J. Mbwambo's article: tumekuwa taifa 'gonjwa' - raia mwema. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

J. Mbwambo's article: tumekuwa taifa 'gonjwa' - raia mwema.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Resi, Apr 8, 2011.

 1. Resi

  Resi Member

  #1
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 73
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Wana jamvi, hi. Hapa chini ni mwawazo yangu kuhusu makala ambayo columnist anayeheshimika hapa kwetu na kwingineko, Johnson Mbwambo wa Raia Mwema aliandika katika gazeti hilo, toleo la 180, internet edition.

  Ndugu Mbwambo, habari,

  Nimesoma makala yako "tumekuwa taifa 'gonjwa'" katika toleo 180 la 'raia mwema', internet edition. Nimeona siwezi kuyaacha uliyoyasema humo bila kutoa mwawazo yangu. Kwanza kabisa mimi naamini kwamba ile 'taa ya mchana' inatakiwa siyo tu kwa Tanzania, bali kwa dunia yetu nzima! Na imani yangu hii nitaidhihirisha hapa chini. Napenda nianze kwa kusema kwamba, kinyume na wewe, mimi sioni madhara katika hiki ntakachokiita 'the Loliondo phenomenon', badala yake naona faida tu kwa Wa-Tz. Nasema hivyo bila kujali kama dawa ya Babu inatibu magonjwa yanayotajwa ama la, maana nakubaliana na wewe kwamba 'efficacy' ya dawa hii ya Babu tutaiona baada ya muda kupita na utafiti wa waliotibiwa kufanyika.

  Ndugu, imani za kishirikina hapa duniani haziko Tz peke yake; miracle cures - ziwe za magonjwa ya kimwili, ya kisaikolojia, ya ki-roho, nk, zimekuwapo tangu enzi na enzi mpaka enzi hizi za sasa; pia haziko confined kwenye nchi zisizoendelea tu kama Tz, Kenya, Sudan, nk, bali hata zile zinazoitwa zimeendelea kama USA, England, Japan, nk. Naomba nitoe mifano.

  Ivory - pembe za ndovu, faru, nk. Katika nchi za Japan, Korea, China na nyingine za Mashariki inaaminiwa kwamba zinatibu/kupunguza impotency, reduced 'male powers' nk. Na hii imepelekea kuwindwa kwa wanyama wetu hapa Africa kwa njia halali au la kunakochochewa na imani hii ya hawa ndugu zetu. Japan, China, Korea nk, ni nchi ulizozitolea mfano kwamba wana maendeleo ambayo sisi tunawajibika kuiga.

  I am sure you also remember KEMRON and its purpoted ability to 'cure' AIDS. Where is it now??

  Visima/maziwa/mabwawa/mawe/chemchemu mbalimbali huko India, the Black Sea, Brazil, Fatima - Portugal-, Saudi Arabia, na kwingineko duniani ni mifano michache ya maeneo ambayo watu wanaamini kwamba ukioga, kunawa, kujipaka, kubusu nk utapona magonjwa, utaondoa 'balaa', utaleta 'baraka' katika maisha yako nk.

  As for Uganda's Alice Lakwena and the LRA, please refer to Jim Jones of Jonestown, Guyana, where in 1978 he killed 909 people belonging to his cult, by cyanide poisoning; he believed (and them too!!) that he was preparing them for the journey to heaven!! Now the kicker - these were good citizens of the good, old, grand, advanced, developed, educated US of A!! Please refer to Google & Wikipedia for confirmation of this sad incident. Secondly, please refer to the incident in which 80 members of the Branch Davidians, led by their leader, Mr David Koreshi, died in Waco, Texas, also in the grand USA!! HIYO NI MIFANO MIWILI TU, KATI YA MIFANO MINGI SANA, ya matokeo ya watu kupoteza imani katika mifumo mbalimbali ya dunia hii, na kugeukia mazingaombwe! Sidhani kwamba elimu na maendeleo ya nchi yana influence yeyote katika hilo, kama unavyodai.

  Kuhusu utafiti unaofanywa na Mamlaka za Nchi yetu ya Tz, mimi nasema kwa nini tusifanye utafiti wa kwetu kuhusu dawa ya Babu!!?? Kumbuka kuwa faida ziada za ASPIRIN -ambayo pia asili yake ni mzizi- (apart from its ability to reduce fever), zimekuwa zikigundulika na utafiti mpya unaondelea kufanywa na maabara za nchi mbalimbali hapa duniani. Kwa hivyo tuendelee na utafiti wa "carisa edulis - mugariga" hata kama wengine wamefanya utafiti juu ya mti huu. Kufanyika kwa utafiti mmoja sio mwisho wa jambo hilo.

  As for the 'Daily Nation' article, which you say has poured scorn on the Loliondo cup, I say don't pay attention to these 'naysayers' and 'we have done it already' phantoms. Wana sababu zao. Leave them be.

  Waziri wa Utalii hajakosea pale alipoambatanisha utalii wa wanyama pamoja na safari za kwenda Loliondo kwa Babu. Mfano mzuri ni Fatima, Portugal. Mahala hapo inasemekan Bikira Maria aliwatokea vijana watatu hapo mwanzo mwa karne iliyopita. Hivi sasa ni Tourist and pilgrimage sight, na inaingizia Portugal pesa nyingi sana. So what is wrong with making a little cash, hah!!??

  Papa Mbwambo, take it easy; please try and see the positives in this issue. I totally understand your concerns and I hope we never go down that road, but such is life - you are only offered possibilities and probabilities, and you have to make choices from all of them. You are an intellectual force in the Tanzanian intelligentsia; you have a big following among us, your readers. I am proud to say that every week I look forward to reading your carefully thought-out articles - and I am not ass-kissing here, honest!!
   
 2. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2011
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Dah! Una Viji=Pointi hapo, Mkuu. Mbwambo pia ana Viji-pointi kwenye makala yake which means mwisho wa yote tunarudi kule kule kwa kwamba mwenye kauli ya mwisho kabisa kuhusu Babu wa Loliondo na kikombe chake ni...Mtu na IMANI yake.
   
Loading...