Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,745
Jaji Mutungi avitaka vyama kutosusia chaguzi.
Na Mary Geofrey
27th January 2016
B-pepe
Chapa
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, ameviasa vyama vya siasa kushiriki chaguzi zinazotangazwa, ikiwamo uchaguzi wa marudio wa Zanzibar uliopangwa kufanyika Machi 20, mwaka huu na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
Kwa mujibu wa barua ya Jaji Mutungi aliyoviandikia vyama vya siasa jana na msingi wa Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 inasisitiza vyama vya siasa kushiriki chaguzi zote zinazotangazwa na tume za uchaguzi ili kufikia malengo yake ya kushika dola.
Katika barua hiyo, Jaji Mutungi alisema kwa chama cha siasa kinachoamini misingi ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa, hakuna njia mbadala ya kufikia malengo yake zaidi ya kushiriki chaguzi.
“Ni wajibu wa kila chama cha siasa nchini kama wakala wa kukuza demokrasia, utawala wa sheria na amani ya nchi kuwa wa kwanza kutii matamko ya kisheria yanayotolewa na mamlaka husika,” ilisema.
Alisema kama kuna chama cha siasa ambacho hakiridhiki au kimekwazwa kwa njia moja au nyingine na suala lolote kuhusu masuala ya uchaguzi, njia stahiki na inayonyesha ukomavu wa kisiasa si kuhamasisha kugomea uchaguzi, bali ni vema kikafuata utaratibu uliowekwa katika sheria za uchaguzi.
Jaji Mutungi alisema japokuwa kwa mujibu wa sheria za nchi ni suala la hiari kwa chama kushiriki uchaguzi, lakini utashi huo wa hiari unaenda sanjari na umuhimu wa kila chama kushiriki kila uchaguzi unaotangazwa na tume ya uchaguzi.
“Hivyo ni muhimu basi kila chama cha siasa kuelewa kuwa uchaguzi ni kipimo cha uhai wake kisiasa. Chama cha siasa kisiposhiriki uchaguzi kinaua uhai wake katika mtazamo wa harakati za kisiasa,” ilisema.
Tamko hilo la Jaji Mutungi limekuja siku chache baada ya Mkurugenzi wa ZEC, Jecha Salum Jecha, kutangaza marudio ya uchaguzi uliofutwa Zanzibar kutokana na kubainika kasoro mbalimbali yatafanyika Machi 20. mwaka huu.