ITV kwa hili mmekiuka maadili ya chombo chenu!

ITV kwa hili mmekiuka maadili ya chombo chenu!

Unakataa huo mchezo usionyeshwe au na Wewe ni " Mdau " wa " mauza uza " hayo ya Ushoga hivyo unaogopa sasa upuuzi wenu kuwekwa hadharani?
tatizo ni kwamba watoto wadogo wakiona wanaiga. siku hizi watoto wadogo wa kiume wanakutwa wakiwa wanafanyiana haya mambo.
 
Ndiyo maana Serikali ikawawekea Chuo Kikuu cha Sanaa cha Bagamoyo ili mkatoe ujinga wa kutofahamu nini maana ya Sanaa na uwasilishaji wake kwa audience. Kwa kukusaidia tu katika Drama yoyote Character anatakiwa kuuvaa ule uhusika 100% ili kile anachotaka kukifikisha kwa Jamii kifike vizuri na sawia hivyo basi nadhani tena badala ya kuwalaumu na kuwashutumu ungekuwa wa Kwanza kuwasifu kwa wanachoigiza kwani kwa uelewa wako " finyu " wa masuala mazima ya Sanaa utaona wanakosea au wanajizalilisha ila tunaojua tunafurahi kwani wanafikisha ujumbe ambao kwa namna moja au nyingine utasaidia kubadili mwenendo mzima wa Jamii yetu ambayo sasa " imekengeuka " huku Vitendo vya " Kishoga " vikizidi kushika kasi tena hasa kwa Vijana.

ITV hongereni sana kwa hiyo Program na BASATA nina imani nanyi kuwa mmebobea katika Sanaa na Maudhui yake hivyo sitegemei kama nanyi " mtakengeuka " na kuufungia huo mchezo na badala yake nadhani mtawaandalia TUZO hao Characters wote wa huo mchezo. Unakataa huo mchezo usionyeshwe au na Wewe ni " Mdau " wa " mauza uza " hayo ya Ushoga hivyo unaogopa sasa upuuzi wenu kuwekwa hadharani?
Hivi kweli wewe uko timamu kichwani? Ngoja nisiandike kitu maana nitapigwa ban bure hapa. Nimekupuuza, jitu zima na akili za kitoto.
 
Hivi kweli wewe uko timamu kichwani? Ngoja nisiandike kitu maana nitapigwa ban bure hapa. Nimekupuuza, jitu zima na akili za kitoto.

Kupigwa kwako BAN na kunijibu kwa HOJA kunahusina nini? Naona umedhihirisha " upumbavu " wako kwani kama umeshindwa tu kuelewa nilichokiandika hapo nadhani mahala sahihi kwa Wewe kuwepo ni Hospitalini Milembe.
 
Kuna Tamthiliya ya Kibongo inarushwa kila Jumapili saa 1.30 jioni kupitia kituo cha ITV kwa jina la "MAMA KUBWA",binafsi nilikuwa naifuatili ila inaanza kunitia kichefu chefu. Kuna humo ndani kaigizi basha jina lake halisi anaitwa Mrisho, kuna kijana mwingine anaigiza kama bwabwa, yaani Shoga anaigiza kwa jina la Robert. Nimeona tena wanaigiza kipumbavu kabisaa, maana mara washikane shikane mara hii wanaoga wote bafuni. Stupid saana.

Ningeshauri BASATA waifungia Tamthiliya hii na ikiwezekana kuwapa onyo Kali ITV.

Ifahamike kituo hiki cha TV tulikuwa tunakiheshimu hata kuangalia na watoto tulionelea inafaa, sasa badala yake wanataka kuharibu maadili yetu kweupe.
Japokuwa tunajua Ushoga upo lakini si kwa kuendelea kuushabikia.

ITV mnakishushia heshimu kituo chenu cha TV. Chukueni hatua.
Kama ni kweli basi wanastahili adhabu kali. Maadili ni muhimu
 
Kama uliangalia hata iliyopita sehemu ya 21 pale walikuwa bar na huyo Robert, Mrisho na binti fulani ambaye imetokea amempenda Robert, baadaye akaona anapapaswa Mrisho kush Washroom na yule dada akamchana Mrisho kuwa hiyo tabia ya ku-deal na Gays itakoma lini na akamwambia Julieth na Robert wanatoka familia moja. Yaani kuna ujinga unaendelea mle. Serikali iliangalie hili haya si mafunzo mema kwa jamii yetu.
Sasa mbona yule binti kama anajua tobert gay mbona bado anampenda aisee nilikua sijui
 
Back
Top Bottom