mafutamingi
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 2,773
- 2,182
Juzi Msajili wa Vyama vya siasa Jajio Mutungi alikaririwa akikiasa chama kikuu cha upinzani Zanzibar CUF kutosusia uchaguzi unaotarajiwa kurudiwa hivi karibuni.
Alikaririwa akisema kwa kuwa ZEC imetangaza tarehe ya kurudiwa uchaguzi huo ni vyama CUF wakashiriki. Mimi nadhani Jaji Mutungi anaingiza siasa katika majuku yake.
Uchaguzi unarudiwa kwa kuwa ZEC "ilifuta" uchaguzi uliofanyika Oct 2015, uchaguzi ambao watazamaji wa nje na ndani walisema ulikuwa huru na wa haki.
Napenda kumwuliza Jaji Mutungi, je ZEC walifuta uchaguzi huo kwa kutumia sheria gani? Kama ZEC walikuwa sahihi, kwa nini Mutungi hakutoa tamko la kuwaunga mkono?
Alinyamza kimya hadi anaibuka leo wakati ZEC imetangaza tarehe ya kurudia uchaguzi! Namshauri Jaji Mutungi aache kuingiza siasa katika mambo ya sheria hasa ukizingatia kwama yeye ni Jaji.