Jaji Sinde Warioba kanishangaza

Njema kabisa

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
699
Reaction score
238
Ikumbukwe kuwa Jaji Warioba alikuwa akizunguka kutoa elimu ya uraia pamoja na kueleza wananchi jinsi maoni yao yalivyotupwa kwenye rasimu ya katiba jambo ambalo lilifanya atukanwe, adhihakiwe, adharauliwe na hata kudaiwa kupigwa.

Kilichonishangaza ni yeye kusimama jana na kupiga kampeni kwa wagombea, wakati kwanza chama hicho ndo kilihusika kusigina maoni ya wananchi, pili mmoja wa wagombea alikuwa makamu mwenyekiti bunge la katiba sasa Mh. Warioba ulikuwa unazunguka kufanya nini kwa wananchi ikiwa leo una wanadi waliosigina maoni ya wananchi?

Sikutegemea kwa kweli, sasa vipi ile rasimu ya wananchi ndo huitetei tena? Nimewaza kwa sauti wajamaeni.

 
huyu si ndio maana alipigwa na makonda, asipoangalia atadundwa tena
 

Amefnya hivyo kwa sababu gamba tayari limevuka, Fisadi hayupo tena CCM, Nachama kimebaki salama
 
Wallah walioba ni miongoni mwa Wa tz wasaliti.nashangaa nanazid kushangaa hili taiga Mzee kamahuyu nae!!!
 
Huyu Huyu Mzee Warioba Ndiye Alipigwa Na MaCCM Wenzake Kwa Sababu ya Kushaabikia rasimu yake ya Katiba. Leo Ni

Kimbembele wa Kuishaabikia CCM. Kweli CCM Ni Ile Ile..Do Hata Dr. Magufuli Hawezi Lolote Kwa MiCCM.
 
Njema kabisa
Hapo ndo utaona watanzania tuko tofauti duniani yule ni mwanasheria yuko vile je sie darasa hakuna tuko vipi ila huo ndo mfumo tuliojengewa watanzania ndo mana kenyatta alimwambia nyerere kuwa unaongoza maiti tanzania
 
Namuheshimu sana Jaji Warioba, lakini kwa hili la kukubali kutumika pamoja na kutukanwa sana na kupigwa kwa baraka ya chama hicho hicho, na bado akasimama nao jana linampunguzia sana heshima kwangu.. Nakumbuka Bulembo alivyomtukana huyu mzee and yet jana wakawa jukwaa moja..!
 
Uzee unachangia mambo mengi Warioba keshazeeka jamani Tumuache.
 
mtoto wake atapewa viti maalumu ni ahadi ... kazi zimekuwa issue now days
 
Tatizo tumbo na kuhakikishiwa ulinzi kwenye maslahi yake binafsi.
 
Msichoelewa ni nini katika huu wimbo? "CCM ni ile ilee, oo ni ile ile ileee... "
 
Nimepata jibu kelele za Humphrey Polepole hawa ndo waliokuwa wanamtuma!
 
Sikujua kama huyu mzee ni mnafki kiasi hiki; anaamua kusimamia masilahi ya chama anaacha masilahi ya Taifa!!!!? Hata hana uchungu wowote wa zile pesa za walipakodi alizozunguka nazo Tanzania nzima kukusanya maoni ya wananchi, duuuuuuh We are so foolish.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…