Itumie jumapili usiku namna hii

Itumie jumapili usiku namna hii

Ocran

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2017
Posts
1,045
Reaction score
1,384
Jumapili Usiku/Sunday Night !! Jumapili Usiku ndiyo wakati sahihi wa kuipanga week yako nzima iliyo usoni mwako !! Pata mda usiku ukiwa umetulia jumapili......andika malengo yako unayotaka kuyakamilisha ndani ya week husika.

Jiwekee walau kila siku hakikisha una vitu vitatu umekamilisha au umefanya kwa kiasi kikubwa !
Andaa nyimbo zako tano kwenye listi yako ya nyimbo zenyewe kukutia hamasa na kukufanya uamke mapema kitandani na kukupa imani juu ya kile unachokifanya.......pia andaa videos zako tatu kwenye you tube zenye kukutia hamasa na hata elimu juu ya kile unachotamani kukitimiza......sikiliza na kuangalia ukiamka au baada ya kazi zako za siku !! Weka alarm yako ya kila siku tafadhali amka kila siku kabla ya saa kumi na moja asubuhi hii itakusaidia kupata mda wa kusali kwa imani yako na kutafakari kwa kina juu mambo mengi juu yako kabla ya kuianza siku !! Nawatakia week yenye mafanikio tele juu yenu....!!
 
Mpendwa kwa nini iwe juma pili na sio Juma mosi? au ijumaa ?
 
Hizi nadharia za kina Anton luvanda na Chris's Mauki zilinishinda zamani sana......
 
Kwangu wiki yangu naipanga ijumaa maana ndo siku yangu ya mwisho ya wiki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom