Ivory Coast Vs Tanzania

Simba ooh soryy Taifa Stars wanatamani Ivory Coast na yenyewe ingekuwa na migogoro
 
DISALLOWED GOALIt's all action in Bangui - CAR have had a third goal disallowed. kibongobongo tutasema Refa kashapewa chake
 
Gervinho kule kushoto itakuwa kama anaingia Toilet yake ya Master bedroom yake,Drogba pale kati atakuwa anashangaa kina kelvin Yondani na Aggrey Moris wanavyojigongagonga miguuni mwake,kina Domayo against kina Toure itakuwa ni hangaisha ***** pale kati,wee ngoja
 
Hizo ndo kama zetu tutakazokula muda mfupi baadaye
Mkuu Anselm naona wewe kazi yako ni kuombea mabaya tu dhidi ya Simba na timu ya Taifa, inawezekana tukafungwa kweli lakini si magoli mengi kama unavyoomba na dua zako mbaya mbaya hizo.
 
Hivi ikitokea vijana wakatoa sare si unaweza ukavunja computa yako kwamba haikuletei habari za ukweli.
 
kikosi ni kizuri ila mechi ya marudiano hapa dar itaathiliwa na U-YANGA NA U-SIMBA,yanga watawashangilia akina DROGBA!
 
Mkuu Anselm naona wewe kazi yako ni kuombea mabaya tu dhidi ya Simba na timu ya Taifa, inawezekana tukafungwa kweli lakini si magoli mengi kama unavyoomba na dua zako mbaya mbaya hizo.

Unajua Mkuu hakuna mtu anayeombea mabaya hapa tunaongelea reality.Cote de' Ivoire na Simba Mseto wapi na wapi?
Ni sawasawa na mtu analala katikati ya barabara highway gari zinakuja tunasema yule atagongwa unasema tunamuombe mabaya,kufungwa tunafungwa tena za kutosha,hilo halina ubishi, wee subiria
 
Simba ooh soryy Taifa Stars wanatamani Ivory Coast na yenyewe ingekuwa na migogoro
hahaha, haki ya kweli, inawezekana walipofika pale waliuliizia kwa wenyeji kaama timu yao ina migogoro, wakaambiwa hamna mgogoro wowote, sasa mimi sijui nifanye nini, manake naona moyo utauma sana na mapresha kupanda na kushuka kushangilia timu ambayo najua asilimia mia moja kuwa leo inafungwa....cha kuomba Mungu ni kwamba wafungwe machache basi, na wachezaji wa simba wasiwashangae akina drogba, wacheze booli.
 
Drogba vs samata! Samata lazima a shine, unabishaa ? Weka mzigo tu bet !
 
TBC mtaonyesha mpira huu, au ndo supersport?
 
Yanga undeni timu ya mpira na nyie muwe mnaitwa timu ya taifa maana kwenye timu ya masumbwi wame watosa......
 
kikosi ni kizuri ila mechi ya marudiano hapa dar itaathiliwa na U-YANGA NA U-SIMBA,yanga watawashangilia akina DROGBA!
inamaana kule tunafungwa mbona unaonyesha kukata tamaa....
 
Hivi ikitokea vijana wakatoa sare si unaweza ukavunja computa yako kwamba haikuletei habari za ukweli.

Watoe droo na nani? wameshindwa kutoa droo na Club ya kawaida kula Shandy itakuwa Taifa Stars...thubutuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…