Jaji Mutungi,usisahau barua yako

Jaji Mutungi,usisahau barua yako

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,usiisahau barua yako uliyoiandika CHADEMA 'kumzuia' Mbowe kugombea uenyekiti.

Ushindi wake umetuchanganya. Ushindi wake ni kushindwa kwetu. Ushindi wake ni maumivu yetu kimkakati kuelekea 2015. Ikumbuke na usijali mwaliko wao.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Adui akikuchagulia siraha ya kukabirina nae ujue anakutakia akushinde.

Mutungi ni mlezi wa vyama lakini hakuchaguliwa na vyama, aliteuliwa na ccm.

Aone aibu kujiita mlezi wa vyama vyote kwa usawa wakat ni zao la ccm.
Ni ushamba, ningekuwa mm ningejiudhuru fasta na kuda katba mupyaaa
 
mpaka uchaguzi wa elfu 2015 tutaona mengi,hizi propaganda za njaa zitatufikisha pabaya.nadhan mpangilio wa uchaguzi cdm uwefundisho maana ulikuwa wazi kila kitu tumekiona kwenye tv!
 
Sio kusahau tu; bali pia Jaji Francis Mutungi anajuta kuwahi kuiandika barua ile! maana kama alikuwa sahihi kwa maandishi yale basi alistahili kuukataa mwaliko wa CDM outright kwa sababu alikuwa na kila sababu ya kuona wazi kwamba Kmnd Mbowe alikuwa anakwenda kuchaguliwa kwa muhula wa tatu kwa kishindo kuendelea kuwa mwenyekiti wa CDM.

Na kama ulimuangalia vizuri jana pale ukumbini; Mlimani City akitokwa na kijasho chembamba na kukosa cha kuongea; uso umemshuka kwani kazi aliyotumwa na paymaster wake imemshinda na pale ukumbini alikuwa anapewa kavu kavu za uso mpaka anajiinamia tu kijana wa watu; akabaki mdomo wazi!

No wonder amewahi kutamka kwamba "asichonganishwe na CDM"
 
Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,usiisahau barua yako uliyoiandika CHADEMA 'kumzuia' Mbowe kugombea uenyekiti.

Ushindi wake umetuchanganya. Ushindi wake ni kushindwa kwetu. Ushindi wake ni maumivu yetu kimkakati kuelekea 2015. Ikumbuke na usijali mwaliko wao.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Alishajibiwa na Tendwa kuwa ajaribu kuangalia makabati ofisini kwake vizuri atapata majibu.
 
Barua aliandika Mwigulu na Mwigamba yeye alipewa tu kupeleka kosa lake liko wapi?
 
na alienda kutoa salamu. hahaha!! siasa bhana..

huyu jamaa hana aibu kwa kweli kama mimi ningemtuma msaidizi wangu au mwakilishi
ila hakuna adui wala rafiki wa kudumu kwenye siasa
 
Nilishangaa sana UJASIRI wa Judge Francis Mutungi kuhudhuria mkutano huo wa CDM, bila aibu eti naye akatoa salama kwa wajumbe wa mkutano mkuu! Yaani nchi hii viongozi wetu hawaishi vituko.
 
Ukiambiwa jambo lazima usahau kwa haraka sana,maamuzi aliambiwa ndo maana alisahau na akajikuta yupo kwenye mwaliko japokua alikumbushiwa na bosi wake masaa machache kabla ya tukio.
 
Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,usiisahau barua yako uliyoiandika CHADEMA 'kumzuia' Mbowe kugombea uenyekiti.

Ushindi wake umetuchanganya. Ushindi wake ni kushindwa kwetu. Ushindi wake ni maumivu yetu kimkakati kuelekea 2015. Ikumbuke na usijali mwaliko wao.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

kumbe kwenye sakata hilo mlimtumia ?
 
Ukiambiwa jambo lazima usahau kwa haraka sana,maamuzi aliambiwa ndo maana alisahau na akajikuta yupo kwenye mwaliko japokua alikumbushiwa na bosi wake masaa machache kabla ya tukio.

Jamani kumbe si kweli kuwa kila mtu anaweza kujadiri siasa. Sasa mtungi kwenda kwenye mkutano tatizo ni nini? Na uchaguzi kurushwa live haimanishi kuwa Demokrasia. Buyers of events.
 
SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kuwekewa pingamizi la kutogombea nafasi hiyo kwa awamu ya tatu, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, amesema kinachotokea kwenye chama hicho ni matokeo ya kupuuza ushauri wake.

Mbowe amewekewa pingamizi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Tabora, Kansa Mbarouk, ambaye pia ni mgombea wa nafasi hiyo, kwa madai ya kukiuka katiba ya chama hicho na maagizo ya msajili wa vyama vya siasa.

Akizungumza na MTANZANIA jijini Dar es Salaam jana, Jaji Mutungi alisema kuwa ofisi yake iliwashauri viongozi wa chama hicho kuhitisha mkutano wa Kamati Kuu ili waweze kufanya marekebisho ya Katiba yao kabla ya uchaguzi, lakini walipuuza ushauri wake.

Alisema kuwa baada ya ushauri wake huo kupuuzwa, Mbarouk ameona fursa hiyo na kuamua kuitumia.

“Tuliwashauri Chadema muda mrefu kuhitisha mkutano wa Kamati Kuu ili wafanye marekebisho ya Katiba yao, lakini walitupuuza na kuanza kutulaumu. Kinachotokea sasa ni matokeo ya kile ambacho tulijua kinaweza kutokea katika uchaguzi wao,” alisema Jaji Mutungi.

Alisema baada ya kuwaambia hayo, viongozi wa chama hicho waliishutumu ofisi ya msajili na kudai kuwa inatumika.

Jaji Mutungi alisema kutokana na hali hiyo, ofisi yake imeamua kukaa kimya na kuacha mchakato wa uchaguzi uendelee, lakini mwishowe wanatakiwa kuwasilisha taarifa zao katika ofisi hiyo.

“Tumeamua kuwaacha waendelee na mchakato wao, watavutana mwisho watachoka wakimaliza watatufuata,” alisema.

Mbarouk aliwasilisha taarifa yenye kumbukumbu namba Mbarouk/UCH/14 kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chadema na Msajili wa Vyama vya Siasa ambayo inasema kuwa kufikia Septemba 14, siku ya uchaguzi mkuu wa chama hicho, Mbowe atakuwa ametumikia vipindi viwili katika nafasi ya mwenyekiti taifa.

Kulingana na Katiba ya Chadema kama ilivyothibitishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, hakuna mwanachama anayeruhusiwa kuchaguliwa kuongoza zaidi ya vipindi viwili katika cheo kimoja na ngazi moja.

Juni mwaka huu, msajili alidai kuwa Mbowe hawezi kuwania nafasi hiyo kutokana na Katiba yao kuwa na kipengele cha ukomo wa uongozi wa vipindi viwili.

Alisema ili aweze kuendelea na nafasi hiyo, alipaswa kuitisha mkutano wa Kamati Kuu ili waweze kufanya marekebisho katika Katiba yao ikiwa ni pamoja na kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi.

Katika hatua nyingine, chama hicho kimesema hakijapata taarifa za Mbowe kuwekewa pingamizi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho jana, Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi, Singo Benson, alisema kulingana na Katiba ya chama hicho walioomba kuteuliwa kama wana pingamizi au malalamiko wanapaswa kupeleka ofisini, lakini hawajapokea hadi sasa.

“Sisi tumesoma tu kwenye magazeti, hatuna taarifa yoyote ya pingamizi hadi sasa. Huyo anayesema alileta je, alilileta kwa njia gani na kama ‘dispatch’ ipo, aseme nani alipokea na kusaini,” alisema Benson.

Alisema ofisi ya chama hicho iko wazi muda wote na kwamba kwa siku ya juzi alikuwapo ofisini hadi saa 5 usiku, lakini hakupokea pingamizi la aina yoyote.

Wakati huo huo, chama hicho jana kiliwatangaza washindi wa uchaguzi wa Baraza la Wazee Taifa.

Nafasi ya mwenyekiti ilichukuliwa na Hashim Juma Issa kutoka Zanzibar, Makamu Mwenyekiti Bara ni Suzan Lyimo na Makamu Mwenyekiti Zanzibar ni Omar Masoud Omar.

Wengine ni Rodrick Lutembeka ambaye alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu na Erasto Gwota aliyechaguliwa kuwa Mweka Hazina.
 
Back
Top Bottom