Jaji Joseph Warioba aunguruma: Agusia Katiba mpya, upungufu wa chakula na vita madawa ya kulevya

Toka mzee alivyopigwa na Bashite kisa UKAWA, then akaenda Jangwani kuwapigia debe waliomtuma Bashite kisa tu mwanae apewe jimbo nilimchoka naye.

Ni wale wale tu. Nasubiri kumwona Pro Kabudi baada ya kuingia kwenye timu ataendelea kuitetea rasimu yao au ile ya Mar Sita!
 
Amesubiri kiboko yake bashite hayupo ndio akahutubi, chezea kupigwa wee... (ni utani tu)
 
Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Jaji Joseph Warioba amewataka watanzania wote kuungana na kujiaandaa kukabiliana na baa la njaa ambalo huenda likatokea, huku akikiri kuwa tatizo la upungufu wa chakula kwa mwaka huu, ni kubwa kuliko kawaida.




warioba%202.jpg

jaji Joseph Warioba

Akizungumza leo wakati akizindua kongamano la 'Wanawake na Uongozi' katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam, Jaji Warioba amesema hakuna haja ya watanzania kubishana na kulumbana kama kuna njaa au upungufu wa chakula, bali kujiandaa ikiwa ni pamoja na kujifunza kujifunza katika nchi ambazo tatizo hilo limetokea ikiwemo Kenya na Somalia.

"'Haijalishi kama njaa ipo au kuna upungufu wa chakula kinachotakiwa ni kuungana na kujiandaa kwa pamoja ili kujua ni jinsi gani tutaweza kukabiliana na baa la njaa endapo litatokea kama jinsi inavyosemwa, tujifunze kupitia Kenya na Somalia. Siyo sawa kurushiana maneno huyu anasema hivi huyu anamjibu vile, tuungane kwa pamoja" Amesema Warioba ambaye pia alikuwa ndiye Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba a kuongeza“Serikali ijiandae kukabiliana na njaa kwa sababu ingawa tumezoea kwamba kila mwaka zipo sehemu zenye upungufu wa chakula, mwaka huu tatizo ni kubwa”

Kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya, Warioba ametaka elimu itolewe kwa watu wanaojishughulisha na dawa za kulevya hususani wanaolima bangi lakini pia wasaidiwe wapate njia mbadala za kuweza kujikimu ili kuachana na shughuli hizo ambazo zinaathiri asilimia kubwa ya vijana.

Ameongeza kuwa tatizo la dawa za kulevya linaripotiwa kawaida kama siyo tatizo kwa sababu limefanywa kama jambo la siasa

bangi%202.JPG


Shamba la bangi lililokamatwa hivi karibuni mkoani Mbeya

"Tatizo la dawa za kulevya linazungumzwa kama jambo la kawaida, badala yake tumetafuta mchepuo wa kisiasa, ambao ndiyo unazungumzwa, Karibu kila siku utaona taarifa kwamba wameenda askari wameharibu dawa za kulevya katika mashamba ya bangi, inaripotiwa tu kama tukio halafu basi. 'Tuseme hapana matumizi ya madawa, madawa ni mengi sana yanayoingia , tunajua madhara yake, tuyazuie yanayoingia kutoka nje pamoja na yanayolimwa, tujitahidi kuwasaidia vijana walioathirika. Tunahitaji kujenga nguvu za pamoja" Amemalizia jaji Warioba.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba, ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, na limetumika pia kuzindua kitabu chenye jina 'Nguvu zetu, Sauti zetu, Ajenda katika mchakato wa katiba mpya' kilichoandaliwa na mtandao huo jijini Dar es salaam,
 
Atupe takwimu za njaa..ye kakaa oysterbay habari za njaa kazitoa wapi.
 
Anaejua kuna njaa nchi hii au hamna ni mmoja tuu.. Na yeye ameshasema hakuna njaa, hao wanaosema wana njaa Mtukufu amesema ni wavivu.. Serikali yake haitapeleka hata punje mmoja ya chakula kwa wavivu..

Jaji Warioba kuwa makini, ohoooo..
 
Akili zitawakaa sawa.

Sasa mvua zinanyesha ila wakulima wamegoma kupanda mahindi kwa hofu ya kukaukiwa. Tena Wapo ambao wamekula mpaka mbegu na wengne wanekimbilia mjini na kuacha mashamba yao.

Sasa Africa ipo under attack ya viwavijesh ambao wanashambulia mahindi na mpunga. Viwavi Jeshi (Armyworms caterpillars) wa aina ya ajabu washambulia mashamba ya Mahindi.
Nchi kama Namibia , SA etc, zimekutana kufanya mikakati kumkabili huyu kiwavijeshi. Tanzania yenyewe haina hata habar na Rais wao anayejifanya kuignore majanga ya msingi na kudeal na wapimnzani tu.

Njaa ipo na ipo kubwa. Hii serkal isiyokuwa na mbele wala nyuma itawaumiza Watanzania kama hawatabadilika na kutambua majukumu yao kama wananchi juu ya sherikal.

Wamedanganya sana kuhusu takwimu za uongo sasa watasema tu ukweli.
 
Tatizo ni kuwa watu wanafahamu mbwa mzee asiye na meno akibweka wala hatishi tena! Huyu mzee tangu alipounga mkono chama kilichomdhalilisha hadharani kwa kuwatumia kina Daudi Bashite wakati wa uchaguzi, namwona hana mvuto tena wala hastahili tena kusikilizwa!
 
Back
Top Bottom