Jaji Mkuu: Acheni kulalamika chukueni hatua.

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
8,099
2,000
Kauli hii ya Jaji wetu Mkuu ina maneno machache sana lakini ina ujumbe mkubwa sana kwa watanzania wote. Watu wamezoea kulalamikia uvunguni, sitting room, maofisizi, kazini, barabarani, vijiweni, mitaani, mikutanoni vitendo vya uvunjifu wa sheria na Katiba bila kuchukua hatua za kisheria na kikatiba kuzuia ukiukwaji huo ambao unaonekana wazi hata machoni kwa Jaji Mkuu.

Nadhani wasomi wetu ambao tumewasomesha kwa kodi zetu ndio zimwi linalotutafuna na tuangusha sisi ambao hatujapata bahati ya kupata elimu kama wao. Wasomi wetu wanatumia elimu tuliowapatia kwa maslahi yao binafsi, familia na marafiki zao na kuyasahau maslahi mapana ya taifa na wanataifa. Wao ndio wanaofahamu namna mwananchi anavyoweza kushiriki katika kuchukua hatua pale sheria zinapovunjwa na watendaji tuliowapa madaraka na mamlaka ya kutwatumikia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom