Kimwakaleli
JF-Expert Member
- Apr 16, 2018
- 15,331
- 22,312
Jaji mkuu wa Tanzania, prof. Ibrahim Juma, amewataka mawakili wa serikali kutafuta suluhu ya kesi nje ya Mahayana badala ya kung'ang'ania mahakamani wakati wakijua hawawezi kushinda. Prof. Juma, aliyasema hayo wakati wa mkutano wa pili uliowakutanisha mawakili 900 jijini Dodoma. Haya mambo yamekuwa yakiighalimu serikali, lakini pia usumbufu kwa wathirika wa kesi zinapokuwa mahakamani, hii husababisha wengi wa waathirika kufa kwa msongo wa maisha. Si wa serikali tu hata kwenye mashirika ambayo serikali ina hisa zake huko, mfano mzuri ni kesi ya BOT na wafanyakazi waliofukuzwa zaidi ya miaka ishirini wangekubali kuyamaliza nje ya mahakama zingekuwa si kubwa Sana. Wanasheria na wadau naomba michango yenu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app