Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma katika Utendaji

Mkuu Ipara, usemayo ni kweli, wakati napita UDSM, nilikuta 1st Class ya mwisho ni ya Prof.Majamba ikiwa ni more than ten years na sasa it's more than 20 years now bado sijabahatika kusikia 1st class nyingine ya sheria, hivyo inawezekana
(a) Wanafunzi wa zamani walikuwa vichwa
(b) Wanafunzi wa zamani walisoma kwa bidii.
(c) Waalimu wa zamani walikuwa ni wazuri
(d) Waalimu wa zamani walifundisha kwa bidii.
(e) Wanafunzi wa sasa ni vilaza
(f) Wanafunzi wa sasa hawasomi kwa bidii.
(g) Waalimu wa sasa ni wabovu
(h) Waalimu wa sasa hawafundishi kwa bidii.
Paskali
 
Mzandiki na mzushi Mkubwa. Sijui lini tu bavicha mtaacha hiyo tabia
Hujui kitu mjomba utulie na kutazama tu , kwenye hili huna mchango wowote , waache wajuzi waendelee kutoa yaliyofichwa .
 
Toa mifano ya kesi amabazo ziliihusu Jamhuri dhidi ya Vyama Pinzani au kesi zenye mgongano wa masilahi kati ya serikali na wafanyabiashara au CCM na Wapinzani. Kubwabwaja bila mifano ni kupoteza muda na ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa
 
Mkuu Masanja Asante kwa kumtendea haki Prof. Ibrahim Juma, sisi wengine tumejaaliwa kuiona integrity ya mtu kwa macho tuu, hivyo watu wote wenye jicho la uoni wa ndani ya mtu, watakubaliana na mimi, Prof. Ibrahim Juma is a man of integrity and you can see it just by naked eyes!.

Pamoja na madudu yote ya rais Magufuli kukanyaga katiba lakini kuna machaguo anaongozwa na Mungu na ndio maana kati ya majina matatu aliyopelekewa, aliweza kumuona Prof. Juma.

Paskali
 
Mkuu Pasco, concern yangu si weledi au utaaluma wa mhusika

Nimefuatilia majadiliano kinachojitokeza ni kila mmoja kuja na tuhuma au sifa zake

Nafasi ya Jaji mkuu ni kubwa na inahitaji 'vetting' kwavile ni mhimili na unyeti wake

Ukifuatilia US sasa mawaziri rekodi zao zinapitiwa hadharani na bunge

Kwa Jaji wetu, kunapokuwa na doubt, kunaongeza doubt eneo lenye doubt tayari

Pili, Sijui unaongeleaje hili suala la Jaji mkuu Kukaimu nafasi hiyo. Maoni yako tafadhali
 
Mkuu Nguruvi3, hizo ni tuhuma za kutungwa tuu, kwa sababu kama ni ku disco, watu wengi sana tuu tumecheza disco na tukazipangua tukiwa ni watoto wa wakulima masikini na wenye njaa!. Bahati nzuri nilikuwa chuo kipindi cha tuhuma hizo na sii kweli, ila kitu ambacho kipo kwenye mamlaka ya baraza la seneti la chuo, lina mamlaka ya kuongeza points 2 za gratis kwa yoyote kama hizo point zitamuokoa na disco if idadi kubwa ya watahiniwa wamefeli somo hilo!, nakumbuka land law ya Prof. Fimbo ilizungusha wengi sana karibu nusu ya darasa, inapotokea ukawa na jina kubwa, chochote kizuri utakachofanya kinatafsiriwa kama preferential treatment kwa sababu ya jina lako. Usiziamini tuhuma hizo after all jamaa namfahamu sio kibonde wa kihivyo!.

Hili la kukaimu kiukweli ndio leo nasikia nafasi ya mkuu wa chombo cha dola ikikaimiwa as if amestaafu ghafla!. Tunamsubiria kaimu CDF, na Kaimu IGP!, nadhani hata ule mhimili kutakuwa na kaimu Katibu wake!.

Paskali
 
Jaji mzuri niyule anaehukumu kwahaki kisheria hatakàma ukishinda kesi zote haijalishi. Mahakama zatanzania haziko huru tunahitaji Uhuru ili tuiamin

baharia Ar: ninafuatilia na kusoma kwa umakini mjadala huu, hakika umejaa kila aina ya lugha na taaluma.

Bado kuna maswali yanayohitaji tafsiri ya Katiba kutokana na hoja nzito za wanaJF, kama ya kwako:
1) Madaraka ya kuteua Jaji Mkuu na majaji wengine! - Rejea Sehemu ya Pili na ya Tatu ya Katiba JMT (1977).
2) Mamlaka ya kuchunguza na kudhibiti vitendo vya majaji - Rejea Sehemu ya Tano ya Katiba ya JMT.
3) Hatua gani zichukuliwe kulinda na kusimamia uhuru wa mahakama - Rejea Sehemu ya Kwanza ya Katiba JMT.

