Nianze kwa kusema kuwa kwa nature ya kazi yangu huwa sipati muda wa kuangalia habari za usiku kila siku. Ila kila ninapoangalia kile kipengele cha kipima joto huwa nabaki hoi, najiuliza ni nani haswa anahusika na ku-frame maswali yanayoulizwa? mfan, swali la jana lilisomeka : je serikali imeshindwa kuzuia matumizi mabaya ya tindikali ( as if ni lazima kuwa na leseni ili kumiliki tindikali). swali la leo likasoma: wanaotumia vibaya tindikali je wanyongwe?
kwangu mimi napata shida nikijaribu ku-assimilate ujumbe ama objective ya maswali ambayo yako framed kwa mantiki ambayo kwa critical thinker lazima ikupe shida kunyambua.
Mkuyati
Katika dhana nzima ya "safety and security" ilikuwa ni LAZIMA kila anayeuza na kununua tindikali za aina zote LAZIMA awe amesajiliwa. Kumiliki silaha ya moto LAZIMA usajiliwe na silaha yako isajiliwe pia, kwa kuwa ina uwezo wa kutumika vibaya kwenye matukio ya uhalifu.
Kwa hiyo, jinsi ilivyodhihirika, tindikali nayo ina uwezo (na imeshatumika mara kadhaa) wa kutumika kwenye uhalifu; kumwagia mtu tindikali kwa nia ya kumdhuru huo ni uhalifu.
Tusiishie hapo. Kuna zaidi ya tindikali. Kule Arumeru kwenye "mashamba" ya maua, wafanyakazi wengi, wake kwa waume, wameathirika na matumizi mabaya ya viuatilifu vya kuua wadudu kwenye maua. Hawakupewa kinga stahiki. Wanaume wameathirika vibaya kutokana na kuishiwa kabisa nguvu zao za kiume; wanawake wengi wamepata matatizo ya mimba zao kuharibika. Kwa hiyo, hata wauza viuatilifu na wateja wao, wote kwa pamoja LAZIMA wasajiliwe.
Kuna vitu vingi ambavyo ni hatarishi kwa maisha yetu, kwa mfano, chakula: Je, unajua kwamba kuna aina fulani za uyoga ambazo zina sumu kali ndani yake?
Kuna watu wanafuga na kumiliki wanyama hatari, kama vile nyoka na aina fulani ya chura, ambao wana sumu kali. Hebu fikiria, hivi sasa kuna mtindo wa watu kuwatupia akina-dada nyoka bandia kwenye magari yao (iwapo watakuta hawajafunga madirisha), hapo kuzua mshtuko mkubwa na kuwasababishia ajali, kwa nia ya kuwapora mali zao. Kwa hiyo hata hao wanaoagiza vitu bandia kama vile nyoka bandia (wanaotengenezwa kwa mpira laini), bastola za plastiki ambazo hufana kwa karibu sana na zile halisi, n.k., LAZIMA nao wasajiliwe, na wanaotaka kumiliki vitu hivyo pamoja na wanyama hao hatari, LAZIMA wasajiliwe.
Ni kwa ajili ya usalama wetu kaka! Lakini kwa bahati mbaya, serikali yetu hailioni hili suala kwa upana wake; kwa sasa ni tindikali. Ngoja mtu mzito atupiwe nyoka wa bandia kwenye VX yake, itokee ajali mbaya, ndio wataamka!