Jaji Werema: CUF wamevunja Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Werema: CUF wamevunja Katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jan 9, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]NI KWA KUDHARAU AMRI YA MAHAKAMA, ASEMA KOSA HILO LINAKIFANYA KIKOSE UHALALI WA KUWA CHAMA CHA SIASA
  Kizitto Noya
  MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema amesema Chama Cha Wananchi (CUF) kitakuwa kimevunja Katiba, kama kweli kilipuuza amri halali ya Mahakama iliyokizuia kuendesha kikao kilichowajadili na kuwafukuza Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na wanachama wake wengine wane.

  Januari 4, mwaka huu Jaji Augustine Shangwa wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, alitoa hati ya pingamizi kuzuia kufanyika kwa mkutano wa Baraza Kuu la CUF, na hatua yoyote ya kuwajadili Hamad Rashid na wenzake, lakini CUF kiliendelea na mkutano huo ambao uliwafukuza uanachama makada hao ambao wote walikuwa ni wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi.

  Jana, Jaji Werema akizungumza na Mwananchi kuhusu mgogoro unaoendelea kufukuta ndani ya CUF dhidi ya mbunge huyo wa Wawi, alisema "... Sina hakika kama amri hiyo ipo, lakini kama kweli kuna 'court injuction' iliyotolewa na Mahakama kuzuia Hamad Rashid na wenzake wasijadiliwe na Baraza la Uongozi na kuwafukuza, basi CUF imevunja Katiba," alisema Jaji Werema na kuendelea:

  "...Tena hakiishii (CUF) kuvunja katiba tu, kosa hilo linaenda mbali zaidi na kukifanya chama hicho kikose uhalali wa kuendelea ku-exist (kuwepo)."

  Pamoja na Hamad Rashid, wengine waliovuliwa uanachama na kikao hicho cha Baraza Kuu ni wajumbe wa baraza hilo na maeneo wanayotoka yakiwa kwenye mabano ni Doyo Hassan Doyo (Tanga), Shoka Hamis Khamis Juma (Pemba) na Juma Saanane (Unguja).

  Jaji Werema alisema katika mifumo ya utawala duniani, lazima kuna chombo cha mwisho cha uamuzi, ambacho kimsingi, kinapaswa kuheshimiwa na vyombo vingine vyote bila kuhojiwa na kwa hapa nchini, mahakama ndiyo yenye mamlaka hiyo.

  "Lazima kuwe na mtu au chombo ambacho kikisema, wengine mnasikiliza sasa kama kweli CUF waliiona amri ya Mahakama na wakaendelea na walichotaka kufanya, huku ni kuvunja Katiba. Na chama cha siasa kikivunja Katiba, kinakosa uhalali wa kuendelea kuwepo," alisisitiza Jaji Werema.

  Jaji Werema alisema ingawa CUF inaweza ikawa sahihi kabisa katika uumuzi wake huo, lakini kama kilikaidi amri halali ya Mahakama, kimekosea.

  "Ni ngumu kusema CUF imekosea kumfukuza Hamad wala kupuuza madai ya Hamad dhidi ya CUF. Kikubwa hapa ni nidhamu. Nidhamu kwa pande zote mbili, na nidhamu hiyo iambatane na heshima kwa sheria za nchi," alisema Jaji Werema.

  ...Aungana na Tendwa
  Awali, Jaji Werema aliungana na kauli iliyotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini John Tendwa kutaka kufanyike marekebisho ya sheria ili vyama vya siasa visiwe na mamlaka ya mwisho kumfukuza mbunge akisema:

  "Mimi naungana na Tendwa kwamba sasa ni wakati muafaka wa kurekebisha sheria hii. Mbunge ni wa wananchi, lakini kikatiba mbunge pia ni wa chama. Inaonekana sasa vyama vya siasa vimeanza ku-abuse dhamana tuliyowapa ya kuwadhamini wabunge na kuanza kuwafukuza ovyo."

