ITV/Radio One vs CHADEMA kunani?

ITV/Radio One vs CHADEMA kunani?

Issue siyo kuandia issue ni kusoma magazeti yalichoandika kwanini hukwepa kusoma habari zinazoihusu chadema aau tuwasusie kama TBC...........

Suluhisho la kudumu ni CHADEMA kuanzisha TV na RADIO ... Vinagharimu kiasi gani?
 
Mi Si shangai wala kujiuliza kuhusu Media za IPP kutokuandika ama kutangaza habari fulani kama unakumbukumbu nzuri, 1. wamewahi goma kuandika habari za cuf kabla haijawa ccm b' 2, wamewahi susia kuandika na kuriport habari za club ya simba, na sasa wamehamia CDM, Usihofu wakikua wataacha hi tabia ya ovyo na ya kuzilazila
 
Wakuu Salama?

Kuna suala leo limenitatiza sana ingawa limekuwa likijotekeza mara kwa mara katika mazingira fulani fulani

Habari kubwa kwenye magazeti almost yote ya leo ni Juu ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa kugoma kuhojiwa na Jeshi la Polisi kwa kile alichoeleza kuwa hana imani na Jeshi hilo kwani limekalia taarifa nyingi za uchunguzi ikiwemo ile ya kutegewa kinasa sauti chumbani kwake kule Dodoma.

Aidha, habari hiyo ambayo inauza magazeti yote ya leo imeambatana na maamuzi mbalimbali ya kamati kuu ya CHADEMA iliyoketi kwa siku mbili.

Nimejaribu kufuatilia vipindi vya udondozi wa magazet kwenye TV na Radio kuanzia Star TV, RFA, Magic FM na Channel 10 kote wamesoma habari hiyo kubwa nchini. Maajabu ITV na Radio One kwenye vipindi vyao vya udondozi wa magazeti hawajasoma kabisa habari hiyo na mara zote watangazaji wamekuwa wakiudanganya umma kuwa, habari iliyopamba magazeti yote ni ile ya Rais wa Jumuiya ya madaktari kufikishwa mahakamani.

Kinachokera zaidi, Mwandishi anasoma; nanukuu "Katika Gazeti la Tanzania Daima habari kubwa iliyopamba ukurasa wa mbele ni ile isemayo MADIWANI 22 WA CCM MISUNGWI WAJIORODHESHA KUHAMIA CHADEMA" wakati habari kubwa ni ya Dkt. Slaa.

Aidha, taarifa za habari za jana kwenye TV stations zote hakukuwa na habari hiyo ya CDM isipokuwa Channel ten pekee. Niliikodolea macho ITV bila mafanikio.

My Take
-Hivi ITV/Radio One kuna nini hadi kwa makusudi wanaudanganya umma juu ya habari kubwa kwenye magazeti ya leo?
-Kuna tatizo kati ya ITV/Radio One na CHADEMA?
-Inakuwaje mhariri/mwandishi anaruhusu upotoshaji na upindishaji wa ukweli makusudi?

Nawasilisha...

Kwa mtazamo wa haraka haraka inaweza kuwa kweli kwani hata mimi nimefatilia hilo asubuhi na jana kipindi cha taarifa ya habari.
Lakini katika utendaji ITV imekuwa mstari wa mbele kuripoti habari za M4C kuanzia pale jangwani na hata ziara nzima ya OKOA KUSINI na pia kuripoti harakati mbali mbali za M4C kama kule Iringa, Geita na hata DSM.
Kwa tendo hili hatuwezi kuwahukumu ila imetupa fursa ya kufatilia kwa kina jinsi watakavyokuwa wanaripoti habari za OPERASHENI SANGARA II.
 
