Jaji Ramadhani tafadhali bwana! Ama unasema kweli au la...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
40,000
1104808

Na. M. M. Mwanakijiji

Wakati mwingine unaweza kujisikia kizunguzungu ukiwasikiliza viongozi wetu ambao sasa wanaonekana “wanajua”. Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani amenukuliwa na gazeti moja akionesha kuunga mkono uamuzi wa Mahakama Kuu kutangaza kuwa mfumo unaowaweka viongozi au wanachama wa chama tawala kama wasimamizi wa uchaguzi ni kinyume na Katiba. Amedai kuwa tangu 1995 (akiwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi) walitoa mapendekezo ya kuondoa utaratibu huo. Lakini kwa miaka ishirini hilo halijatokea hadi hivi sasa.

Jambo ambalo linanitibua mimi zaidi ni kuwa Jaji huyu huyu ambaye anadai kuwa wana viongozi na mashabiki wa vyama vya siasa wasijiwekwe kusimamia uchaguzi alijitokeza 2015 akiwa amevaa magwanda ya CCM akitaka kugombea Urais chini ya mfumo ule ule ambao anadai wao hawakuupenda! Mfumo ambao anataka tuamini kuwa aliona hautakuwa wa haki (fair) kwa vyama vingine?

Sasa Jaji Ramadhani tafadhali bwana; hivi kama kweli ulijua kuwa mfumo huu ni mbaya kilichokufanya usimame na kutaka kugombea Urais kwa tiketi ya CCM ilikuwa ni nini? Unataka tuamini kuwa mapenzi yako kwa CCM yalikuja baada ya kuwa umeondoka Ujaji Mkuu? Je, haiwezekani kuwa kumbe mwenzetu tangu miaka “ile ya nineteen kweusi” ulikuwa ni mwanachama na shabiki wa CCM? Kwamba ulipokuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ulikuwa tayari na “mahaba” na chama tawala?

Kama hili ni kweli basi kuna mambo mawili; kwamba, unaamini kuwa kwa wewe kuwa na mapenzi au uanachama wa Chama cha Mapinduzi hakukufanya uvunje uadilifu wako wa kusimamia taratibu au sheria bila kujali mgombea anatoka chama gani. Kwamba, kama Augustino Mrema angeshinda mwaka 1995 wewe na wenzako mlikuwa tayari kumtangaza mshindi hata kama CCM ingeondoka madarakani? Je hili ni kweli?

Kama hili ni kweli unataka tuamini kuwa mwanachama wa chama cha siasa akisimamia na kuzingatia viapo vyake, maadili ya kazi, sheria na haki anaweza kusimamia uchaguzi bila kupendelea chama chake. Kwamba, ndio maana wapo wabunge wa vyama vya upinzani ambao wameshinda na kurudia kushinda kwenye majimbo yao licha ya wasimamizi wa majimbo hayo kuwa ama ni wanachama wa chama tawala au mashabiki wa chama hicho.
Jambo la pili ni kuwa kama hilo la kwanza si kweli basi ni wazi kuwa hukuwa mwadilifu na kuwa ulikuwa unafanya kazi kwa upendeleo ukiongozwa na mahaba kwa chama chako. Kwamba, kwa vile tunajua sasa kuwa wewe ulikuwa ni mwana CCM ulikuwa unafanya kazi kwa kificho kumbe moyoni ulikuwa na chama unachokipendelea kishinde.

Kama hili la pili ni kweli basi hoja yako ya kuwaondoa mashabiki na wanachama (walijionesha wazi) wa CCM kwenye kusimamia uchaguzi ni jambo la msingi, la lazima na ambalo haliepukiki. Hii ina maana kuwa siyo wana CCM tu bali Watanzania wote wanapaswa kushuku kila wakati na mara zote unapofanyika uchaguzi pale ambapo wasimamizi wa uchaguzi bado ni wana CCM. Kwamba, WAtanznaia na hasa wapinzani wasidhanie hata kwa mbali kuwa wakurugenzi hawa wa uchaguzi wanaweza kutenda haki.

