Tokyo40
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 2,065
- 1,926
Wale wa East Africa umewasahau mkuu
Wapo chini Mkuu. Siwezi kuwasahau kina Kagame na Nkurunziza.
Wale wa East Africa umewasahau mkuu
Naombeni kueleweshwa; hivi kipimo cha udikteta ni kukaa madarakani muda mrefu au matendo yako ya kiungozi? Kama issue ni time frame nashangaa kwanini hawa wana miss kwenye list yako Kagame, M7, Malkia Elizabeth, mfalme wa Saudi Arabia, Jordan nk, au tunakaririshwa tu na wazungu, kiongozi akigombana na wazungu hasa Wamagharibi then na sisi tunamwita dikteta?
Burundi, uganda, rwanda haziko A.Mashariki? maana huko kuna madikteta au unafikiri kuwa Dikteta ni lazima uuwe raia wako?Amesema Afr
Amesema Africa Mashariki na sio Africa kwa ujumla
Dikteta hapimwi kwa muda aliokaa madarani tu.
Jaji Mihayo, usiingize siasa mahakamani.
Kuna madikteta wengi tu Afrika. Nashangaa msomi kama wewe unashindwa kujua hilo.
Hawa ni baadhi ya madikteta Afrika:
1. Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo
Nchi : Equatorial Guinea
Madarakani: Tangu August 1979
Kampindua mjomba wake Francisco Macías Nguema.
Equatorial Guinea ina utajiri wa mafuta lakini pesa yote anaiba yeye na familia yake. Wananchi wanakufa na njaa.
2. José Eduardo dos Santos
Nchi: Angola
Madarakani: Tangu September 1979 alipokufa Rais Agostinho Neto.
Binamu yake ni makamu wa Rais.
Mtoto wake wa kike, Isabel, ni bilionea wa kwanza wa kike Afrika.
Angola Ina utajiri wa mafuta na almasi lakini wananchi wake wanakufa na njaa. Ukiishi zaidi ya miaka 41, unabahati.
Familia ya Rais Dos Dantos, inamiliki makampuni mingi katika uchumi wao mpaka kuweza mtoto wake Isabel kununua share katika mabenki na makampuni ya magazeti makubwa ya Ureno.
3. Rais Robert Mugabe
Nchi: Zimbabwe
Madarakani: Tangu 1980 (Waziri Mkuu, Rais wa Nchi 1987)
Asilimia 60 ya wananchi hawana kazi, wengi wanakimbilia Afrika Kusini kutafuta kazi.
Baada ya kutaifisha ardhi iliyokuwa inalimwa na raia wa kizungu wa Zimbabwe, uchumi ukashuka. Wakulima Wazawa wakashindwa kuitumia ardhi vizuri kutokana na sababu za kifedha na kielimu.
Sasa nchi inaomba msaada wa chakula nje na vyakula ni adimu madukani.
Pia, wapinzani wake wamebanwa koo na serikali yake.
4. Mfalme Mswati III
Nchi: Swaziland
Madarakani: Tangu 1986
Wananchi wake wanaishi miaka 46, wengi wanakufa na ukimwi na njaa. Asilimia 40 hawana kazi.
Mfalme ndiyo Mkuu wa Nchi. Hamna kura ya kuchagua kiongozi.
Mswati anatumia fedha za Nchi kama za kwake. Anajulikana zaidi duniani kama mpenzi wa magari ya BMW na huowa karibu kila miaka michache. Ana wake 14.
5. Rais Omar Al-Bashir
Nchi : Sudan
Madarakani: Tangu 1989 baada ya kumpindua Sadiq al- Mahdi.
Vita nchini vimeua watu milioni moja na maonevu dhidi ya raia wa Kiafrika wa Kusini mwa Sudan imesababisha Sudan kugawanyika mwaka 2011 na kuwa Sudan na Sudan ya Kusini baada ya raia hao kupigana vita na serikali ili wapate haki zao.
Wananchi wa Sudan hawana haki yoyote chini ya serikali yake ya chama kimoja, National Islamic Front. Wabunge wake wote 500 ni wa kuteuliwa.
Bado sijaongeza kina Museveni, Kagame na Nkurunziza.
