hawakushiriki kuhamasisha," alisema Rais.

  Akizungumzia mradi huo mkubwa wa maji uliogharimu sh bilioni 79.5, Rais Kikwete alisema umejengwa kwa ufadhili kutoka nchi za Jumuiya ya Ulaya iliyotoa sh bilioni 36.9, Ujerumani sh bilioni 13.5 na serikali sh bilioni 29.1 kupitia programmu yake ya maji.

  Pia aliwaonya wananchi kuacha tabia ya kuharibu vyanzo vya maji na kuagiza kuwa wanapaswa kuvilinda na kuhifadhi miundombinu ya maji na kuvitaka vyombo vya dola kuwachukulia hatua wananchi watakaoshikwa wakiiba vifaa vya maji ambavyo vimenunuliwa kwa gharama kubwa.

  Katika uzinduzi huo ulioshuhudiwa na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Klaus Brandes, alisema kuwa nchi yake imekuwa ikishirikiana na serikali tangu mwaka 1973 katika miradi mbalimbali ya maendeleo na itaendelea kufanya hivyo kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili.

  Naye Kamishina wa Maendeleo ya Jumuiya ya Ulaya, Andris Piebalgs, alisema kiasi hicho cha fedha kilichotolewa na jumuiya hiyo, kimesaidia kukamilisha mradi huo.
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kuna thread nimeisoma hapa jana kuwa kuna mwenyekiti wa wilaya wa chama fulani wilaya ya Handeni alikuwa anawakataza wananchi kuchangia gharama za uboreshaji huduma za afya, mpaka ikafikia hatua wakarushiana maneno ya vitisho na diwani.

  Kwahiyo, Rais Kikwete yuko sahihi, kuna vyama vinavyobeza maendeleo. Hata yakipatikana vinaumia roho. Viongozi wa vyama kama hivyo wanatamani nchi iendelee kuwa maskini tu, ili wapate cha kusema.
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wamemkunukuu vibaya rais wetu? Rais hawezi kutoa hoja nyepesi na zilizokaa kimipasho hivyo. It is un-presidential!.

  Upinzani hawakusanyi kodi, hawapokee misaada kwa niaba ya nchi kama ambavyo EU wame-fund huo mradi wa maji huko Mbeya. Kupatikana kwa maji infact inaweza kuwa sifa kwa upinzani maana kama sio wao hata huo mradi usingekamilika. Ufuatiliaji wa upinzani na ukaribu wao na wananchi ndio unaifanya serikali na CCM yake kukumbuka shuka alfajiri!

  Hata hivyo ahadi za rais ni nyingi na sidhani kwa muda uliobakia anaweza kuzitimiza zote, na hapo bado ilani ya chama.
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Magwanda haya hawayaoni. Kwi kwi kwi teh teh teh!
   
 5. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Tuna miaka 50 tangu tuwe taifa bado tunaongelea miradi ya maji tu???
  Hivi ni lini maji yameanza kuwa muhimu nchini Tanzania?
  Leo hii tulitakiwa kuongelea ukuaji wa viwanda na hata kutafuta namna ya kuanza kuunda matrekta yetu wenyewe??
  Ndo kwanza karibu tunafikisha miaka 51 ya Uhuru Rais wa nchi anajivunia hatua ya kuondokana na visima vya maji??
  Kuna matatizo ya maji machafu toka vyooni na mabafu katika kila nyumba Tanzania,
  Ni lini tutajenga miundo mbinu ya kisasa ya maji machafu?
  Miji yetu inanuka mikojo na mavi masaa 24 wote tunaona sawa tu?!
   
 6. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Kikwete anapozungumza hivyo namsamehe kwasababu wakati wake umepita,tatizo langu ni pale hao wanaoitwa wanasiasa vijana wa CCM wanapoongea lugha kama hizi!!!
   
 7. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Jk chapa kazi,wanakukubali kimoyomoyo!
   
 8. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  SASA KUNA NINI HAPA AMBACHO HATUONI? Mbona hii haiko kwenye ahadi? Upuuzi mtupu
   
 9. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Teh teh eti thread kwani ni mangapi ccm wanayafanya wazi tena mchana kweupe tena mengine ni janga kwa taifa na ndo yaliyotufanya tuwepo hapa tulipo na umasikini wote huu na hajayaongea wala kuyafikiria? Kwa ushauri kwa jk na wewe angalieni kibanzi kama siyo jabali lililopo kwenye macho yenu kabla ya kuangalia kwa mpinyani wenu
   
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  your so so right, isitorhe kwa hii miaka miwili aliyokaa madarakani hajatimiza hizo ahadi zake hata kwa 10% iweje kwa hii miaka mitatu?
   
 11. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Chezea ccm walio wavivu kufikiria
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Umepita ila imekuwa kama ni garika ama mafuriko yalitupiga waTZ kwani amedidimiza uchumi wetu zaidi ya nchi zilizo vitani
   
 13. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  rais hayupo sahihi kwamba vyama pinzani vinafikiria kuanzisha vurugu hii siyo kweli! waanzishaj ni wao wanaovamia mktano
   
 14. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Kweli tumeanguka na tunatia aibu kutokana na rasilimali tulizo nazo,lakini anguko letu hata sisi tumeshiriki. Ni ukweli mchungu ambao wengi wetu hatupendi kukiri. Tunapiga kura kama malofa nj haya ndiyo matokeo ya uchaguzi wetu!
   
 15. b

  bashemere Senior Member

  #15
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ​wape chadema robo ya hiyo misaada mtaona tanzania kama paradise tatizo la rais wenu ni mswahili kagame alimwita mswahiliswahili upeo wa ubongowake ni kama wewe zoba imagine jiangalie wewe na maoni yako hata ukipewa u dc utakuwa kituko kwi kwi kwi
   
 16. African American

  African American Senior Member

  #16
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikwete is the second smart president after Nyerere. You know why? This is the only URT President who has led this country without its first founder and yet goes well! Kikwete truly deserves some hands!
   
 17. Umslpogaaz

  Umslpogaaz Member

  #17
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 14, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kasema hayo, amejidhalilisha kwa hao waliotoa fedha kufadhili mradi huo maana inaelekea hajui maana ya kuwa na vyombo vya upinzani. Ni kazi ya serikali kutekeleza miradi yote pamoja na ile ambayo imefadhiliwa kutoka nchi za nje. Uthibiti wa vyama vya upinzani dhidi ya ufisadi ndio unamfanya kusema hayo, vinginevyo tungeona hizo pesa zinaliwa na mafisadi.
   
 18. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu baba hana aibu kabisa..si jukumu la wananchi kichangia miradi ya maendeleo hiyo ni kazi ya serikali..
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi na wewe unajiita Mtanzania?
   
 20. S

  Same ORG JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni aibu chama tawala kila neno kuvizungumza vyama vya upinzani,ni wakat wa chama tawala kujilaumu tokea miaka ya uhuru mpk leo bado mulikua wapi mpk vyama vya upinzani wapate mwanya wa kuzungumza makosa yenu?
   
Loading...