It's time for change | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

It's time for change

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chilisosi, May 27, 2012.

 1. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  We need change not history.
  CCM waondoke wawapishe chadema halafu kama wakishindwa basi miaka mitano baadae tunarudisha magamba.
  Mie natabiri kifo cha CCM kama kile chama cha kaunda wa zambia UNIP.
  UNIP iliongoza Zambia kwa miaka mingi sana toka enzi zile za wazambia kupewa unga na mkate bure mpaka pale copper ilipokwisha thamani na mkate ikabidi wanunue wakati hela hawana.
  Huwezi kuamini kuwa chama cha Kaunda kwenye matokeo ya uchaguzi uliopita mwaka jana kilipata asilimia 0.13% yaani chini ya asilimia moja, kwa maana nyingine hata wale wajumbe wake wa nyumba kumi na makatibu kata hawakupiga kura bali waliokipigia kura ni mabalozi wake, mawaziri wake na vingunge kadhaa wenye imani.
  Mkutano wa jana pale jangwani umetugusa wengi sana hadi wale walio ndani ya CCM.
  Huwezi shangaa kesho ukisikia January Makamba ameamua kumfuata Zitto Chadema au kusikia Mwakyembe pamoja na kupewa uwaziri akaamua kujiunga na M4C.
  Kila jambo na wakati wake. na CCM imepita wakati wake. Watu wamechoka sana kiasi kwamba hata kama CCM wakiamua kuvua magamba sasa itakuwa ni too late. ni sawa na kumnyima mgonjwa chakula bora ili apone halafu unapoona anakaribia kufariki ndio unamletea machungwa ujue kuwa atayatapika tu kwa sababu utumbo umeisha jikunja.
  CCM NI SAWA NA MTU ALIYEMNYIMA HELA ZA MATIBABU NDUGUYE HALAFU ALIPOFARIKI ALIMNUNULIA JENEZA LA DHAHABU.
  Tumeona mifano mingi sana ZAMBIA, MALAWI, EGYPT, FRANCE, MAREKANI na kwingineko duniani ambapo watu wanapewa uhuru wa kuamua mabadiliko kwa kupigia kura chama wanachokitaka ili kukiondoa walichokichoka na sasa watanzania wamechjoka CCM wanataka chadema.
  CCM hata wakimtumia huyu Shibudu mkabila mwenye mdomo mkubwa unaotoa maneno bila kufikiri haitawasaidia kitu. mdomo mali yake anaweza kuufanyia lolote hata akiamua kula m..vi ni mdomo wake sitamlaumu.
  CCM walitakiwa wabadilike pale Mrema alipohama kwani aliwaamsha watanzania wengi wa mjini wakaanza kuamini mabadiliko wakabaki wale wa vijijini wakiogopa upinzani kwa sababu waliogopa vita. Badala yake waliendelea kuwadanganya wananchi kuwa mkichagua upinzani mtakuwa mnapigwa viboko na kunaweza kutokea vita. lakini sasa ukiangalia nchi nzima inataka maendeleo. leo hii nenda jeshini,polisi, magereza, walimu, maofisini nahata pale ikulu penyewe kapige kura za siri uulize mnataka chama gani kiingie ikulu.
  Mie nakuapia usishangae ukakuta hadi mkuu wa kaya mwenyewe akapigia kura chadema kwa sababu itakuwa siri na hakuna mtu atakayejua umechagua nani.
  Htukatai CCM imefanya mengi mazuri na mabaya vile vile kwa sababu hata hivyo viwanda tunavysema imeviua ni wao wenyewe walivijenga. Mie huwa najiuliza, Hivi Nyerere alitumia akili gani kiasi cha kujenga miundombinu mizuri sana wakati ule ambao hata teknolojia ilikuwa duni sana.
  NYERERE alijenga Viwanda na kila kiwanda kilikuwa na hadi nyumba za wafanyakazi
  NYERERE alijenga mahospitali
  NYERERE alijenga nationa housing kwa wafanyakazi wote serikalini. mie nimezaliwa kwenye kota za serikali.
  NYERERE aliwashawishi wachina wakajenga TAZARA.
  Nyerere alijitahidi sana kwa uwezo aliokuwa nao lakini kilicho muangu=sha ni ile vita ya kagera, sasa hawa warithi wake hajapigana vita hata moja lakini wanashindwa kwa nini? tena siku hizi tuna migodi, gesi nk? na wasomi ni kila kona sio enzi zile chuo kikuu ilikuwa mlimani tu.
  LET'S BE HONEST, WE NEED CHANGE!
  HUWEZI VAA SHATI LA KIJANI MIAKA YOTE!
  JARIBU GWANDA LA KHAKI UONE TOFAUTI.
   
Loading...