Uchaguzi 2020 Jaji Mutungi avitaka Vyama vya Siasa kuheshimu Sheria na Taratibu za Uchaguzi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,867

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa vyama vya siasa na wadau wote kuheshimu Sheria na Taratibu za Uchaguzi kama zilivyoainishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, katika kikao kati ya viongozi wa vyama vya siasa amesema “hiki si kikao cha kuja kusutana ila ni kikao cha kuja kuongea na kuangalia mwelekeo unavyokwenda kwenye kampeni, lakini pia nafasi ya Msajili kama mlezi nikaona nisiwanyime hiyo nafasi ya kukutana nanyi na kuwapa maneno mawili ya kuwakumbusha wajibu wenu.”

Jaji Mutungi amewaomba wagombea pamoja na wadau wa vyama vya siasa kuimarisha Demokrasia ya nchi kwa kufanya siasa za kistaarabu ambapo amewataka wagombea washindane kwa ustaarabu huku wakifuata sheria na taratibu za nchi.

Aidha ameeleza kuwa mtu yoyote atakayeonekana kwenda kinyume na maelekezo na taratibu za Uchaguzi atachukuliwa hatua kulingana na taratibu zilizowekwaza uchaguzi Mkuu 2020

“Tuachane na ile dhana ya kwamba mtu anasema wakiniacha wananiogopa, wakinishughulikia wananionea, sasa huu ujumbe ninaousema uende pande zote, na sisi taasisi ambazo zimepewa mamlaka ya kusimamia utekelezaji wa hii sheria, tuisimamie kwa haki kwa sababu tusipofanya hivyo tunaweza sababisha tafarani” amesisitiza.
 
Lissu anaharibu maadili ya Uchaguzi ili akamatwe.

Tume imuache huyu hadi Uchaguzi uishe ndio akumbane na mkono wa sheria.
 
Kama mnaweza Kwa nini mnatisha nyau? Kaeni kimya halafu mfanye basi, mbona sasa mnaongea sana. Tit fir tart is essential
 
Huyu jaji anatia aibu hata kabila lake! Wahaya hawako hivyo ati! Wewe unakiuka maadili, unawaacha CCM wanavunja sheria za uchaguzi kana kwamba huoni, halafu unajitia kuongelea eti watu waheshimu sheria za uchaguzi! Potea huko!
 
Sehemu ya mbeleko za chama mbogamboga kazini
 
Safari hii mtatema tu ndowano, Lissu siyo kama ilivyokuwa kwa Lowassa maana mzee Lowassa alikuwa akiitwa na jeshi la polisi ilikuwa mpaka amuulize mbowe, sasa kwa TL ni tofauti anakwenda kwa vifungu vya sheria.
 
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa vyama vya siasa na wadau wote kuheshimu Sheria na Taratibu za Uchaguzi kama zilivyoainishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, katika kikao kati ya viongozi wa vyama vya siasa amesema “hiki si kikao cha kuja kusutana ila ni kikao cha kuja kuongea na kuangalia mwelekeo unavyokwenda kwenye kampeni, lakini pia nafasi ya Msajili kama mlezi nikaona nisiwanyime hiyo nafasi ya kukutana nanyi na kuwapa maneno mawili ya kuwakumbusha wajibu wenu.”

Jaji Mutungi amewaomba wagombea pamoja na wadau wa vyama vya siasa kuimarisha Demokrasia ya nchi kwa kufanya siasa za kistaarabu ambapo amewataka wagombea washindane kwa ustaarabu huku wakifuata sheria na taratibu za nchi.

Aidha ameeleza kuwa mtu yoyote atakayeonekana kwenda kinyume na maelekezo na taratibu za Uchaguzi atachukuliwa hatua kulingana na taratibu zilizowekwaza uchaguzi Mkuu 2020

“Tuachane na ile dhana ya kwamba mtu anasema wakiniacha wananiogopa, wakinishughulikia wananionea, sasa huu ujumbe ninaousema uende pande zote, na sisi taasisi ambazo zimepewa mamlaka ya kusimamia utekelezaji wa hii sheria, tuisimamie kwa haki kwa sababu tusipofanya hivyo tunaweza sababisha tafarani” amesisitiza.
Huyu mutungi anadhalilisha wadhifa wa u-jaji..

Mbona hajawahi kumuonya pombe na wenzie kwa uovu mwingi wanaofanya?
 
Lissu anaharibu maadili ya Uchaguzi ili akamatwe.

Tume imuache huyu hadi Uchaguzi uishe ndio akumbane na mkono wa sheria.
Tundu Lissu ni untouchable - iwe kabla au baada ya uchaguzi, iwe kachaguliwa urais ama vinginevyo.

inabidi MATAGA mjifunze tu kuishi na Lissu kama Lissu (akiwa rais au vinginevyo)!
 
MATAGA wootee akili wameuza! Sielewi mtu anayejifanya haoni uhuni unaoendelea sasa hivi; wala uhitaji kuwa mpinzani kuona maovu yanayotendwa na Mutungi na genge lake, wakiongoza nayule anayewatuma!
 
Hujitambui! Tatizo MATAGA hivyo vijisenti mnapewa mnaviona vya maana hadi vinawatoa ufahamu; subiri uchaguzi uishe ndo mtagundua mmetumika tu kama TP!
 
Kama kweli huyu Mutungi anamaanisha anachonena, ampe onyo Rais Magufuli na CCM kwa kukiuka mara nyingi maadili ya uchaguzi. Vinginevyo ni asanii mtupu, hana tofauti na Mahera.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa vyama vya siasa na wadau wote kuheshimu Sheria na Taratibu za Uchaguzi kama zilivyoainishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, katika kikao kati ya viongozi wa vyama vya siasa amesema “hiki si kikao cha kuja kusutana ila ni kikao cha kuja kuongea na kuangalia mwelekeo unavyokwenda kwenye kampeni, lakini pia nafasi ya Msajili kama mlezi nikaona nisiwanyime hiyo nafasi ya kukutana nanyi na kuwapa maneno mawili ya kuwakumbusha wajibu wenu.”

Jaji Mutungi amewaomba wagombea pamoja na wadau wa vyama vya siasa kuimarisha Demokrasia ya nchi kwa kufanya siasa za kistaarabu ambapo amewataka wagombea washindane kwa ustaarabu huku wakifuata sheria na taratibu za nchi.

Aidha ameeleza kuwa mtu yoyote atakayeonekana kwenda kinyume na maelekezo na taratibu za Uchaguzi atachukuliwa hatua kulingana na taratibu zilizowekwaza uchaguzi Mkuu 2020

“Tuachane na ile dhana ya kwamba mtu anasema wakiniacha wananiogopa, wakinishughulikia wananionea, sasa huu ujumbe ninaousema uende pande zote, na sisi taasisi ambazo zimepewa mamlaka ya kusimamia utekelezaji wa hii sheria, tuisimamie kwa haki kwa sababu tusipofanya hivyo tunaweza sababisha tafarani” amesisitiza.
Huyo mzee mpuuzi niaje?
 
Back
Top Bottom