  Aliendelea," Nasema nakubaliana naye (Tendwa) sheria ibadilike na tutafute njia ambayo inaweza kuleta mwafaka zaidi. Hatuwezi kuendelea kuikalia kimya sheria hii. Zamani tulipotaka mbunge adhaminiwe na chama, tulikiamini sana chama, lakini siku hizi mambo yamebadilika. Ukosefu wa nidhamu uko pande zote, siasa siku hizi ni ubishi tu."

  Kwa mujibu wa Jaji Werema, ili kulinda demokrasia ya kweli, ni lazima sheria hiyo ibadilishwe ili vyama visiwe na mamlaka ya kumfukuza mbunge moja kwa moja.

  "Wito wangu kwa watanzania ni kwamba, tutumie fursa hii ya marekebisho ya Katiba kujadili suala hilo, iwe kabla au baada ya mchakato, lakini sheria hii haitufai," alisisitiza.

  Tendwa akizungumza na waandishi wa habari Ikulu wiki iliyopita, alipinga uamuzi huo wa CUF kumfukuza Hamad Rashid akisema ulikiuka maslahi na haki ya wapigakua waliomchagua, kwani umeangalia maslahi ya chama zaidi na kwamba ipo haja ya sheria kubadilishwa ili mbunge aliyechaguliwa asiweze kufukuzwa kabla ya muda.

  Kauli ya Seif

  Lakini, juzi Maalim Seif katika mkutano wake wa hadhara jijini Dar es Salaam, alisema CUF hakijapokea barua yeyote kutoka mahakama kuu kuhusu pingamizi na kuwa kama kuna pingamizi lilishachelewa kwani chama hicho kilishafanya uamuzi.

  Alisema kama mahakama ilitoa pingamizi hilo, basi walikuwa na sababu ya kupeleka katika Ofisi za CUF kabla ya chama hicho kukaa kikao ambacho kilitumia Sh30 Milioni kufanya uamuzi mgumu ya kufukuza wananchama wake.

  “Mahakama zinajua Ofisi za CUF zilipo, lakini imeshindwa kuleta pingamizi hizo halafu Kibwetere (Hamad Rashid Mohamed) anasimama kwenye vyombo vya habari kuongelea pingamizi la mahakamani”

  Alisema kinachoongelewa ni Hamad Rashid ni kupitia vyombo vya habari na sio mahakama kuleta barua ofisi za CUF. Alisema kama mahakama itafanikisha mpango wake wa kumsaidia Hamad Rashid basi mbunge huyo atakuwa wa jimbo la Mahakama na sio jimbo la Wawi.

  Maalim Seif alisema Spika wa Bunge Anne Makinda ameshapewa Barua ya kufukuzwa uanachama Hamadi kama ataamua kumlea ni hiari yake.

  Alisema Spika ni mwenye uamuzi wa kutangaza Hamad Rashid sio mbunge kwakuwa hana sifa ya kuwa mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Wawi baada ya kupelekewa barua na chama na sio mahakama, na kumtahadharisha spika kuwa ukimya wake utampoza kutokana na kushindwa kufanya uamuzi wa kitaifa.

  Dk Kashililah
  Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashililah jana alishindwa kuthibitisha wala kukanusha kauli ya Seif kwamba CUF imeshakabidhi barua kwa spika kumjulisha kuwa Hamad Rashid amevuliwa uanachama CUF hivyo sio mbunge wa chama hicho.

  "Soma gazeti la jana naona wakusema hivyo CUF, sasa unataka nithibitishe nini tena, huamini kauli yao? alihoji Dk Kashililah katika ujumbe wa simu ya mkononi

  Akizungumzia hatua hiyo ya CUF kudharau amri ya mahakama juzi, Hamad Rashid alisema anachojua yeye bado ni mbunge na leo anaenda mahakamani kujua hatima yake baada ya CUF kukaidi amri ya Mahakama.

  Awali Hamad aliwaambia waandishi wa habari siku moja baada ya uamuzi wa kufukuzwa kwake kuwa anasikitika kwamba Maalim Seif hajitambui kuwa ni nani katika jamii, kwani angelijua hilo, asingebishana na mahakama.

