Jaji Lubuva: Hakuna lolote jipya la kujifunza kutoka katika uchaguzi wa Kenya

Ulitaka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi apendekezwe na CHADEMA au mbowe au Lipumba?
Hivi ww mbona karibu kila comment zako unatetea vitu visivyo na msingi au ni kada wewe
jamaa kaeleza vzur kuwa haiwezekan mwenyekit watume ateuliwe nawatu walio madarakani au watawala very simple, akimaanisha ata CHADEMA wakija kuwa watawala haistahili wapendekeze au kuyeua mwenyekiti..... .. Ww umekaa ku comment nonsense

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mzee bhna nikajua alitakiwa kusema tunachojifunza kupitia kenya nikupata katiba mpya itakayo kuwa very transparent na ya kidemokrasia ambayo tume iwe huru na matokeo ya uraisi yaweze kupingwa mahakamani kama uko kenya,,.....eti hatuna lakujifunza


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Familia yake ijiandae kumvisha nepi maana anarudi Kwenye utoto.
 
Nina wasi wasi na Jaji na mara nyingi simwelewi kabisa

Jambo la kujifunza, ukiwepo utaratibu mzuri nchi za Afrika zinaweza kuepuka aibu ya mapigano kama yaliyotokea Kenya miaka michache iliyopita
Tunajiufunza uwepo wa vyombo huru vya sheria ni sehemu muhimu ya amani ya nchi
Tunajifunza mpinzania anaweza kuheshimu tume, na mshindi akaheshimu mahakama
Ni Jaji huyu aliyewahi kueleza matokeo kutohojiwa na chombo chochote kile.
Hapa nchini ingetokeaje ikiwa matokeo ya ZNZ hawayakuweza kuhojiwa na ikiwa sheria haziruhusu kuhoji matokeo. Nina bahati mabya sana huwa simwelewi huyu mzee asilani
“Yote hayo ni ya kawaida. Hatuwezi kusema Kenya ni role model (mfano wa kuigwa), wamefana hivyo kulingana na mazingira yao,” alisema.
Jaji, ni role model hata kama wewe binafsi hutaki.
Kutoka mapigano hadi majibizano ya hoja bila kupigana ni role model
Ni role model kwasababu kilichopo kwetu ni dhalili kuliko kilichoonekana Kenya, Jaji!
Jaji Lubuva aliteuliwa na mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais.

Tulishuhudia mambo yalivyokuwa yanakwenda, leo anasema wapo huru!
Majaji wanateuliwa na Rais ambaye ni mwenyekiti wa chama.

Acha mwenyekiti , hata viongozi wa chama tu majaji hawana kauli katika masuala yanayohusu chaguzi, vyama n.k.

Angalia taasisi zinazoongozwa na Majaji pima hadhi ya Ujaji na utendaji wa taasisi hizo.
Ni kweli, taaluma ya Ujaji imepoteza hadhi kwasababu za siasa. Hilo halina ubishi Jaji
Amesema kwa upande wa NEC kuna maamuzi mengi wamewahi kufanya na Rais au vyombo vya usalama havikuwaingilia.
Mzee anasikitisha sana
Alipoulizwa vipi kitendo cha Rais kubadili watendaji wa Tume wakati au karibia na uchaguzi, amesema kuhusu kamishna aliyetuliwa kuwa Jaji yeye aliulizwa na kukubali kwa kuwa lilikuwa ni suala la mtu kupanda cheo.
Jaji hakuona tafsiri ya jambo hilo mbele ya umma.

Jaji anaona ni sahihi kabisa kilichofanyika hakujiuliza kwanini wapandishwe vyeo wakati wa uchaguzi. Hakuona tafsiri ya jambo hilo kabisa mbele ya Jamii. Jaji!
“Hawa wengine wakiondolewa ni utaratibu tu, mbona hata huko Kenya wameondolewa wote kwenye Tume,” amehoji.
Ni Jaji huyu anayesema Kenya si role model halafu anafanya ufanano.

Halafu jibu la swali siyo Kenya wanafanya nini, ni yeye alifanya nini.
Hili si jibu analoweza kutoa mtu wa hadhi yake.
“Hata hapa kwetu waangalizi huwa tunawaeleza wasiiingie jikoni.
Ooops, Jaji kajisahau na kusema asiyotakiwa kuyasema.

Huko jikoni mnafanya kitu gani Jaji ikiwa kura zimepigwa vituoni?
Jaji haoni kabisa madhara ya kauli hiyo. Jaji Lubuva: Hatuna la kujifunza kutoka Kenya
 
Majij wengine bana, kashindwa kusema kuwa katiba ibadilishwe ili kuwe na usawa, na kwa nn wasimamizi wa uchauzi wa kimataifa huwa hawaruhusiwi kuingia jikoni basi hapa hakuna ukwel hata mmoja zaidi ya wizi wa kura kufaanywa jikoni huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Anataka kutuambia kuwa, kwa umri wake anajua mbinu zote za wizi wa kura wanazotumiaga kwa hiyo hana la kujifunza.

You can not teach an old dog new tricks.
 

Bora Jaji Lubuva umekiri kwamba kama tume hamtaki waangalizi waingilie mambo ya "jikoni." Ukweli ni kwamba huko jikoni ndio mnapika matokeo ya uchaguzi kinyume na kile walichotaka wananchi. Na kwanini sheria na taratibu za Bongo zisiruhusu matokeo kupingwa mahakamani kama sio nyie CCM ndio hamtaki mabadiliko ya katiba? Mfano, ni mchakato wa mabadiliko ya katiba ambao tume yako na Kikwete mliamua uishie njiani....
 
Kuna binadamu anaweza akashindwa kujifunza kwa wenzie. Basi kama yupo atakuwa na matatizo ya kli ,na hiyo inaonyesha kwenye tume kulikuwa na magumash kibao. Hata kuona umuhimu wa mahakama kuchukukua nafasi yake na kuepusha machafuko haoni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaji Lubuva unajivunjia heshima tu!TUME yako ni haramu unateuliwa na Rais ambaye huyo huyo unasimamia chaguzi ambayo na yy anashiriko
Kibaya zaidi unawajibika kwake na anaweza kukufuta kazi akiamua!
Tunataka tume huru!!
 
Nayo jumuhiya madola au madoa? Hivi kweli hiyo jumuhiya haina watu hata ikamtuma Lubuva? Au inahusika mambo yanayotokea kwenye chaguzi za Africa? Kweli wazungu ndio walimpeleka Lubuva? Naombeni jibu na mnipe anuani zao hao wanaojiita jumuhiya ya madola.
 
Amezowea wizi ndiyo maana hawezi kujifunza chochote toka kenya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…