MENGI huwa anajifanya POPO ila kumbe ni GAMBA KUU KUU.
 
hivi jamani niambieni, mambo pale nyumbani yakienda ndivyo sivyo mfano mabinti wanapata mimbo au vijana wanaanza kuvuta bangi ovyo ovyo tu, je, tutakuwa sahihi kosa si la baba kwasbb yeye hashindi na watoto muda mwingi hivyo ni kumlushia lawama mama yao? kama JIBU NI kumlauma hata baba, basi tukubaliane kuwa hata mzee mengi kama mmiliki wa vyombo hivyo vya habari THERE IS NO WAY tunaweza acha mlaumu kuwa anashiriki katika unafiki huu. ni kweli vyombo vya habari vya IPP vimekuwa na hulka ya kinyongo kwa baadhi ya watu au taasisi fulani fulani. mfano mzuri kama alivyo-site ndugu hapo juu viliwahi goma kutangaza habari za timu ya SIMBA.

Kuna kila dalili kuwa huenda MANJI akashinda nafasi ya uenyekiti wa club ya YANGU (mimi ni simba). stashangaa kuona vyombo vya IPP vikaanza kutoripoti habari za YANGA. si mnajua MANJI na MENGI ni chui na paka.

MZEE Mengi kama kweli uhusiki basi tafadhari geuza shingo uvitazame vyombo vyako. vinaendeshwa KI-ABRAKADABRA sana. CDM ni kama chakula. usipokula ugali, utakula wali au matoke.
 
Call a Spade a Spade not a BIG SPOON!
ITV/radio one ni aje bana....?
 
Kwa mtazamo wa haraka haraka inaweza kuwa kweli kwani hata mimi nimefatilia hilo asubuhi na jana kipindi cha taarifa ya habari.
Lakini katika utendaji ITV imekuwa mstari wa mbele kuripoti habari za M4C kuanzia pale jangwani na hata ziara nzima ya OKOA KUSINI na pia kuripoti harakati mbali mbali za M4C kama kule Iringa, Geita na hata DSM.
Kwa tendo hili hatuwezi kuwahukumu ila imetupa fursa ya kufatilia kwa kina jinsi watakavyokuwa wanaripoti habari za OPERASHENI SANGARA II.

Unaweza kuwa sahihi lakini si sahihi pia. ITV/Radio One hawakuwa na jinsi zaidi ya kuripoti M4C na hata Operesheni okoa Kusini yenyewe kwani it was under agreement (airing live + paying one of the staff for the tour). ITV/Radio one ni media kubwa hapa nchini na wamekuwa wakifanya vizuri hili halina ubishi.

Tatizo langu si ITV/Radio One kutotangaza habari za CDM bali kuudanganya umma kuwa habari kubwa kwenye magazeti yote ya leo ni kufikishwa mahakamani kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari wakati ni tofauti. Lakini kituko kingine ni wao kutokusoma kabisa habari kubwa iliyopo ya Dkt. Slaa na CDM.

Maswali ya kujiuliza ni Je hawakuiona kwenye magazeti? Wana sababu gani ya kutoichambua wakati iko kwenye magazeti yote likiwemo la Nipashe linalochapishwa na IPP? Haikuwa habari kwenye magazeti ya leo?
 
Wakuu Salama?

Kuna suala leo limenitatiza sana ingawa limekuwa likijotekeza mara kwa mara katika mazingira fulani fulani

Habari kubwa kwenye magazeti almost yote ya leo ni Juu ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa kugoma kuhojiwa na Jeshi la Polisi kwa kile alichoeleza kuwa hana imani na Jeshi hilo kwani limekalia taarifa nyingi za uchunguzi ikiwemo ile ya kutegewa kinasa sauti chumbani kwake kule Dodoma.

Aidha, habari hiyo ambayo inauza magazeti yote ya leo imeambatana na maamuzi mbalimbali ya kamati kuu ya CHADEMA iliyoketi kwa siku mbili.

Nimejaribu kufuatilia vipindi vya udondozi wa magazet kwenye TV na Radio kuanzia Star TV, RFA, Magic FM na Channel 10 kote wamesoma habari hiyo kubwa nchini. Maajabu ITV na Radio One kwenye vipindi vyao vya udondozi wa magazeti hawajasoma kabisa habari hiyo na mara zote watangazaji wamekuwa wakiudanganya umma kuwa, habari iliyopamba magazeti yote ni ile ya Rais wa Jumuiya ya madaktari kufikishwa mahakamani.