  "Huyo ndiye makamu wa kwanza wa rais anayepingana na mahakama. Atawezaje kuendelea kuwa kiongozi kama hatambui hata mipaka yake?" alihoji.

  chanzo.
  http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/19153-jaji-werema-cuf-wamevunja-katiba.html
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  werema ***** sana
   
 3. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  atakuwa mbuge anayeiwakilisha mahakama bungeni !!!
   
 4. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Hebu rudia tena ,sijakusoma vizuri hapo kwenye nyota.
   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Ni wakati gani amri ya mahakama inahesabika kuwa imetolewa/imefikishwa kwa mlengwa/walengwa? Mahakama/Hamad wanasema imetolewa, CUF wanasema hawajaipata! Kwa mwenye weledi juu ya jamboi hili ningeomba afafanue zaidi ili tuielewe vizuri zaidi 'senema' hii.
   
 6. m

  mariantonia Senior Member

  #6
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 135
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hamad rashid anatumika sana na ccm lazima atetewe
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jan 9, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mbona Maalim Seif anaidharau sana Mahakama?
   
 8. Tz-guy

  Tz-guy JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Yaelekea una wazo zuri, embu fafanua kidogo.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sasa Jaji Werema kasema vizuri kweli - chama cha siasa kikivunja Katiba ya Muungano kinakosa Uhalali wa kuwepo. Tunakubali.

  Na ni vizuri kuwa amesema "chama" bila kulazimisha kuwa inahusu vyama vya upinzani hivyo nami naamini maneno yake yanakihusisha CCM vile vile.

  a. Kwenye sakata la mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar tunajua kuwa viliwekwa vipengele na CCM ambavyo vinakinzana moja kwa moja na Katiba ya Muungano.

  b. Kwenye kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya tunajua CCM (rais na wabunge wake) wamefanya jambo ambalo hawana uwezo kulifanya chini ya Ibara ya 98 ya Katiba. Hawana uwezo wa kuanzisha mchakato wa kuandika "Katiba Mpya". Uwezo pekee walio na kikatiba ni wa kufanyia mabadiliko Katiba iliyopo na utaratibu wa kufanya hivyo umeanishiwa Kikatiba. Hivyo sheria yao ya na maamuzi yao kuelekewa Katiba Mpya ni kinyume na Katiba ya sasa.

  SWALI: Je, CCM inapata wapi uhalali wa kuendelea kuwepo madarakani kama nayo imevunja Katiba kama vile CUF inatuhumiwa kufanya?

  Hapa ndio utaona simulizi la "vikapanda vikashuka" linapoanza.
   
 10. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Tatizo sio kutumika! tatizo ni serikali kufulia! haina pesa za kuendesha chaguzi ndogo.
   
 11. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  duu :shock:
   
 12. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  sawa kabisa..
   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  masikini Hamad Rashid weeeeee.

  Ulimi umekiponza kichwa.
   
 14. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanajamii!
  Sasa naona AG Werema anaanza kupevuka. Sheria ya kulazimisha watu kugombea nafasi za misuses huku wakimilikiwa na vyama vya siasa inavunja Katiba iliyopo. Kwa maneno ya Jaji Werema CCM hakipaswi kuwa chama cha siasa kwa sababu ni Serikali ya CCM iliyopeleka Bungeni mswada wa sheria kupinga Hukumu iliyotolewa na Mahakama kuu miaka kadhaa iliyopita kuruhusu kuwepo kwa Mgombea binafsi jambo ambalo hata marehemu Baba wa Taifa aliliona ni kosa la kimsingi lilofanywa na CCM zaidi ya miaka kumi iliyopita "by default CCM broke the constitution" sasa kwa mantiki hiyo kwa nini Watz mnaogopa kesi Kama hiyo ya kikatiba ikifunguliwa uwezekano wa kushinda ni mkubwa . Kwa mtaji huo CCM yaweza kufutwa kama Tendwa ataacha u- CCM wake and then tunaweza kuleta mageuzi ya aina yake katika sehemu hii ya Africa! Tuchaingie hii mada bila jazba ni uwezekano wa kufunga bao kwa ulimi!:A S 465:
   
 15. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  werema mnafiki,badala ya kuongelea mgombea binafsi,anaongelea kubadilisha sheria ya uchaguzi/vyama vya siasa kutofukuza wabunge,..target yao ni kutaka mapandikizi yao kama shibuda na wengineo kutofukuzwa...
   
