Jaji Joseph Warioba aunguruma: Agusia Katiba mpya, upungufu wa chakula na vita madawa ya kulevya

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Habari wakuu,

Jaji mstaafu, Sinde Warioba yuko ukumbi wa Makumbusho katika mwaliko wa kongamano la wanawake katika uongozi kuzindua kitabu alichoandika dibaji kilichoandikwa na professa Meena kuhusu hatua za kutengeneza katiba mpya.

Amesema Profesa Meena ameandika safari nzima kila hatua ambayo anadai haijaisha na bado wanaendelea, amesema kitabu kimeanisha maeneo 12 yanayohusika katika kutengeneza katiba mpya na jinsi ya kufikisha ujumbe katika nguvu inayostahili.

Amesema nchi hii imezoeleka wazo likitolewa na kiongozi wa chama kimoja, kinatokea chama kingine kupinga lakini kwenye mambo ya kitaifa ni lazima kukubaliana na kinamama wameonyesha kuweza na ni somo ambalo watanzania wamepewa.

Jaji Warioba amedai nchi ina matatizo mengi na baadhi ya matatizo hayo yanahitaji nguvu ya pamoja bila kujali vyama na kama wanawake wameweza wa vyama tofauti wameweza inakuwaje wengine washindwe.

Ametolea mfano wa tatizo la upungufu wa chakula ambalo kuna dalili likatokea nchia na amesema Somalia watu wanakufa kwa njaa na Kenya mifugo inakufa kwa njia pia zipo nchi kubwa kama Nijeria zimekubwa na tatizo hilo.

Amedai dalili zinaonyesha tatizo hilo litatupata na haitakuwa mara ya kwanza kwani lishatupata huko nyuma na watu wote wakajiandaa na wote walishiriakiana kuwasaidia kuwapa wakulima ikiwemo maarifa na taarifa za hali ya hewa. Kwa hio sasa hivi viongozi wasambe wasaidie wananchi na serikali ijiandae japo imezoeleka kila mwaka sehemu zenye za upungufu zinafidiwa lakini mwaka huu tatizo linaonekana ni kubwa.

Amesema haina haja ya kubishana kama kutakuwa na njaa ama haitakuwepo na watu waige wanawake.

Mfano wa pili ametolea kuhusu dawa za kulevya na kusema pia ni tatizo la pamoja na linahitaji nguvu ya pamoja, amesema kinachoendelea ni matukio na yanaripotiwa kama matukio kisha yanapita, amedai kuna haja ya kuwaelimisha wananchi madhara ya kulima na kutumia bangi na kwa pamoja tuwasaidie njia mbadala kama njia yao ya maisha.

Amesema madhara yanajulikana ya kutumia bangi na tujenge nguvu ya pamoja na inahitajika ushirikiano wa kila mtu lakini linazungumzwa kama tatizo la kawaida na umetafutwa mchepuo wa kisiasa na ndicho kinachozungumzwa sasa badala ya tatizo lenyewe.

 
Kwa usemi huu ina maana likubalike hata lisilofaa?
"Amesema nchi hii imezoeleka wazo likitotolewa na chama kimoja, kingene kinapinga"

Halafu mbona sijaona mahali akizungumzia katiba? Au ni macho yangu

Atangulie polisi maana ni mchochezi kataja neno njaa. Au hili neno ni la upande mmoja tu. Mbon a hajaenda dodoma au yeye siyo mjumbe
 
Katiba mypa muhimu ili kudhibiti Ubashite unaoendelea kwenye hii awamu ya 5
 
Amezungumzia wakina mama kwa mujibu wa posti yako, na sio katiba mpya kama ulivyoandika katika kichwa cha habari.
 
Habari wakuu,

Jaji mstaafu, Sinde Warioba yuko ukumbi wa Makumbusho katika mwaliko wa kongamano la wanawake katika uongozi. Kwa sasa anazindua kitabu alichoandika dibaji kilichoandikwa na professa Meena kuhusu hatua za kutengeneza katiba mpya.

Amesema nchi hii imezoeleka wazo likitotolewa na chama kimoja, kingene kinapinga lakini wakina mama wameungana bila kujali vyama vyao.

Ameongea suala la upungufu wa Chakula na kusema haina haja ya kubishana kwani dalili zote za hali zinaonyesha kutakuwa na upungufu wa Chakula na hali hiyo imeshawahi kuwepo mwanzo na watu wote walijiandaa kukabiliana na hali hiyo.
huyu mzee tutakuwa hatusaini penshini yake we muache
 
Katiba sio kipaumbele kwa sasa.kama mliikwamisha wakati wa kikwete,imekula kwenu tupo bize na viwanda na mihadarati
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom