Kinachonisikitisha zaidi ni kwanini Wanasheria wetu makini toka UKAWA pamoja na Jumuiya ya Jukwaa la Katiba (JUKATA) pamoja na Taasisi ya Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wanapoteza muda bila kufungua kesi mahakamani kuzuia ufujaji huu unaoendelea chini ya TUME na Serikali na kusababisha hasira za umma zizidi kujilimbikiza?
Tunawaomba Wanasheria hawa watambue kuwa utawala dhalimu siku zote unaziba masikio na kutokusikiliza chochote kinachohusu HAKI pale ambapo wanakusudia kutimiza udhalimu na malengo yao dhidi ya umma, na hivyo bila [Wanasheria watetezi] kuchukua hatua za dharura kunusuru hali hiyo, raia wasio na hatia wanakosa mtetezi wa mwisho, na hivyo kuathirika vibaya mbali na kupaaza sauti sana!
Tunawaomba Wanasheria wachukue dhamana ya kuinusuru hii dhahma inayoweza kutokea ktk nchi yetu, baadaye kwa kutokuzuia huu uovu wa Tume na Serikali inayotaka kutimiza kwa kulazimishia wayatakayo wao, huku wakikiuka wazi wazi sheria, kanuni na taratibu zilizoainishwa ikiwa ni pamoja na sheria na taratibu za utungwaji wa Katiba mpya. Msubiri hadi hili mpaka watu waanze kusababisha ghasia kama nchi nyingine? Hapana, tuilinde AMANI, ila tuidai HAKI bila kuchelewa.
Inatia hasira sana kwa ukimya huu wa wanasheria wetu!