Isaya Nehemia
JF-Expert Member
- Jun 6, 2013
- 555
- 452
Kwan kiongozi kukaa madarakini kwa muda mrefu au umasiki wa wananchi wake ndo udikteta kwa maoni yako. Kwa hiyo na Nyerere naye alikuwa dikteta?
Jaji Mihayo, usiingize siasa mahakamani.
Kuna madikteta wengi tu Afrika. Nashangaa msomi kama wewe unashindwa kujua hilo.
Hawa ni baadhi ya madikteta Afrika:
1. Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo
Nchi : Equatorial Guinea
Madarakani: Tangu August 1979
Kampindua mjomba wake Francisco Macías Nguema.
Equatorial Guinea ina utajiri wa mafuta lakini pesa yote anaiba yeye na familia yake. Wananchi wanakufa na njaa.
2. José Eduardo dos Santos
Nchi: Angola
Madarakani: Tangu September 1979 alipokufa Rais Agostinho Neto.
Binamu yake ni makamu wa Rais.
Mtoto wake wa kike, Isabel, ni bilionea wa kwanza wa kike Afrika.
Angola Ina utajiri wa mafuta na almasi lakini wananchi wake wanakufa na njaa. Ukiishi zaidi ya miaka 41, unabahati.
Familia ya Rais Dos Dantos, inamiliki makampuni mingi katika uchumi wao mpaka kuweza mtoto wake Isabel kununua share katika mabenki na makampuni ya magazeti makubwa ya Ureno.
3. Rais Robert Mugabe
Nchi: Zimbabwe
Madarakani: Tangu 1980 (Waziri Mkuu, Rais wa Nchi 1987)
Asilimia 60 ya wananchi hawana kazi, wengi wanakimbilia Afrika Kusini kutafuta kazi.
Baada ya kutaifisha ardhi iliyokuwa inalimwa na raia wa kizungu wa Zimbabwe, uchumi ukashuka. Wakulima Wazawa wakashindwa kuitumia ardhi vizuri kutokana na sababu za kifedha na kielimu.
Sasa nchi inaomba msaada wa chakula nje na vyakula ni adimu madukani.
Pia, wapinzani wake wamebanwa koo na serikali yake.
4. Mfalme Mswati III
Nchi: Swaziland
Madarakani: Tangu 1986
Wananchi wake wanaishi miaka 46, wengi wanakufa na ukimwi na njaa. Asilimia 40 hawana kazi.
Mfalme ndiyo Mkuu wa Nchi. Hamna kura ya kuchagua kiongozi.
Mswati anatumia fedha za Nchi kama za kwake. Anajulikana zaidi duniani kama mpenzi wa magari ya BMW na huowa karibu kila miaka michache. Ana wake 14.
5. Rais Omar Al-Bashir
Nchi : Sudan
Madarakani: Tangu 1989 baada ya kumpindua Sadiq al- Mahdi.
Vita nchini vimeua watu milioni moja na maonevu dhidi ya raia wa Kiafrika wa Kusini mwa Sudan imesababisha Sudan kugawanyika mwaka 2011 na kuwa Sudan na Sudan ya Kusini baada ya raia hao kupigana vita na serikali ili wapate haki zao.
Wananchi wa Sudan hawana haki yoyote chini ya serikali yake ya chama kimoja, National Islamic Front. Wabunge wake wote 500 ni wa kuteuliwa.
Bado sijaongeza kina Museveni, Kagame na Nkurunziza.
Listi ni ndefu mno.