Jaji Lubuva: Msitegemee jipya kutoka kwangu

Sheria ya sasa inasema matokeo ya Urais ili yawe rasmi ni lazima yatangazwe na Tume ya TAifa ya Uchaguzi; na kuwa wana uwezo wa kuzuia matokeo hayo kutangazwa majimboni kama walivyofanya mwaka jana. Sasa Lubuva afanye nini?

Sheria ya sasa hairuhusu kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais baada ya mtu kutangazwa kuwa kashinda; sasa Lubuva afanye nini?

Mkitaka Lubuva afanye tofauti au apunguziwe nguvu haitoshi kumwangalia yeye; ni kuangalia Bungeni huko. Kwani Bunge laweza kubadilisha sheria kabla ya kubadili hata Katiba.
 
Mbona kasema kitu cha kweli na wazi. Mkitaka tuibadilike badilisheni Katiba na sheria. Marefa mbalimbali mchezo uleule.

Hakika Mkuu kwa maana nyigine ni kuwa Sheria zilizopo/zitumikazo mpaka sasa hivi zinamfunga mikono kiutendaji/kiutekelezaji.
Kama vile mtu kufanya kosa kubwa na Adhabu ikaonekana ndogo, Lakini kama ndio adhabu iliyotamkwa na Sheria hata Jaji awe alichukizwa vipi hawezi akakurupuka na hukumu toka kichwani kwake.
Wadau Tujinoeni katika Mchakato wa KATIBA mpya mapambazuko yataanzia hapo.................
 
Back
Top Bottom