Listi ni ndefu mno.
Udikteta wa Mugabe uko wapi hapo?
Kwamba alichukua ardhi ya wazungu na kuwapa wazawa ambao wameshindwa kuiendeleza kwa kukosa elimu na utalaam wa kilimo ndiyo udikteta wenyewe?
Kama ndivyo, basi tuna safari ndefu. Ukumbuke kuwa wazungu wanafanya kila njama ili wazawa waliopewa ardhi wasifanikiwe. Wazungu maana yake ni nchi za magharibi wakiongozwa na Uingereza.
Ufumbuzi suala la ardhi Zimbabwe sio kuirejesha kwa wazungu, bali kuwawezesha wazawa walime kwa ufanisi.
Ukisoma habari kwenye vyanzo vya nchi za Ulaya hasa Uingerezabila kuongeza za kwako hilo ndiyo logical answer.Wazawa wamepewa ardhi, imewashinda. Hawana uwezo wala utaalamu. Mimi pia napendelea Wazawa wapewe ardhi lakini kwanza wawe tayari, siyo kukurupuka.
Angependa haki, azingewaumiza na kuwabana koo wapinzani wake. Angeheshimu haki ya wananchi wa Zimbabwe ya kutawaliwa na viongozi waliowachagua kihalali kwa njia ya kura.
Hamna mtu yoyote mwenye akili timamu anaweza kuamini Mugabe, kiongozi wa umri wa miaka 91, kachaguliwa kihalali.
Lakini kila kitu kina mwisho wake.
View attachment 322179
Ukisoma habari kwenye vyanzo vya nchi za Ulaya hasa Uingerezabila kuongeza za kwako hilo ndiyo logical answer.
Wananchi wa Zimbabwe wanajua zaidi.
Ukisema wazawa wasipewe ardhi hadi wawe tayari kui manage, haitatokea hata siku moja. Mkakati uwe kuwawezesha sasa.
Jaji Mihayo, usiingize siasa mahakamani.
Kuna madikteta wengi tu Afrika. Nashangaa msomi kama wewe unashindwa kujua hilo.
Hawa ni baadhi ya madikteta Afrika:
1. Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo
Nchi : Equatorial Guinea
Madarakani: Tangu August 1979
Kampindua mjomba wake Francisco Macías Nguema.
Equatorial Guinea ina utajiri wa mafuta lakini pesa yote anaiba yeye na familia yake. Wananchi wanakufa na njaa.
2. José Eduardo dos Santos
Nchi: Angola
Madarakani: Tangu September 1979 alipokufa Rais Agostinho Neto.
Binamu yake ni makamu wa Rais.
Mtoto wake wa kike, Isabel, ni bilionea wa kwanza wa kike Afrika.
Angola Ina utajiri wa mafuta na almasi lakini wananchi wake wanakufa na njaa. Ukiishi zaidi ya miaka 41, unabahati.
Familia ya Rais Dos Dantos, inamiliki makampuni mingi katika uchumi wao mpaka kuweza mtoto wake Isabel kununua share katika mabenki na makampuni ya magazeti makubwa ya Ureno.
3. Rais Robert Mugabe
Nchi: Zimbabwe
Madarakani: Tangu 1980 (Waziri Mkuu, Rais wa Nchi 1987)
Asilimia 60 ya wananchi hawana kazi, wengi wanakimbilia Afrika Kusini kutafuta kazi.
Baada ya kutaifisha ardhi iliyokuwa inalimwa na raia wa kizungu wa Zimbabwe, uchumi ukashuka. Wakulima Wazawa wakashindwa kuitumia ardhi vizuri kutokana na sababu za kifedha na kielimu.
Sasa nchi inaomba msaada wa chakula nje na vyakula ni adimu madukani.
Pia, wapinzani wake wamebanwa koo na serikali yake.
4. Mfalme Mswati III
Nchi: Swaziland
Madarakani: Tangu 1986
Wananchi wake wanaishi miaka 46, wengi wanakufa na ukimwi na njaa. Asilimia 40 hawana kazi.
Mfalme ndiyo Mkuu wa Nchi. Hamna kura ya kuchagua kiongozi.
Mswati anatumia fedha za Nchi kama za kwake. Anajulikana zaidi duniani kama mpenzi wa magari ya BMW na huowa karibu kila miaka michache. Ana wake 14.
5. Rais Omar Al-Bashir
Nchi : Sudan
Madarakani: Tangu 1989 baada ya kumpindua Sadiq al- Mahdi.
Vita nchini vimeua watu milioni moja na maonevu dhidi ya raia wa Kiafrika wa Kusini mwa Sudan imesababisha Sudan kugawanyika mwaka 2011 na kuwa Sudan na Sudan ya Kusini baada ya raia hao kupigana vita na serikali ili wapate haki zao.
Wananchi wa Sudan hawana haki yoyote chini ya serikali yake ya chama kimoja, National Islamic Front. Wabunge wake wote 500 ni wa kuteuliwa.
Bado sijaongeza kina Museveni, Kagame na Nkurunziza.
Listi ni ndefu mno.
Let us agree not to agree.Siyo kila kitu lazima tusome katika magazeti ya ulaya.
Common sense should dictate policies.
Nchi ilikuwa inazalisha vyakula vya kila aina. Kilimo kilikuwa bora sana.
Sioni sababu yoyote ya msingi ya kuwafukuza wazungu na kuwapa ardhi Wazawa kabla ya kuwaelimisha na kuwapa msaada wa kifedha.
Kuna faida gani Wazawa wamepata baada ya kumiliki ardhi yao?
Si bora, wangekuwa katika JV na wazungu? Kumbuka kuwa hawa wazungu pia ni raia wa Zimbabwe.
Leo, Wazawa wasingeliwa na simba, kujaribu kuingia Afrika Kusini kimagendo kutafuta ajira.
Siku tatu baada ya Rais John Magufuli kueleza kuwa yeye si kichaa, si dikteta wala mnyama, Jaji Thomas Mihayo ameungana na mkuu huyo wa nchi akisema hajauona udikteta wake.
Jaji Mihayo alikuwa akifafanua kauli alizotoa Rais Magufuli kwenye kilele cha Siku ya Sheria, wakati alipomuahidi Jaji Mkuu Othman Chande Sh12.3 bilioni za kuendeshea shughuli za mahakama na kumtaka aharakishe kushughulikia kesi za ufisadi ili Serikali iokoe Sh1 trilioni, ambazo kati ya hizo atatoa Sh250 bilioni kwa ajili ya Idara ya Mahakama.
Rais pia alitaka kesi ambazo watuhumiwa wanakamatwa na ushahidi, zifikishwe mahakamani mara moja na kuamuliwa, lakini akataka asichukuliwe kuwa ni dikteta kutokana na maamuzi yake.
“Ninapochukua hatua mimi si mnyama, si dikteta, si shetani. Ni mpole kweli, lakini inafika mahali lazima nifanye (uamuzi). Yanayofanyika serikalini ni mambo ya ajabu sana, nataka kutoa sadaka yangu, inawezekana hata nikifa naweza kuwa rais wa malaika,” alisema.
Kauli hiyo imeibua mjadala miongoni mwa wanasheria wanaodai Rais anaingilia uhuru wa mahakama kwa kutaka uamuzi wa kesi hizo ufanywe kwa utashi wa Serikali, huku baadhi ya hatua kali anazochukua zikielezewa kuwa zina harufu ya udikteta.
Lakini jana, mkuu huyo wa nchi alipata mtetezi wakati Jaji Mihayo alipoongea na waandishi kufafanua kauli hiyo ya Siku ya She ria, akisema Rais dikteta ni yule asiyefuata misingi ya sheria.
“Wanaosema Magufuli ni dikteta hawawajui madikteta. Hakuna kiongozi dikteta Afrika Mashariki isipokuwa Idi Amini tu,” alisema jaji huyo mstaafu ambaye alisema ameamua kutoa ufafanuzi huo baada ya kuona mjadala mkubwa kuhusu kauli hiyo ya Rais na kupata baraka kutoka kwa Jaji Mkuu, Othuman Chande.
Jaji Mihayo, ambaye ni mwenyekiti wa majaji wastaafu, alihoji inawezekanaje kiongozi ambaye mataifa mengine wanatamani akaongoze nchi yao angalau kwa miezi miwili, aonekane kuwa ni dikteta.
