Izack Emil afikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumtukana Rais Magufuli Facebook

Pius J. Kiwarya Lema

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
1,097
566
SHERIA YA MAKOSA MTANDAONI: Kijana Izack Emil afikishwa mahakamani Arusha leo asubuhi kwa tuhuma za kumtukana Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Facebook.
216bfeeb3a41cdaac8f67361343a424d.jpg

Kwa maoni yangu:

Hongera kwa Hatua hiyo, Msiishie hapo, kwenye mitandao ya kijamii kila siku ni matusi, badala ya hoja . Hata Lowassa pia anatukanwa, Matusi na Udhalilishaji kwa yeyote hayajengi!. Na Mashabiki wa Kisiasa ndo wanaonekana kupalilia kufilisika huku kwa mawazo.

Tujikite kwenye hoja sio matusi.
 
Hahahhahaha makamanda sheria mliyokuwa mnaipinga sasa hivi ndiyo mnaitumia.

Lowasssa angejifunza kwa Kikwete kila Pro-CHADEMA kaishamtukana lakini hata siku mmoja hakuhangaika na zaidi ya kuangalia huo ndiyo ukomavu wa siasa.

Kikwete anavyotukanwa mpaka yeye mwenyewe kwenye hotuba zake alikuwa anasema naongea hapa lakini baadae najua mtaniandika vibaya na kunitukana.
 
Hivi Lowassa na Kikwete nani ndo anayetukanwa zaidi??? Ingekuwa chuki za watu zinadhuru nadhani Kikwete na familia yake wangekuwa washakufa siku nyingi sana, Lakini kamwe Mungu hamtupi mja wake, wanatukana yanapita

Suala hapa ni nani anayetukanwa zaidi ama kutukunwa? Nadhani hata hao wanaotukanwa hawajali sana maana wanalipiza kwa kufisidi kodi zetu. Hapo ni nani anayeumia? Na ukiona mtu anatukanwa sana ni kama kuonyesha hisia za huyo mtukanaji dhidhi ya mtukanwa lakini anakosa lugha ya staha tu kufikisha yaliyo moyoni mwake.
 
SHERIA YA MAKOSA MTANDAONI: Kijana Izack Emil afikishwa mahakamani Arusha leo asubuhi kwa tuhuma za kumtukana Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Chanzo : Mwanachi

Kwa maoni yangu:

Hongera kwa Hatua hiyo, Msiishie hapo, kwenye mitandao ya kijamii kila siku ni matusi, badala ya hoja . Hata Lowassa pia anatukanwa, Matusi na Udhalilishaji kwa yeyote hayajengi!. Na Mashabiki wa Kisiasa ndo wanaonekana kupalilia kufilisika huku kwa mawazo.

Tujikite kwenye hoja sio matusi.
tupe tafsiri ta neno tusi au kutukana. Mfano kwa uelewa wangu nakuona wewe mjinga kwa sababu wajinga wapo, hilo ni tusi? Kama ni tusi basi maana yake huwa hakuna wajinga. Je si haki yangu kukuoba wewe ni mjinga?
 
Face book siyo mbaya ila wanaotumia waitumie kwa kuelimisha na kutoa hoja za msingi kwani matusi hayafundishi.
 
SHERIA YA MAKOSA MTANDAONI: Kijana Izack Emil afikishwa mahakamani Arusha leo asubuhi kwa tuhuma za kumtukana Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Chanzo : Mwanachi

Kwa maoni yangu:

Hongera kwa Hatua hiyo, Msiishie hapo, kwenye mitandao ya kijamii kila siku ni matusi, badala ya hoja . Hata Lowassa pia anatukanwa, Matusi na Udhalilishaji kwa yeyote hayajengi!. Na Mashabiki wa Kisiasa ndo wanaonekana kupalilia kufilisika huku kwa mawazo.

Tujikite kwenye hoja sio matusi.
Hata Lowassa anatukanwa ndio nini? jenga hoja watu kuheshimu watu na matusi ywe mwiko. Kutaja majina kujenga hoja ni kujifahamisha kuwa ni "simple minded person" Nomba radhi usinipeleke mhakamani!"
 
Wengi hasa enzi za jk tulizoea kusema neno lolote juu ya rais na hakuna aliye tugusa. lakini toka awamu hii ianze watu wengi sana wapo rumande kwa kumsema vibaya Rais. Kuna jamaa jana huko arusha kasweka ndani kwa kusema Magufuli ni mbwege.

so chunga mdomo, ikulu ya sasa ni simba.
 
Nimesikia eti anashtakiwa kwa kupinga kuwa Magufuli hawezi kufananishwa na Sokoinne.

Sijui sasa kaka ni lazma tukubali kuwa anafananishwa na Sokonne!!
 
Naona sasa Watu kutoka Lumumba wanahamisha Mjadala !

Kisa katajwa Lowassa tu kama mfano wa watu waliotukanawa lakini wahusika bado wanatafutwa!!!

Basi tuseme hata kikwete anatukanwa !
 
Back
Top Bottom