Wataalamu wa "constituional law" watujuze, kabla ya kusakama utendaji wa mahakama au watumishi wake, hasa majaji.
 
Mkuu kama nilivyosema tuhuma au sifa si tatizo ninaloliona

Ninachokiona ni kupata mtu wa mhimili bila vetting. Huyu ni mtu muhimu sana hivyo rekodi yake inapaswa kuwa public,akipewa nafasi ya kuhoji au kuhojiwa
Kwasasa system yetu hairuhusu hilo, ndipo wasi wasi ulipo

Kuhusu kukaimu, hii nafasi kweli inahitaji kukaimu?
Nilisema jana, kukaimu kuna mweka katika conflict of interest kati ya taasisi na matarajio yake kama mwanadamu na mtumishi.

Jaji Othman alijulikana anastaafu, hivi tunahitaji mtu wa kukaimu kweli!

Kama ulivyosema tumekuwa na wakuu wa vyombo wanaokaimu. Kama sikosei DCI anakaimu. Hili linaleta utata sana katika utendaji wao. Ni kuwafunga mikono kama si kuwaweka chini ya.

Ikitokea jambo linalohusu CCM, maamuzi yake yanamgusa Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais na mteuzi wa kaimu Jaji mkuu.
 
Kwangu hili la kukaimu halina tatizo, vetting imefanywa vema tuu, ila final vetting ni ya kwenye field, mkanyaga katiba kaikanyaga aliyepaswa kukemea kawekwa kwapani, huyu Jaji Juma sio mtu wa mchezo mchezo hivyo huwezi kumletea ujinga ujinga akakubali tuu hivyo dawa ni kumkaimisha na kuridhika kwanza if he will dance to the tune ya mpiga zumari, if not, atawekwa pembeni atafutwe mcheza muziki mahiri.

Paskali
 
"Pascal Mayalla, post: 19357352, member: 17813"]Kwangu hili la kukaimu halina tatizo,
Hili ni tatizo kubwa sana. Kwanini nafasi ya Jaji mkuu iwe ya kukaimu?
Ina maana hawakujua Othman anastaafu?

Na kukaimu kwa mujibu wa katiba yetu mbovu ya 1977 inamweka wapi ikitokea isivyotarajiwa?
vetting imefanywa vema tuu, ila final vetting ni ya kwenye field,
Well kwa mfumo wa sasa ni njema, katika uhalisia ilitakiwa indepedent body kumthibitisha.

Nafasi kama hizi si za uteuzi tu kama wenyeviti wa chama.

Ndiyo maana walikataa katiba mpya
Huyu Jaji Juma sio mtu wa mchezo mchezo hivyo huwezi kumletea ujinga ujinga akakubali tuu
Kuna mhimili uliozama zaidi kwenda chini, atauweza?
Dawa ni kumkaimisha na kuridhika
Je wasiporidhika kuwa hatekelezi maagizo au hafikii matarajio yao yakiwemo ya kisiasa huoni ni njia ya kumweka njia panda
kwanza if he will dance to the tune ya mpiga zumari, if not, atawekwa pembeni atafutwe mcheza muziki mahiri.
Kwa mfumo wetu ambao wewe ulikuwepo ikisema 'kuna mhimili uliozama' na '' maagizo kutoka juu'' unatarajia ana 'guts' gani kama mwanadamu kusimama taasisi na kujisimamia

The system is broken, tuna mhimili mmoja tu.Mingine ni kama matawi tu
 
Hujui kitu mjomba utulie na kutazama tu , kwenye hili huna mchango wowote , waache wajuzi waendelee kutoa yaliyofichwa .
Shida yenu bavicha mnapenda sana uzushi na uongo. Prof. Juma hamumjui kwa lolote ila tu mnataka mumzushie uongo nyoyo zenu zifurahi. Hivi Saanane kapatikana?
 
Shida yenu bavicha mnapenda sana uzushi na uongo. Prof. Juma hamumjui kwa lolote ila tu mnataka mumzushie uongo nyoyo zenu zifurahi. Hivi Saanane kapatikana?
Tatizo unauchukulia uzi huu kama wa jana , hebu angalia uliandikwa lini
 
Kwani jaji mzuri ni yule anayeiangusha serikali?

Ama kweli wengine vichwa vyenu mnatumia kufugia nywele!
Taratibu mkuu,usiwe na hasira na mleta mada hebu mpinge kwa hoja,samahani lakini ni hayo tu.
 
Ni Kada wa CCM ngoja niwawekee kadi namba yake
Teh,teh,teh,namkumbuka naibu wa mjengoni wabunge walipombananisha kwa kuwa na kadi ya chama tawala,kisomo hakikumsaidia kujibu swali hilo akawa mdogo kama zile dawa ziletazo usingizi.
 
Teh,teh,teh,namkumbuka naibu wa mjengoni wabunge walipombananisha kwa kuwa na kadi ya chama tawala,kisomo hakikumsaidia kujibu swali hilo akawa mdogo kama zile dawa ziletazo usingizi.
Na hatokaa aisahau siku ile .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…