ITV napendekeza iwe TV ya taifa

ITV napendekeza iwe TV ya taifa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,892
Kwa mtizamo wangu ITV ya bwana Mengi nimetokea kuipenda kwa sababu ina utaifa wa kweli wa bila kupendelea upande wowote na zaidi imekuwa mstari wa mbele kulinda na kutetea maadili ya nchi na mengine mengi ni tofauti na inayoitwa TBC ambayo imekuwa kama tv ya chama badala ya umma
 
Yes wazo zuri Mwambie mbunge wako apeke hoja binafsi bungeni.
 
Hata mimi naona Itv haina kificho kwa habari zake kama Tbc inaonekana kama ya chama fulani.
 
Sawa kabisa...ITV ndo TV ya Watanzania....Pia Star Tv wapo njema pia..

kwa kuwa yeye anataka itv iwe ya taifa na wewe unapendekeza na star tv sasa ipi iatakuwa ya taifa? au zote ziwe?
 
Labda hilo Taifa liwe "The united Republic of HIMO TO NAMANGA"
 
ITV tv ya taifa? may be taifa la mengi.
ITV ina mazuri mengi BUT waandishi wake hawapo huru, hasa when it comes to habari zinazo mhusu mengi. just like TBC wandishi wasivyo huru kuandika habari zinazo kosoa serekali

kama iki hitajika tv mbadala wa tbc NINGESHAURI sibuka tv kwa wanao ifahamu wanajua haiko biased
 
Back
Top Bottom