PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 354
- 395
Mbunge wa Jimbo la Kisarawe mkoani Pwani, Dkt. Selemani Jafo ametilia mkazo suala la wajibu wa kila mtanzania kulinda amani ya nchi akieleza kuwa ajenda ya amani haina mbadala hivyo inapaswa kulindwa kwa wivu mkubwa.
Dkt. Jafo ametoa mfano kwa kutaja baadhi ya mataifa ambayo uchumi wake umeharibika baada ya amani kutoweka huku akiwasisitiza vijana wote nchini kulinda kwa wivu mkubwa amani na kutokukubali nchi ikaharibika mikononi mwao.
Ameeleza hayo leo Januari 29, 2026 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la 13, iliyoeleza muelekeo wa serikali yake.
Aidha, ameongeza kuwa Rais Samia ametoa ahadi zinazotekelezeka huku akianisha miradi mbalimbali iliyotajwa katika hotuba hiyo na kufafanua namna miradi hiyo itabadili uchumi wa Tanzania.