“Magufuli anafuata sheria kwa sababu hajafanya jambo lolote ambalo linamfanya awe juu ya sheria. Sijawahi kusikia kasema mfunge huyu au kusema sheria hii isitumike na hii itumike” alisema.
Alisema ni kawaida kwa viongozi wanaokemea uovu kuonekana kama madikteta kwa sababu wanataka kuondoa rushwa.
Kadhalika, Jaji Mihayo alisema anaupenda utendaji kazi wa Magufuli ili wanaokiuka sheria wawajibishwe na walalahoi wapate haki yao.
Magufuli na Mahakama
Kuhusu ahadi yake ya kuipa Idara ya Mahakama Sh12.3 bilioni ili izitumie kwenye shughuli zake na agizo la kuharakisha uamuzi wa kesi 442 ili Serikali iokoe Sh1 trilioni, Jaji Mihayo alisema kitendo hicho hakiingilii uhuru wa mahakama bali ni katika kuhakikisha kesi zinamalizwa kwa wakati na serikali inakusanya mapato ya kutosha.
“Maneno ya Rais ya kuwataka majaji wamalize kesi kwa haraka na kuwaahidi kiasi kile cha fedha, si kuwahonga bali ni motisha na mbinu ya kukusanya mapato,” alisema.
Alisema kauli ya Rais isitafisriwe kuwa ni lazima Serikali ishinde kesi dhidi ya rufaa ya kodi, bali alitaka majaji wafanye kazi zao kwa wepesi zaidi.
Akifafanua kesi za rufaa za kodi, Jaji Mihayo alisema mashauri hayo yatakusanya fedha nyingi kwa hata kama wanaodaiwa watashinda, kisheria ni lazima watoe theluthi ya kodi wanayodaiwa.
Jaji Mihayo pia alisema maneno ya Magufuli yasichukuliwe kuwa yatawavuruga majaji kwa sababu wanafanya kazi yao kwa kufuata kanuni na sheria.
“Uhuru wa mahakama upo ‘guaranteed (umehakikishwa)’ na katika kifungu namba 107 (a) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano.Hata kama Rais akiamrisha vipi, kama ni kitu ambacho ni kinyume na utaratibu, hakiwezi kutekelezwa” alisema.
Kuhusu Magufuli kuwachukulia hatua majaji na mahakimu 502 ambao hawajafikia malengo ya kumaliza kati ya kesi 250 na 260 kwa mwaka, Jaji Mihayo alisema JPM alionyesha kukerwa na ucheleweshaji wa kesi na wala si kuingilia uhuru wa mahakama.
Alisema hata Jaji Mkuu Othman Chande alishachukua hatua kwa kuwataka mahakimu hao watoe maelezo kabla sheria haijachukua mkondo wake.
“Tatizo la ucheleweshaji wa kesi ni kubwa, si dogo kama unavyofikiria ndiyo maana linamkera JPM,” alisema.
Utendaji wa mawaziri, wakuu wa mikoa
Kadhalika Jaji Mihayo pia alizungumzia pia jinsi mawaziri wa JPM wanavyotoa kauli za kuwafukuza kazi au kuwasimamisha watendaji wa Serikali, akisema siasa inatawala kuliko sheria.
Alisema kisheria kiongozi wa Serikali hawezi kusimamishwa kazi au kufukuzwa bila maandishi.
“Watendaji hawatachukuliwa hatua bila kauli ya waziri kuwa katika maandishi, hilo jambo halichukuliwi kijumla tu,” alisema.
Alisema Katibu Mkuu Kiongozi akimsimamisha au kumfukuza mtu kazi, hilo linakuwa limeshafanyiwa kazi kwa kina.
“Vinginevyo, huwezi kumfukuza mtu kazi bila mchakato na uchunguzi wa kuhakiki kama ni kweli ana haki ya kusimamishwa au kufukuzwa,” alisema.
Let us agree not to agree.
Hawa wenye vinywa vichafu kama vyabataAsante Jaji Mihayo kwa kunyoosha mambo. Vinywa vilivyopinda tena vilivyojaa sumu tayari vilianza kumng'ata rais licha ya utendaji wake mzuri. Watafute mengine ya kutuhumu.