Kinachokera zaidi, Mwandishi anasoma; nanukuu "Katika Gazeti la Tanzania Daima habari kubwa iliyopamba ukurasa wa mbele ni ile isemayo MADIWANI 22 WA CCM MISUNGWI WAJIORODHESHA KUHAMIA CHADEMA" wakati habari kubwa ni ya Dkt. Slaa.

Aidha, taarifa za habari za jana kwenye TV stations zote hakukuwa na habari hiyo ya CDM isipokuwa Channel ten pekee. Niliikodolea macho ITV bila mafanikio.

My Take
-Hivi ITV/Radio One kuna nini hadi kwa makusudi wanaudanganya umma juu ya habari kubwa kwenye magazeti ya leo?
-Kuna tatizo kati ya ITV/Radio One na CHADEMA?
-Inakuwaje mhariri/mwandishi anaruhusu upotoshaji na upindishaji wa ukweli makusudi?

Nawasilisha...

Kwa kweli huu upuuzi unachosha sasa. Kama Chadema wanadhani wao ni muhimu na ni lazima wawe wanatjwa kwenye TV basi waanzishe ya kwao kama walivyofanya kwa gazeti siyo kudhani kwamba kuna media house yenye responsibility ya kuwataja hata kama there is nothing to write home about.

Hivi Chadema imetoa mchango gani ambao ni meaningful kiasi cha kutaka wawe wanaimbwa kila mara. Hizo siasa za kitoto hazina nafasi na ndiyo udikteta wenyewe wakutaka kuimbwa na kuabudiwa hata kunapokuwa hakuna sababu. Hivi Slaa kuvunja sheria ni suala la kulisifia mpaka unataka kila mtu asome?
 
mmiliki wa chombo cha habari anaimpact kubwa kwenye mtiririko wa habari ipi isikike na ipi isisikike bado mapema kutoa hitimisho.
 
hiyo ndiyo shida ya watu kushindwa kusimamia dhamira zao na kutumikia dhamira za watu wengine hata kama imani zao haziwaruhusu. Some times inawezekana nao wameshaanza kuwatumikia mafisadi.
 
Katika hesabu tunasema kuwa huwezi uka"prove"ukweli kwa kawaida ukweli hujitetea wenyewe. Wafanye wafanyavyo siku zote ukweli utajisimamia wenyewe. Kwa hiyo mkuu usihofu kwa sababu Mungu akiwa upande wetu ni nani atakayetupinga???
 
hata mengi hana imani na vyombo vya usalama sasa nitashangaa mbaba huyu kama hata waunga mkono chadema kwa hili..vinginevyo anaendeleza ukada wake kwenye chama cha mabwepande..hivi kesi ya mtoto wake kutaka kushikishwa madawa ya kulevya..

Nasikia walimfuata watu wa Ikulu na kumwambia kwamba ajitazame yeye ni msafi kiasi gani ndiyo aendelee kuinyoshea nyoshea Serikali kidole. Tokea pale amekuwa mpole sana sijui huyu mzee ana uchafu gani ambao aliwahi kuutenda ambao kwasasa Serikali inamsitiri.
 
Mkuu lengo langu halikuwa kueleza habari ni nzuri kwa CDM au laa bali kuonesha jinsi mwandishi anavyoweza kuudanganya umma kuwa, habari kubwa ni hiyo ya MADIWANI 22 WA CCM KUTAKA KUHAMIA CDM wakati ni tofauti.Nimekupata lakini.

Nakubaliana na mwandishi/msomaji "MADIWANI 22 WA CCM KUTAKA KUHAMIA CDM" kwangu ni habari kubwa kuliko unavyoiona wewe
 
Sijasema si habari kubwa ni kubwa lakini ya pili kwa ukubwa kwenye magazeti ya leo. Mtangazaji anaposimama na kusema habari kubwa iliyopamba magazeti karibu yote ya leo ana maana ni ile kubwa.

