J. Makamba, Sumaye, B. Membe hamuwaoni, Kwa nini Lowassa?

J. Makamba, Sumaye, B. Membe hamuwaoni, Kwa nini Lowassa?

Sumaye hana doa. Hata kwenye ufisadi hatujamsikia. Kwa uchapa kazi wawaulize Mzee Mwinyi na Mkapa ni nani alikuwa jembe lao. Ofisini mpaka saa 6 usiku.Hana makundi na huko makanisani alikuwa akialikwa na hotuba zake ni za kukemea ufisadi. Yeye mwenyewe ni mkulima na mfugaji wa kisasa. Ni mtu aliyetulia.CCM watuletee huyo wanaweza kupambana na Ukawa.

Sumaye aling'oa mitambo ya kusindika nyama kiwanda cha Tanganyika pekas kawe akaenda kuuza anapojua yeye, wakati JK anaingia madarakani walimkuta anamiliki ma-tirioni kwenye A/c yake wakamsihi akirejeshe akaludisha kimya kimya, ana mapungufu mengi sana ngoja wamteue Uone Uovu wake wote.
 
maswali ya msingi kabisa.......tatizo hawatakujibu japo najua January, membe,wassira wote wana watu wao humu........kiufupi tu ni kuwa lowasa hana mpinzani ndani ya CCM maana wote ni ukoo wa panya wanafanya tu kuzidiana maujanja.

January makamba hana chake, Jk hamtaki baada ya kugundua kuwa alitumia ikulu kiujanja kupenyeza dili zake, Mfano Dili la mararia alipora sugu na kupa Ruge kisha wakamchomekea JK akawa Mlezi pasipo kujua matokeo yake hiyo Dhuruma ikampa promo Sugu hadi kupata Ubunge, Rais JK hamkubali wala hawezi kumuunga mkono January kutokana na Dili nyingi alizofanya kupitia kiviuli cha ikulu Wakati akiwa msaidizi wa JK , alipata 10% kwenye kampuni kibao za kuwekeza kwa mbinu za kijanja janja tu kisa yupo ikulu January kwanza si mwaminifu ni mzurumaji sana wengi waliofanya naye Dili amewadhurumu hivyo kumlaani sana na Laana zao zinafanya kazi licha ya January kupenda magic Lakin wana imani haitasaidia, kwani hata baba yake alikuwa mchawi lakini siku zilipofika alifutwa Ukatibu mkuu wa CCM na ndumba ziligoma kufanya kazi.
 
Hao wote uliowataja wana akili kushinda bwana mazingaombwe Lowassa.hata hivyo kama walitoa rushwa hawafai kuwa viongozi lakini kwa uwezo wa kuongoza bora hata januari kuliko huyo laigwanani.waswahili wanasema bora nusu shari kuliko shari kamili. Lowassa ni kilaza sana hana credibility za kuwa president.
 
Wote wametoa Rushwa. Asiyetoa Rushwa kati ya wagombea CCM aje aseme . Muacheni Lowasa miaka 100 aende zake Magogoni akatupe raha.
 
Kama ulifuatilia makala zote 9 zenye kichwa cha "Lowasa pasua kichwa" zilizoandikwa na Absolom Kibanda katika gazeti la Rai uaona alichotafakari kuhusu mchakato wa Urais ndani ya CCM ni hiki tunacho kishuhudia leo hii. Hata CCM kuendelea kuwaweka "kifungoni" kina Lowasa, Makamba, Wasira na wengine mlengwa mkuu ni Lowasa maana wakimpa muda mrefu hakamatiki. Kwa maana nyingine "All eyes are on Lowasa" (macho yote yako kwa Lowasa). Kuna mwandishi aliandika kitabu kinaitwa "A vulture is a patient bird" yaani Tai ni ndege mwenye subira sana. Lowasa is a political vulture. Watake wasitake anawapasua vichwa.
 
JAMANI JAMABI!!!hawa sio ndugu moja wanatuzingua sana
 
Hiv kweli kuna wadanganyika wanawaza Lowassa awe next president wa tz? polokodio....!



Hilo sio swali la kuuliza kwa sababu wanaomuunga mkono wapo bila kujali kuwa ni wengi au ni wachache.
Labda ungeuliza kwamba hivi watanzania wanaomuunga mkono Lowasa watafanikiwa kumpatia ushindi?
Au je,watanzania wanaomuunga mkono Lowasa ni wengi kuliko wa makundi mengine?
 



WAKATI WAGOMBEA WENGINE NDANI YA CCM WANA MLALAMIKIA LOWASSA HEBU TUJIULIZE HAYA MASWALI....


January Makamba amechapisha vitabu vyake na kugawa kwa wajumbe wote wa mkutano mkuu, mbona Lowassa hakulalamika?

January Makamba alinunua Simu za Gallaxy Sumsang zaidi ya 140 akazigawa kwa wajumbe wa baraza UVCCM ZANZIBAR.

January 2013 alipokusanya marais wa vyuo vikuu Tanzania nzima Mt. Uluguru Hotel na kuwalipa laki moja na nusu kila moja ili watoe tamko kuwa anafaa kuwa rais, mbona Lowassa hakulalamika?

Membe amekuwa akipendelea Wafuasi wake kwenda kusimamia chaguzi Kama waangalizi wa Sadc, mbona Lowassa hajalalamika?

Membe kanunua mabasi kwa baadhi ya makanisa, mbona Lowassa hakulalamika...?

Membe amekuwa na kawaida ya kuplant wagombea kama strategy yake na kuingilia Chaguzi nyingi kanda ya ziwa mbona Lowassa hajalalamika...?

Membe alipohudhuria tamasha la wasanii Mwanza na tamasha la extra vaganza (la wasabato) na kujipigia upatu mbona Lowassa hakulalamika?

Mwigulu alikuwa akitembea na mabango ya kuonyesha watu wakimuomba agombee mbona Lowassa hakulalamika...?

Mwigulu pia kaandika mawe karibu yote kila barabara TZ nzima mbona Lowassa Hajalalamika...?

Na mwandosya pia amekuwa akitumia Wanafunzi wa Vyuo Vya Mbeya na juzi wamemuombe agombee Mbona Lowassa hajalalamika...?

Mbona Pia Prof Muhongo anaombwa na umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Kilimanjaro, Arusha na Kanda ya Kaskazini mbona Lowassa hajalalamika.?

Sumaye mwezi december alipozunguka makanisa yote, Mbeya, Dar, na Mwanza kwa ajili ya kujitangaza mbona Lowassa hakulalamika?....


Mzee wote songa Mbele......Huwezi kuzuia Kimbunga kwa Mkono....


 
Back
Top Bottom