 16. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,782
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Werema anaweza akawa anasema kweli lakini siyo mtu wa kuamini kauli zake. Mpaka sasa huwa najiuliza aliteuliwa vp kuwa jaji na kituko cha mwaka kuwa AG. Huyu alipaswa kuwa katibu wa CCM ktk level ya wilaya siyo zaidi ya hapo
   
 17. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  CCM ni chama. Serikali si ya CCM. Ni ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

  CCM kama chama kinahusikaje na katiba ya Zanzibar?
   
 18. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #18
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maandamano!
  Pamoja na unafiki wa AG Werema ukweli unabakia kwamba mbunge anachaguliwa na raia ambapo wengine Kama mimi hatujajiunga na Chama chochote cha siasa "for obvious reasons". Haingii akilini endapo kamati ya utendaji ya chama fulani yenye wajumbe wasiozidi 30 watakula njema "for one reason or the other" kumfukuza chama bila kuzingatia kwamba wao hawakumchagua kuwa mbunge kwa wakati huo huo turudi nyuma for balance and checks hatuwezi kuwabebesha walipa kodi Mzigo wa kugharamia uchaguzi mdogo ambapo gharama yake ni Katibu fedha za Kitanzania (Tshs.) billion 20. Ni bora tubadilishe sheria kesho asubuhi ili Kama atafariki au akijiuzulu mbunge for any reason atangazwe mbunge aliyefuatilia kwa kura lakini mimi sishabikii partisan politics huo Mchezo wa kutimuana sio democratic and it costs us for no reason. So right or wrong hoja ya Werema is very valid.:A S 465:
   
 19. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #19
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Binafsi kama tulivyo wote nakiri Katiba yetu ina mapungufu sana. Tukiwa katika mchakato feki wa kubalidisha katiba ambao umevunja katiba yenyewe, nadhani AG angeongelea suala la kuvunja sheria kulikonywa katika mchakato wa katiba.

  back to the topic, Mchakato halali wa katiba utakapoanza nadhani suala la mgombea binafsi halina mjadala ni lazima liruhusiwe.

  Pili, kuwe na kipengele ambacho kitaeleza clear kuwa iwapo mbunge kupitia chama, atafukuzwa na chama chake, atabaki kuwa mbunge wa kujitegemea hadi msimu wa ubunge huo utakapoisha, (uchaguzi ujao), ila akiamua kuhamia chama kingine, atapoteza ubunge wake, ili kuepuka wabunge wengi kuhama na ubunge wao kwenda chama kingine.

  Sio tu kufanya uchaguzi mdogo ni gharama, bali pia kama tungekuwa na Serikali katika hii ardhi tunayoikalia, fedha hizo ni bora zitumike wkenye masuala ya maendeleo kuliko kurudia rudia uchaguzi, na kupotezeana muda.
   
 20. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Siku zote ukipenda ghasia penda na matokeo yake. Sijui nini kinakuongoza kuona kuwa hili ni anguko la Hamad Rashid peke yake wakati umoja wa wanachama uko mashakani. Kwa taarifa yenu, viongozi wa baadhi ya mashina ya Tanzania Bara wanamkakati wa kushusha bendera matawini na kuzirudisha buguruni zilikotoka.

  Chama cha buguruni na akili zake za kibuguruni hivy hivyo!
  We kaa hapo shangilia ujinga bila kujua mwenzenu Seif Sharif Hamad hivi tunavyoongea ni mteule wa kunywa chai ya Ikulu ambayo ndio alikuwa anaililia miaka nenda rudi.
   
Loading...