J K Nyerere (RIP) Angekuwa Rais Leo!

Kasimba G

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
3,428
2,609
Labda J K Nyerere angekuwa Rais Leo, Kuna baadhi ya viongozi wetu wasingenusa hata chembe za uongozi! Hata wa kijiji! Leo hii uongozi ni kwa kujuana either Ni ndugu au ndugu wa mbali au ni Mtoto wa mganga wake n.k.

J K Nyerere alikuwa na mfumo wake wa kupata kiongozi, aliruhusu Constructive criticsm! Ndio maana aliwapata watu kama akina Kimiti, Sita n.k katika vyuo vikuu. amabo ukiangalia kwa undani ni watu waliokuwa na misimamo furani, ambapo kwa viongozi wetu wa leo ukiwa na constructive critics ni adui!

Kipindi nasoma chuo kikuu kulikuwa na watu wa aina ya uwezo mkubwa, akina Matiku, Maswi (Katibu mkuu Madini), Mutungirehi, Bazigiza, Sweke, na baadae kuwasikia akina Dr. Kitila na wengine wengi wenye uwezo wa juu wa kujenga hoja na kutekeleza kwa kufuatilia mambo, hivi kwa nini tusirudi kwenye mfumo huo ili taifa liende mbele kwa kuwatumia watu wa kariba hiyo?

Mimi nimebahatika kuwa JKT na baadhi ya mawaziri wa JMK, ambao kama ingekuwa ni maswali, kwa ma- Mates zangu, je walistahili kuwa hapo walipo? Jibu ni big NO! Uwezo wa kujenga hoja hawakuwa nao, hatakujitetea na kutetea hoja hawakuweza, lakini ni mawaziri kabisaa! Tukikaa na wenzangu wa wakati huo wananiambai eti, afadhali hata wewe (mimi) ungekuwa waziri!

Nadhani kama taifa kuna kitu tunakosa haswa katika suala la uteuzi, hebu tuteue kwa uwezo, uelewa, na uthubutu, ambapo mawaziri wetu wengii wamekosa quality hiyo! Ndio maana mambo mengi yanakwama kwa kuwa uwezo huo hauko damuni mwao, wanabebeshwa kapu wasiloliweza!

Nawasilisha
 
ni kweli mkuu angalia hawa,adamu malima,wiliam ngeleja,mustafa mkulo, jumanne majembe,stivu kulaka,jakaya kikwete,sofia kuku, ane makinda,asante kawambwa..n.k
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom