Kuna watu wakiwa kwenye sherehe zao, moshi wa nyamachoma zao ulisababisha mimba ya mama mmoja kuharibika. Mume wake akamshitakia Nabii Mussa. Mtume huyo akamwombea dua mke apate mimba nyingine na kuwaomba wanandoa hao kuwasamehe wahusika maana hawakukisudia. Mume hakuridhika, akaenda kushitaki kwa Firauni (Pharaoh). Hukumu ya Firauni ikawa yule mama apelekwe kwa wale waliohusika na uchomaji wa ile nyama. Ilivyokuwa wao ndio walisababisha ile mimba kuharibika, Firauni aliamuru yule mama asiondoke mpaka wampe mimba mbadala! Ndio ukistaajabu ya Musa utapata ya Firauni! Na mimi sio Tomaso. Naajabia tu haya ya Musa kabla ya Firauni hayajaja!wacha kuwa na imani ya Tomaso