Kama mifano ndio hiyoMbona ni wengi tu, ongezea Yoweri Museven, Paul Kagame, Nkuktunzinza, CCM nk.
Nimesema mara nyingi, kuna haja ya kutenga shughuli za majaji na shughuli nje ya ujaji
Majaji wa Tanzania nao wameingia katika mkumbo wa kuishi kwa kauli. Kwamba, ili waendelee kutumikia tume, kamati na kazi nyingine lazima wajihusishe na kujinasibisha na wanasiasa. Hili ni tatizo kubwa sana
Jaji anaposema Magufuli si Dikteta, hivi uchaguzi wa ZNZ anaounga mkono urudiwe bila msingi wowote wa hoja hiyo ni nini?
Hivi, lini mhimili wa serikali umeanza kupanga matumizi yake bila kushirikisha Bunge?
Hivi Jaji Mihayo na wenzake walikuwa wapi kutoa maoni yao kuhusu mkwamo wa ZNZ?
Hivi, Rais anaposema kesi zimalizwe ili apate trilioni 1 hapo ina maana gani? Je kama kesi zitakuwa hazina ushahidi atapataje trilioni na hilo linamweka wapi Jaji mkuu? Nani amesema lazima hukumu itoe trilioni 1 ? Haki ya aliyekwenda mahakamani inazingatiwaje?
Haya ndiyo mambo tunayotarajia kusikia yakitolewa ufafanuzi. Inashangaza mwenyekiti wa Majaji ameyaacha sasa anazungumzia nchi nyingine kutamani Magufuli atawale miezi miwili. Jaji ameacha hoja za eneo lake sasa anarukia mambo ya siasa
Upo umuhimu wa kuwaacha majaji washughulike na shughuli za kisheria, haya mengine wajitoe maana kila wanapoingia wanatutia shaka sana.
Robo trilioni inayopewa mahakama ilipangwa na bajeti ipi? Na kwanini pesa zitoke baada ya kuhukumu. Hapa anawaambia majaji, wakihukumu watuhumiwa kulipwa nao wana robo trilioni. Tunachouliza wapi haki ya kwenda mahakamani kusikilizwa ilipo?Wewe una uhakika gani hana hoja ya msingi inayofanya asiunge mkono uchaguzi urudiwe?
Hela za matumizi ni walizoomba toka bajeti iliyopitishwa na bunge mara ya mwisho kikao cha bajeti kilipo kaa bungeni, so bunge lilisha shirikishwa ni pesa zilikua hazijatolewa
Kwani lazima wao na majaji wenzake watolee maelezo kila kinachotokea nchini
Ametolea ufafanuzi hapo juu ni agizo tu rais alitoa ili majaji wafanye fasta kutoa hukumu, kuhusu kukusanya 1trilion na amesema katiba hairuhusu makama kufata kile rais atakachosema hatakama ni amri, kama ikiwa kinyume na sheria
( “Maneno ya Rais ya kuwataka majaji wamalize kesi kwa haraka na kuwaahidi kiasi kile cha fedha, si kuwahonga bali ni motisha na mbinu ya kukusanya mapato,” alisema.Alisema kauli ya Rais isitafisriwe kuwa ni lazima Serikali ishinde kesi dhidi ya rufaa ya kodi, bali alitaka majaji wafanye kazi zao kwa wepesi zaidi.Akifafanua kesi za rufaa za kodi, Jaji Mihayo alisema mashauri hayo yatakusanya fedha nyingi kwa hata kama wanaodaiwa watashinda, kisheria ni lazima watoe theluthi ya kodi wanayodaiwa.Jaji Mihayo pia alisema maneno ya Magufuli yasichukuliwe kuwa yatawavuruga majaji kwa sababu wanafanya kazi yao kwa kufuata kanuni na sheria.“Uhuru wa mahakama upo ‘guaranteed (umehakikishwa)’ na katika kifungu namba 107 (a) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano.Hata kama Rais akiamrisha vipi, kama ni kitu ambacho ni kinyume na utaratibu, hakiwezi kutekelezwa” alisema.)