Jaji Warioba ni "Bwana Kero" tokea zamani

Jaji Warioba ni "Bwana Kero" tokea zamani

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,357
mkapa.jpg

Kama alivyoandikika Edson Kamukana katika makala yake moja "ukiachilia mbali wasomi kadhaa walioamua kulamba matapishi yao na kumtusi Jaji Warioba na wana-CCM wengi wanaotukana bila kujua wanamtusi nani, katikati yake utaona wanaosalia si bure wana jambo na sababu za kufanya hivyo, hawa bila shaka wanalipa kisasi."

Mnamo tarehe Julai 17, 1997, Rais Mkapa alimteua Jaji Warioba kuongoza Tume ya Rais (Warioba Commission) kuchunguza na kubainisha mianya na vyanzo vikuu vya rushwa nchini. Baada ya kufanya mapitio ya sheria, kanuni na taratibu ndani ya serikali na kuonyesha mianya ya kukua na kuongezeka kwa rushwa nchini, Tume ya Warioba ilichapisha ripoti yake (Ripoti ya Warioba) tarehe 7 December 1997.

Baadhi ya mambo ambayo Tume ya Warioba iliyakuta ni pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa umma kuchukua rushwa kama sehemu ya kujazia mishahara yao (petty corruption) midogo. Lakini pia Tume ya Warioba ilikuta kuwa kulikuwa na rushwa nyingine (grand corruption) aka ufisadi iliyohusisha maafisa wa ngazi za juu na baadhi ya wafanyakazi wa serikali walio na ulafi wa kujilimbikizia mali.

Tume ya Warioba ilitoa mapendekezo ya hali ya juu yaliyogusa wizara na idara zote za serikali. Ripoti ya Warioba iligusa mioyo ya walalahoi na wengi waliotoa maoni ya kumtaka Rais Mkapa awafikishe mahakamani wale wote waliohusishwa na ufisadi kwenye Ripoti ya Warioba. Hata hivyo, ripotii hiyo iliwekwa kabatini na kutiwa kofuli. Ripoti ya Warioba imekuwa adimu sana kupatika kama ilivyokuwa kwa Hati ya Muungano.

Japokuwa ripoti hiyo iliwekwa kabatini, iliwagusa moja kwa moja vigogo kadhaa hasa wa CCM na wengi wao au watoto, ndugu na jamaa zao ndio wanaoshika madaraka leo. Kama mnakumbuka baada ya ile ripoti, ndipo vyombo vya habari vilianza kuripoti masuala ya rushwa, ikiwemo ile skendo ya IPTL iliyomfanya Mwalimu Nyerere aseme kuwa "kama huu ndiyo ushirikiano wa nchi za kusini, basi bora ukoloni urudi." Waliounga mkono au kuipinga IPTL wanajulikana. Wengine mtakuwa mnawakumbuka hata watawala wa miaka hiyo na wizara/idara walizokuwa wanaziongoza.

Akihojiwa na gazeti la Raia Mwema Mei 13, 2008, Jaji Warioba alisema kuwa "Baadhi yetu tumepiga kelele muda mrefu kuhusu hali ya rushwa nchini mpaka ikafika mahali ikawa watu wanatoa dhihaka tu. Kuna rafiki yangu mmoja, yeye alinipachika jina la ‘Bwana Kero' kwa sababu ya taarifa ile ya Tume ya Kero ya Rushwa. Alisema mimi nimegeuka kuwa kero kwa kuzungumzia rushwa kila wakati." Bado anaendelelea kuwa "Bwana kero" kwa kutetea Rasimu ya Katiba Mpya.

Kama alivyouliza Edson Kamukana, inawezekana kweli hao vigogo au watoto wao, ndugu na jamaa zao walioguzwa moja kwa moja na ile ripoti wakamsifu "Bwana Kero" wakati alishawaharibia kitumbua chao? Hatuoni vigogo hao wanautumia mchakato mzima wa Katiba mpya kama mwanya pekee was kumdhoofisha "Bwana Kero" na kujaribu kuendelea kuficha madhambi yao yaliyoyafichuliwa na "Bwana Kero" kwenye ile ripoti yake ya kero za rushwa 1997?

Kwa wale ambao hawakuwahi kuisoma Ripoti ya "Bwana Kero" itafuteni muisome halafu muone "kero" ambazo "Bwana Kero" aliziodhoresha kwenye ripoti yake. Halafu muunganishe the dots kwa kujiuliza ni kwa nini kigogo A na B au mtoto/ndugu/jamaa wa Kigogo C "anakereka" sana mpaka kumtusi "Bwana Kero"? Mara ya mwisho nilisoma muhtasari wa ripoti kwenye maktaba ya HakiElimu. Ilikuwa imejaa vumbi kweli kweli. Inaitwa "The Report of the Presidential Commission of Inquiry Against Corruption", kwa kifupi "The Warioba Report".
 
EMT

Kwenye hiyo picha uliyotumia unamuona huyo jamaa aliyeko katikati, kulia kwa Mwalimu?

Ndiye aliyemteua Warioba kuongoza ile Tume ya Rushwa. Ile ripoti ilimuunguza yeye mwenyewe, chama chake CCM na vigogo hadi vizazi vyao hadi leo. Nasikia naye pia anapinga msingi wa rasimu Shirikisho la Serikali Tatu...

Juzi kuna watu nilikuwa nabishana nao, wakisema Warioba kahongwa nishani. Atakaa kimya. Nikawaambia bahati mbaya 'vijana' wanamfahamu Warioba wa Tume ya Katiba. Nikawaambia mfuatilieni Warioba wa tangu first batch ya UDSM ikingali na kitivo kimoja tu cha sheria.

Nikawaambia ni kutojua tu kwa baadhi ya waandishi wetu na uvivu wa kusoma na kuperuzi wa wahariri na newsroom zetu kutafuta background ndiyo maana walithubutu kuandika uongo kwa kumnukuu mtu kama Abdalla Bulembo eti Warioba alihonga nyama...wakati ni Steven Wasira aliyetoa rushwa na akafungiwa kugombea. Iko kwenye Tanzania Law Report!

Warioba has been consistent. Nakumbuka aliwaambia 'dhamira yangu ni safi kabisa waje wanikamate tu' pale walipokuwa wanataka kumwangushia zigo la ufisadi wa Mwananchi Gold!
 
warioba wakati mwingine hufanya mambo ya maana lakini wakati mwingine naye ni bure kabisa kwenye hii nchi mtakumbuka warioba ni miongoni mwa watu wenye chuki binafsi kwa baadhi ya watu hasa walioko madarakani.

Lakini pia kama mtakumbuka warioba alitaka afukuzwe uwaziri mkuu wakati wa utawala wa mwinyi marafiki zake wakamtonya juu ya mpango wa kufukuzwa kwake akawahi akajiuzuru.
 
Kila binadamu ana Mapungufu yake , Lakini Mzee Warioba anayo Mazuri mengi kuliko mapungufu machache tatizo ni aina ya Nchi anayojaribu kuikwamua kujaa wajanja wengi, hawataki kusikia Azimio la Arusha,wamegoma kuhamia Dodoma na kulinusulu jiji na Foleni,kila kiongozi anataka kuishi Dsm , ni bora Utawala wa Majimbo uanzishwe ili angalau itasaidia Watu waanze kuishi Majimboni kwao na kupunguza Msongamano Dsm.
 
Salute EMT

Heri huyu "Bwana Kero" kuliko "Bwana Keroro"

Wengi sasa tunaelewa kwa nini Warioba hajali tena kuitwa "Bwana kero"
 
EMTWarioba seems to be the only person to influence and inspire people of this generation. Whether CCM will win in this argument or not; the legacy of Warioba, his ethical acts and his superb deliverables in those reports will always live and say something is one of the 'Few Good Men'Wabe
 
Last edited by a moderator:
"Takwimu ni za kweli ni kwanini kwa Nyalali na kwa Kisanga hawakusema twakimu ni za uwongo?" Warioba. Huyu Mzee kweli ni Kero badala ya kujibu hoja analeta porojo.
 
warioba wakati mwingine hufanya mambo ya maana lakini wakati mwingine naye ni bure kabisa kwenye hii nchi mtakumbuka warioba ni miongoni mwa watu wenye chuki binafsi kwa baadhi ya watu hasa walioko madarakani.

Lakini pia kama mtakumbuka warioba alitaka afukuzwe uwaziri mkuu wakati wa utawala wa mwinyi marafiki zake wakamtonya juu ya mpango wa kufukuzwa kwake akawahi akajiuzuru.

Acha unafiki wewe,hii hoja ya serikali 3 inakuuma sana eeh?Warioba uwa anasimama kwenye ukweli na hajali kama atakuumiza au lah,cha maana anaangalia anafanya kazi kwa maslahi ya watu gan
 
"Takwimu ni za kweli ni kwanini kwa Nyalali na kwa Kisanga hawakusema twakimu ni za uwongo?" Warioba. Huyu Mzee kweli ni Kero badala ya kujibu hoja analeta porojo.
 
"Takwimu ni za kweli ni kwanini kwa Nyalali na kwa Kisanga hawakusema twakimu ni za uwongo?" Warioba. Huyu Mzee kweli ni Kero badala ya kujibu hoja analeta porojo.

Tumie kichwa kufikiria ndugu na sio unalalamika mambo ya Takwimu tu,Tanzania ina watu wangap na je kikwete alishinda kwa kura ngapi?kama kweli unasimama kwenye ukweli, then tafuta ratio hapo
 
Angalia hapa Warioba alivyodhalilisha elimu yake:
"wewe ni mtanzania ila kama sio mzanzibar huwezi kupata ardhi Zanzibar pia huwezi kupiga kura znz ila kwao wakija tanganyika ni kinyume chake.

-Hivi kwe hajui kama Zanzibar ardhi imekwisha baada ya Hayati Karume kugawa heka
3 kwa kila mtu bila ya kujali ametoka upande gani wa muungano?
- Hivi kweli hajui Zanzibar ndiyo eneo lilaloongoza kwa mbanano wa watu kwenye
ukanda huu wa Afrika ikifuatiwa na Rwanda?
- Hivi kweli hajui kama Rais wa Zanzibar anachaguliwa na wazanzibar?
 
Huyu mzee ni kiboko! ni tunu ya taaifa tumheshimu tusimzihaki ni hazina ya fikra tumtumie tusije kujuta
 
Back
Top Bottom