Kwenye taaluma ya habari kuna misamiati kama:

1. Lead Story-Hii ni habari kubwa katika gazeti au ile ya kwanza kwenye Radio/TV
2. 2nd Lead Story- Hii ni habari ya pili kwa ukubwa kwenye gazeti na kwa maana hiyo inakuwa ya pili kwneye Radio/TV
3. 3rd Lead Story- Hii ni habari ya tatu kwa ukubwa kwenye gazeti na hivyo ya tatu kwenye Radio/TV
4. Filler Story - Hii ni story ya ukurasa wa mbele ambayo inawekwa kujaza nafasi ukurasa wa mbele lakini yenye umuhimu pia.

Kwa ufafanuzi huo utakuwa umeelewa msingi wa hoja yangu. Ni kwamba wanachokifanya ITV/Radio One kusema habari kuu kwenye magazeti ya leo ni ya Rais wa Jumuiya ya Madaktari kufikishwa mahakamani au MADIWANI WA CCM MISUNGWI kuhamia CDM ni upotoshaji na upindishaji wa taaluma yao. Wameiacha Lead Story ya Dkt. Slaa/CDM na kuipa nguvu 2nd Lead. Kama hawalazimishwi na mwenye mali/ mabosi wao kufanya hivyo basi kuna mushkeli kwenye uelewa wa waandishi/watangazaji hawa. Ni yale yale ya kuita nyeusi nyeupe na nyeupe nyeusi badala ya nyeusi kuwa nyeusi na nyeupe kuwa nyeupe.
 
Nimejifunza toka kwako taaluma dhidi ya objectivity ya story nashukuru. Mwandishi/msomaji katilia kidogo kwangu naona dole. Thanks
 
Wakuu Salama?

Aidha, taarifa za habari za jana kwenye TV stations zote hakukuwa na habari hiyo ya CDM isipokuwa Channel ten pekee. Niliikodolea macho ITV bila mafanikio.

Nawasilisha...

hata mimi mkuu jana hiyo hbr niliisubiri ITV sikuiona
hapa kuna kitu............
 
Mkuu lengo langu halikuwa kueleza habari ni nzuri kwa CDM au laa bali kuonesha jinsi mwandishi anavyoweza kuudanganya umma kuwa, habari kubwa ni hiyo ya MADIWANI 22 WA CCM KUTAKA KUHAMIA CDM wakati ni tofauti.Nimekupata lakini.

Ukubwa wa habari ni suala la hisia binafsi kama mwandishi alisema madiwani 22 kuhama chadema ndo kubwa huenda yuko sahihi
 
hivi jamani niambieni, mambo pale nyumbani yakienda ndivyo sivyo mfano mabinti wanapata mimbo au vijana wanaanza kuvuta bangi ovyo ovyo tu, je, tutakuwa sahihi kosa si la baba kwasbb yeye hashindi na watoto muda mwingi hivyo ni kumlushia lawama mama yao? kama JIBU NI kumlauma hata baba, basi tukubaliane kuwa hata mzee mengi kama mmiliki wa vyombo hivyo vya habari THERE IS NO WAY tunaweza acha mlaumu kuwa anashiriki katika unafiki huu. ni kweli vyombo vya habari vya IPP vimekuwa na hulka ya kinyongo kwa baadhi ya watu au taasisi fulani fulani. mfano mzuri kama alivyo-site ndugu hapo juu viliwahi goma kutangaza habari za timu ya SIMBA.

Kuna kila dalili kuwa huenda MANJI akashinda nafasi ya uenyekiti wa club ya YANGU (mimi ni simba). stashangaa kuona vyombo vya IPP vikaanza kutoripoti habari za YANGA. si mnajua MANJI na MENGI ni chui na paka.

MZEE Mengi kama kweli uhusiki basi tafadhari geuza shingo uvitazame vyombo vyako. vinaendeshwa KI-ABRAKADABRA sana. CDM ni kama chakula. usipokula ugali, utakula wali au matoke.
..kweli.. sikia hii karibuni 40% ya fedha alizochangiwa Ulimboka katoa Mengi abrakadabra!
Piga chini ITV kama tulivyoishusha TBC
 
Back
Top Bottom