ITV rekebisheni maswali ya kipima joto

ITV rekebisheni maswali ya kipima joto

Kwanza nianze kwa kukipongeza kituo cha ITV kwa kazi nzuri mnayofanya kuhabarisha umma wa Tanzania kwa umahiri mkubwa. Pamoja na pongezi hizo; naomba mfanye marekebisho katika kipindi chenu cha KIPIMA JOTO. Sijui ni nani anaeandaa maswali yenu; kwa kweli ni maswali ambayo hayaeleweki na mengine yanakuwa na majibu ya moja kwa moja (rhetorical questions). Endapo mnataka kweli kupima hali ya mambo katika jamii, basi ulizeni maswali ya kufikirisha.

Nitolee mfano swali lililoulizwa jana (Dec 26/2016): "JE WANAOJENGA GEREJI BUBU MITAANI WAKO JUU YA SHERIA?" This is crazy!! Tayari wote tunajua hakuna aliye juu ya sheria!!

Nawatakia Mwaka Mpya wa Baraka na Pia mje na maswali ya maana 2017.
Umeniwahi kuanzisha uzi!
Mfano wa maswali yao: je wanaohujumu uchumi washtakiwe?? WTF is this??
 
Hakuna kitu naonaga kina ukilaza kama hayo maswali ya kipimajoto. Huwa naangalia taarifa ya habari lakini ikifika hapo wanaposema wakazi wa...... wamekuwa na maoni tofauti khs swali letu la kipimajoto....., naondoa mara moja. Maswali haya hayana ubunifu na majibu yake ni obvious
 
SWALI LA KIPIMA JOTO
"Wananchi kutokula maembe wakati bei yake sokoni ni ya kutupa...Je, Wizara ya afya imetoa elimu ya kutosha kuhusu manufaa ya embe dodo mwilini??

Shubaaamit!
 
KUNA SWALI WALIULIZA "WANAOTELEKEZA NDUGU ZAO HOSPITALI JE WANAWATENDEA HAKI?"
 
Maswali ya kijinga kabsa, hayaelimishi,hayafundsh nk, jamii yetu ina vitu vingi sana vya kujadili kwa manufaa ya wote lakn hata hawabuni hayo maswala ya msingi!

Mm binafsi ikifka majibu ya swali lakipima joto huwa nabadli channel maana ni upuuz
 
Ingekua vzur km wangekua wanauluza maswali yanayoibua majibu ya kero fulani miongoni mwa watazamaji wao. Kwa mfano "NINI KIFANYIKE KUZUIA UJENZI WA GEREJI BUBU MTAANI" hapo wangekua wanakusanya maoni mengi sana kuliko maswal ya muongozo.
Sasa tatizo ni kwamba maswali yao yanahitaji majibu ya NDIO,HAPANA,SIJUI. Hayatoi nafasi ya kujieleza na kawaida ya POLL sio kujieleza ni kutoa tu msimamo wako. Kwa hiyo ikiwa watalenga kupata suluhisho la matatizo na changamoto za nchi lazima waandae suluhisho na kuwauliza watazamaji kama linafaa au la.
 
Nadhani wangekuwa wanauliza maswali kutokana na mijadala inayoendelea mitaani na kwenye vyombo vyote vya habari ikiwemo mitandao na kutoa majibu matatu au manne yaliyotokana na mijadala hiyo kwa mtindo wa multiple choice kisha watu wapige kura ingeleta maana sana. Nilishawahi kuona kitu hicho bbc mwaka 1999.
 
Back
Top Bottom