Itv hapa arusha!

Wikiliki

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
528
139
wadau ni muda mrefu sasa kituo cha television cha itv hakionekani hewani kwa njia ya antena za kawaida. Kulikoni au mengi ameona arusha hakuna la maana ndio maana akaamua kuitoa hewani. Kuna wakati nilisikia mitambo ya kurushia matangazo ilipigwa shoti ya umeme lakini mbona ni muda mrefu sana. Mwenye habari zaidi atujuze.
 
Itv ni kituo kisicho kua. Kila mwaka kiko kama mwaka wa juzi, program zilezile umangi meza uleule.
 
baadhi ya maeneo mengi ya nchi tv za bongo zote hazishiki.kuna tetesi eti vituo vyote vinahamia digital ndy maana vingine havipatikani.Wataalam nadhani wanakuja soon kwamajibu ya kina
 
Itabidi walazimishwe wote waweke local channels zote ili watumiaji wachague wanataka channels zipi za nje vinginevyo itakuwa balaa.
 
tutakuwa na rundo la ving'amuzi sasa....dstv, startimes, ting......bado deck yangu....nyumba itakuwa stoo......khaaa....




Sio lazima uwe na ving'amuzi vyote! Unaweza kununua kutokana na channel unazozihitaji.
 
Siyo Arusha tu, hata huku Nyanda za Juu Kusini TV zote za Mh. Mengi yaani ITV, Capital, na EATV hazipo hewani. Vilevile Channel 10 imetoweka muda mrefu sana. The only Tv iliyobaki ni Star TV na TBC-1, ukweli vyombo vya habari vikiwa vichache uhuru wa kupata habari unapungua. HIVI HAWA TCRA WAPO??? KAMA WAPO MBONA KIMYA? HUU UTARATIBU WA VING'AMUZI UTATUFIKISHA MAHALI IKAWA HABARI NI ANASA ILIHALI KIUKWELI NI HAKI YA BINADAMU. TCRA AMKENI ACHENI USINGIZI.
 
Sio lazima uwe na ving'amuzi vyote! Unaweza kununua kutokana na channel unazozihitaji.

sawa......saa hiyo nahitaji kuona Movie magic, channel O au Hallmark.......baadae niangalie tamthilia kwenye STVE1 au music TBC2....nikimaliza taarifa ya habari imefika nataka niangalie ITV.........hapa nafanyaje......?
 
Back
Top Bottom