Nikiangalia yote mawili naamini tatizo letu kubwa haliko kwenye uanachama wa wakurugenzi wa uchaguzi au watendaji wengine. Hii ni kwa sababu huwezi kuondoa mapenzi ya mtu kwa chama Fulani hata kama mtu huyo hatovaa gwanda hilo wakati akiwa kazini. Tatizo letu ni kutokuwa na mfumo ambao uko wazi, unaoneshimika na kila mtu na ambao kila mtu anaweza kuuamini kumtendea haki. Inapotokea kwamba wapinzani wanalazimika “kulinda kura” kwa kuhofia kuibiwa ni wazi kuwa mfumo hauko sawa na hauaminiki.

Badala ya kuhangaika na “uanachama” wa Wakurugenzi wa Uchaguzi naomba kupendekeza kwa heshima na taadhima tuangalia uadilifu wa watendaji – ikiwemo kuweka adhabu kubwa kwa mkurugenzi ambaye anaonekana kuharibu uchaguzi kwa sababu za kisiasa. Ni lazima tuangalie mfumo wa uchaguzi kuhakikisha kuwa wapinzani wanapata haki ile ile wanayopewa CCM. Haiwezekani wapinzani wanalazimika kutumia nguvu kubwa kweli hata kurudisha fomu za kugombea wakati CCM inaonekana wana mlango wao mwingine maalum.

Nitatoa mfano, Rais Magufuli alipozungumza (labda kwa utani au akimaanisha) kuwa yeye anateua wakurugenzi wa halmashauri halafu ati waje kumtangaza mgombea wa upinzani kashinda. Tulitarajia Tume ya Uchaguzi ingesimama na kutetea nafasi yake na kuwataka watendaji wake kutekekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na siyo matakwa ya siasa. Kama Rais Magufuli atawafukuza kazi wakurugenzi wa halmashauri kwa sababu wamemtangaza mpinzani hii ni haki na wajibu wake.

Ndio maana niliposoma habari ya kauli yako hii nimebakia kusema “Jaji Ramadhani, tafadhali bwana!”

Niandikie:mwanakijiji@jamiiforums.com
 
Ndugu MMM kwa kumbukumbu sawa hamna mpinzani aliyetangazwa kashinda ubunge bila msukumo wa wapigakura wake, sehemu ambazo watu walikuwa wastaarabu pasi na msukumo pamoja na kuwa wapinzani walishinda walitangazwa wagombea wa CCM kuwa wameshinda, mifano nichache, Mbagara, Ilala, Rungwe magharibi, Mbeya Vijijini, Kyela, Nyamagana, Ilemela nk . Kiufupi CCM haikustahili Hata kuwa na 1/3 ya wabunge bila uhafidhina wao!
 
Mzee Mwanakijiji;
Muunge tu mkono Jaji Augustino kwa sababu, huenda alitamani kuibuka mshindi ili aje kubadilisha hii kitu. Nadhani hata huyo aliyeko madarakani kuna siku nafsi humsuta anapoona kuwa; Hata ukimuuliza kiziwi atakuambia, haki haikutendeka aliposikia lile tangazo la aliyeshinda
 
Jaji agustino ameghafilika tu baada ya kukaa bench muda mrefu kama Membe na aina yao,nadhani ni muda muafaka wa kutumia neno kuwashwa washwa yeye agustino alisha kuwa kiongozi mkubwa tu kwenye tume ya uchaguzi pia aliwahi kuwa jaji mkuu nadhani kipindi hicho alipaswa kusema hili jambo na kuchukua maamuzi.
 
