Iwe lazima kupiga kura Tanzania

Iwe lazima kupiga kura Tanzania

mwanandugu

Member
Joined
Mar 23, 2014
Posts
44
Reaction score
9
Kupiga kura ni haki ya kila Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18. Lakini wengi hawatumii haki hiyo inavyotakiwa wakati wanajua kwamba ni njia ya kukuza demokrasia.

Napendekeza kuwa suala la ulazima wa kupiga kura lifikiriwe na Bunge na ikiwezekana liwekwe kwenye Katiba mpya ili kila Mtanzania mwenye umri wa kupiga kura alazimike kushiriki zoezi hili muhimu.

Mimi naamini kwamba kukwepa kupiga kura ni njia ya kusema kwamba sitaki kushiriki katika maendeleo ya nchi yangu, jambo ambalo halikubaliki kwa mtu yeyote anayejiita Mtanzania.

Isitoshe, kuwachagua viongozi watakaochukua maamuzi muhimu kuhusu taifa langu ni njia ya kushiriki katika maamuzi hayo. Sasa sioni ni kwanini upigaji kura usiwe suala la lazima.

Napendekeza kwamba iwapo Bunge litakubali kupitisha sheria hii na kuliingiza kwenye katiba mpya, liweke pia kiwango cha faini atakayopaswa kulipa mtu yeyote atakayekwepa kupiga kura bila sababu ya msingi.

Baadhi ya sababu zinazoweza kumfanya mtu asipige kura ni kama kuwa safarini, ugonjwa na kadhalika. Hata hivyo, mtu akiwa safarini siku ya kupiga kura, anaweza kupewa kibali maalumu ambacho kitamwezesha kumruhusu mtu mwingine kupiga kura kwa niaba yake.

Katika nchi kama Australia (ambako upigaji kura ni lazima), mtu mzima akikwepa kupiga kura hulipishwa faini. Katika nchi nyingine watu hao wanaweza hata kunyimwa hati ya kusafiria kama pasipoti. Hii inaonesha ni kwa kiasi gani nchi hizo zinatoa kipaumbele katika suala la upigaji kura.

Wanaelewa kwamba sheria ya namna hii inaweza kuepusha ukwepaji wa kupiga kura bila sababu ya msingi, hivyo kukuza demokrasia na kuwezesha wananchi kuona umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya nchi yao.

Au mnasemaje Watanzania wenzangu kuhusu suala hili ? Nakaribisha mawazo yenu...
 
Sasa unategemea wabunge wa ccm wapitishe sheria itakayokuwa kitanzi chao? Ni utaratibu mzuri sana kuliko watu kuishia kulalama pale matokeo yanapokuwa tofauti wakati hawataki kupiga kura.
 
yeah nakuunga mkono mkuu, hiyo itakuwa imekaa vizuri japo hawatapiga wote lakini idadi ya wapiga kura itaongezeka sio kama ile idadi tuliyoiona kule kalenga na chalinze.
 
naunga hoja mkono maana watanzania wamezidi kwa uzembe,maana huwa najuuliza sababu nini?sipati jibu bora itungwe sheria kuwa ni lazima
 
Back
Top Bottom