ITV kupost kipindi kuhusu mkurugenzi wa SIDO aliyetenguliwa ni kukosa umakini

Ni kweli ni recorded. Lakini si kingeondolewa tu. Badala yake wangeweka hata programu ya wanyama wa mikumi; au kuunganisha na bbc.
Ni fursa kwa mgurugenzi mpya kumuona alomtangulia.Pia ni sawa na kukabidhi ofisi ukizingatia kilirekodiwa akiwa bado mkurugenzi.Binafsi sioni tatizo
 
Ni kweli ni recorded. Lakini si kingeondolewa tu. Badala yake wangeweka hata programu ya wanyama wa mikumi; au kuunganisha na bbc.
Kwani wewe tatizo lako ni nini hasa? Lengo la kipindi kile ni nini; kumtangaza mhojiwa au shughuli za taasisi anayoiongoza? Kwa tukio hilo kama ITV wakati wanarusha kipindi hicho bila kuwa na taarifa za uteuzi mpya unaweza kueleza nini? Na kwani isingetosha mtangazaji katika utangulizi akamweleza mhojiwa kama "aliyekuwa mkurugenzi wa SIDO" na kipindi kikaendelea kurushwa badala ya kukifuta?
 
Hivi mantiki ya kipindi ilikuwa ni kumtambulisha Mkurugenzi aliyopita au kueleza jinsi Sido inavyo fanya kazi na matarajio yake? Bado sijaona tija kabisa ya kuanzisha huu uzi kuilaumu ITV!

Isitoshe aliyekuwa ana hojiwa wala hajakabidhi ofisi na uzuri alicho kuwa ana kieleza hakimuhusu yeye bali kina husu Sido na watanzania! Mimi nilijikita kusikiliza alicho kuwa anaeleza kuhusu Sido kuliko ukurugenzi wake!

"Taarifa iliyotolewa leo Ikulu Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Sylvester Michael Mpanduji umeanzia leo tarehe 18 Julai, 2016.Kabla ya uteuzi huu Prof. Sylvester Michael Mpanduji alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

Prof. Sylvester Michael Mpanduji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Omary Jumanne Bakari ambaye uteuzi wake umetenguliwa."

Wajifunze kuwa juu ya gemu.. uvivu wa kujiimarisha umewajaaa.. wajirekebishe.. huu uwe mfano kwa wengine pia..
 
Ila jamaa bonge mno hadi nikajiuliza huyo kweli ni injinia. Hata kama mkurugenzi bado site unaenda n.k. Sasa huo mwili inaonesha ni kula sana, kusinzia na kujamba ofisini
Come on my dia Kaunga sio kila miili ni ya uzembe na kula kula ovyo, mingine ni inborn. Tema mate chini waswahili husema usitukane wakunga uzazi ungalipo...
 
Kwani wewe tatizo lako ni nini hasa? Lengo la kipindi kile ni nini; kumtangaza mhojiwa au shughuli za taasisi anayoiongoza? Kwa tukio hilo kama ITV wakati wanarusha kipindi hicho bila kuwa na taarifa za uteuzi mpya unaweza kueleza nini? Na kwani isingetosha mtangazaji katika utangulizi akamweleza mhojiwa kama "aliyekuwa mkurugenzi wa SIDO" na kipindi kikaendelea kurushwa badala ya kukifuta?

Highlighted: Hilo halikufanyika. Na huo unakuwa upotoshaji.
 
Aiseee wamemtengua jamaa,he sounded like a visionary for SIDO, dahh serikali hii mtu ht usijipendekeze manaa
 
Sioni tatizo hapa kwa aliyekuwa mkurugezi kuhojiwa kuhusu SIDO...siku kipindi kinarekodiwa muhusika alikuwa bado na dhamana ya cheo chake
Na ratiba ya kipindi ilishapangwa
 
Come on my dia Kaunga sio kila miili ni ya uzembe na kula kula ovyo, mingine ni inborn. Tema mate chini waswahili husema usitukane wakunga uzazi ungalipo...
Jamani mmmh. Mbona vijijini hakuna inborn mabonge kama huyo? Mbona ni sayansi tu hiyo. Shinda na njaa siku nzima na tembea kilometa 10 kwa siku tuone kama kuna ubonge inborn
 
Tatizo lipo, tena kubwa tu! Kumtambulisha mtu kwa wadhifa ambao sio wake ni kuupotosha umma, hilo halipingiki isitoshe hawakuwaomba radhi watazamaji.
Pili, kile kipindi ingawa kilikuwa recorded, hakikuwa kipindi cha marudio, ndo kilikuwa kinarushwa kwa mara ya kwanza, hivyo kulikuwa na kila sababu ya ku-edit kabla ya kurushwa hewani.
Kwa maoni yangu, ITV katika hili wameteleza. Hoja kwamba eti hilo ni jambo dogo halina athari nionavyo mimi si sawa. Tutakuwa watu wa ajabu kama tunafumbia macho makosa hata ikiwa ni madogo kwa sababu hata hayo yanayoitwa makubwa yalianza na madogo.
 
Ni kweli mkuu, makosa yamefanyika ,ni vyema ITV warekebishe kosa hilo kwa namba yeyote watakavyoona inafaa. Ikiwezekana kurudia kipindi hicho nikiwa edited ipasavyo au kutoa tangazo la kukiri kosa na kuclarify kwamba ni walifanya mahojiano na aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Sido.
Much respect to you you are a realy GREAT THINKER. big up kwa mchango wako
 
Back
Top Bottom