Mzee mwanakijiji mm Sina Cha kuongezea maana kwenye maelezo yako umemaliza, na ndo kilichomfanya jaji mstasfu ramadhani atie neno
Chukulie tu huo msemo wa mh. rais kwamba nateua wakurugenzi eti waje kutangaza mshindi mwingine
Kwa kauli hi tu je tume ya uchaguzi kupitia wasimamizi wake hao wanaoteuliwa na rais na pia wakiwa wanachama wa chama chake Cha CCM itaaminika kweli?
Lakini pia upande mwingine kwa mh jaji mstaafu nimejifunza kitu muhimu Sana kwamba SI wakurugenzi tu Bali ata wanaoteuliwa na rais kusimamia na kuongeza hiyo tume ya taifa ya uchaguzi ni wanachama wa CCM mfano mzuri ni huyu mstaafu, inaonekana miaka yote akiwa tume ya uchaguzi na akiwa jaji mkuu wa Tanzania alikuwa na hiyo kadi ya chama Cha mapinduzi.
Hitimisho : hapa tupambane tuwe na tume huru ambayo haisimamiwi Wala kuongezwa na wateule wa rais
 
Kwa hivi ruksa Mkulu kuendelea kuteua wakurugenzi wawe wasimamizi wa uchaguzi hata kama mahakama itapinga au mimi ndio sijakuelewa

Mzee Mwanakijiji uko bias
Tambua miaka yote Hii WaTz wamedhulumiwa haki yao kwa uzandiki huu
Nchi imekuwa ikiongozwa na viongozi waliolazimisha kushika madaraka
Leo umeungana nao
Nyie haya tu!
 
Unaweza kushangaa na kujiuliza wakati kauli kama ile ya Mh Rais inatolewa ni wangapi na akina nani waliupinga waziwazi ? kuna mashetani wengine bado wanairudia kwa kuisema kua Alikua anatania wenda.
Nchi hii inaangamizwa na watu wenye akili timamu ambao wangeiokoa ; unashangaa adi mtu mwenye miaka 65 and above na anaejua sheria na katiba anaogopa kusimama wakati wa mwanga na kutoa ukweli kwa ajili ya nchi yake.

Bora mngeumwa na wadudu mkiwa watoto mkafe ; hua niangalia watu kama Moi Torotich akina Njonjo and like walivyowanyanyasa akina Raila Odinga na maisha ya akina Odinga wa sasa nabaki kucheka tu.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Wakati mwingine unaweza kujisikia kizunguzungu ukiwasikiliza viongozi wetu ambao sasa wanaonekana “wanajua”. Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani amenukuliwa na gazeti moja akionesha kuunga mkono uamuzi wa Mahakama Kuu kutangaza kuwa mfumo unaowaweka viongozi au wanachama wa chama tawala kama wasimamizi wa uchaguzi ni kinyume na Katiba. Amedai kuwa tangu 1995 (akiwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi) walitoa mapendekezo ya kuondoa utaratibu huo. Lakini kwa miaka ishirini hilo halijatokea hadi hivi sasa.

Jambo ambalo linanitibua mimi zaidi ni kuwa Jaji huyu huyu ambaye anadai kuwa wana viongozi na mashabiki wa vyama vya siasa wasijiwekwe kusimamia uchaguzi alijitokeza 2015 akiwa amevaa magwanda ya CCM akitaka kugombea Urais chini ya mfumo ule ule ambao anadai wao hawakuupenda! Mfumo ambao anataka tuamini kuwa aliona hautakuwa wa haki (fair) kwa vyama vingine?

Sasa Jaji Ramadhani tafadhali bwana; hivi kama kweli ulijua kuwa mfumo huu ni mbaya kilichokufanya usimame na kutaka kugombea Urais kwa tiketi ya CCM ilikuwa ni nini? Unataka tuamini kuwa mapenzi yako kwa CCM yalikuja baada ya kuwa umeondoka Ujaji Mkuu? Je, haiwezekani kuwa kumbe mwenzetu tangu miaka “ile ya nineteen kweusi” ulikuwa ni mwanachama na shabiki wa CCM? Kwamba ulipokuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ulikuwa tayari na “mahaba” na chama tawala?

Kama hili ni kweli basi kuna mambo mawili; kwamba, unaamini kuwa kwa wewe kuwa na mapenzi au uanachama wa Chama cha Mapinduzi hakukufanya uvunje uadilifu wako wa kusimamia taratibu au sheria bila kujali mgombea anatoka chama gani. Kwamba, kama Augustino Mrema angeshinda mwaka 1995 wewe na wenzako mlikuwa tayari kumtangaza mshindi hata kama CCM ingeondoka madarakani? Je hili ni kweli?

Kama hili ni kweli unataka tuamini kuwa mwanachama wa chama cha siasa akisimamia na kuzingatia viapo vyake, maadili ya kazi, sheria na haki anaweza kusimamia uchaguzi bila kupendelea chama chake. Kwamba, ndio maana wapo wabunge wa vyama vya upinzani ambao wameshinda na kurudia kushinda kwenye majimbo yao licha ya wasimamizi wa majimbo hayo kuwa ama ni wanachama wa chama tawala au mashabiki wa chama hicho.
Jambo la pili ni kuwa kama hilo la kwanza si kweli basi ni wazi kuwa hukuwa mwadilifu na kuwa ulikuwa unafanya kazi kwa upendeleo ukiongozwa na mahaba kwa chama chako. Kwamba, kwa vile tunajua sasa kuwa wewe ulikuwa ni mwana CCM ulikuwa unafanya kazi kwa kificho kumbe moyoni ulikuwa na chama unachokipendelea kishinde.

Kama hili la pili ni kweli basi hoja yako ya kuwaondoa mashabiki na wanachama (walijionesha wazi) wa CCM kwenye kusimamia uchaguzi ni jambo la msingi, la lazima na ambalo haliepukiki. Hii ina maana kuwa siyo wana CCM tu bali Watanzania wote wanapaswa kushuku kila wakati na mara zote unapofanyika uchaguzi pale ambapo wasimamizi wa uchaguzi bado ni wana CCM. Kwamba, WAtanznaia na hasa wapinzani wasidhanie hata kwa mbali kuwa wakurugenzi hawa wa uchaguzi wanaweza kutenda haki.

Nikiangalia yote mawili naamini tatizo letu kubwa haliko kwenye uanachama wa wakurugenzi wa uchaguzi au watendaji wengine. Hii ni kwa sababu huwezi kuondoa mapenzi ya mtu kwa chama Fulani hata kama mtu huyo hatovaa gwanda hilo wakati akiwa kazini. Tatizo letu ni kutokuwa na mfumo ambao uko wazi, unaoneshimika na kila mtu na ambao kila mtu anaweza kuuamini kumtendea haki. Inapotokea kwamba wapinzani wanalazimika “kulinda kura” kwa kuhofia kuibiwa ni wazi kuwa mfumo hauko sawa na hauaminiki.

Badala ya kuhangaika na “uanachama” wa Wakurugenzi wa Uchaguzi naomba kupendekeza kwa heshima na taadhima tuangalia uadilifu wa watendaji – ikiwemo kuweka adhabu kubwa kwa mkurugenzi ambaye anaonekana kuharibu uchaguzi kwa sababu za kisiasa. Ni lazima tuangalie mfumo wa uchaguzi kuhakikisha kuwa wapinzani wanapata haki ile ile wanayopewa CCM. Haiwezekani wapinzani wanalazimika kutumia nguvu kubwa kweli hata kurudisha fomu za kugombea wakati CCM inaonekana wana mlango wao mwingine maalum.

Nitatoa mfano, Rais Magufuli alipozungumza (labda kwa utani au akimaanisha) kuwa yeye anateua wakurugenzi wa halmashauri halafu ati waje kumtangaza mgombea wa upinzani kashinda. Tulitarajia Tume ya Uchaguzi ingesimama na kutetea nafasi yake na kuwataka watendaji wake kutekekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na siyo matakwa ya siasa. Kama Rais Magufuli atawafukuza kazi wakurugenzi wa halmashauri kwa sababu wamemtangaza mpinzani hii ni haki na wajibu wake.

Ndio maana niliposoma habari ya kauli yako hii nimebakia kusema “Jaji Ramadhani, tafadhali bwana!”

Niandikie:mwanakijiji@jamiiforums.com
Mzee umeandika maneno mengi lakini sioni tija. Haijalishi jaji amesubiri muda gani bali kinachohusika ni je, ameongea ukweli ? Period
 
Back
Top Bottom