Mwanga Lutila
JF-Expert Member
- Nov 10, 2016
- 4,137
- 13,824
Usione ukadhani ndugu yangu kuwa kila mtu ambaye leo anacheka alizaliwa anacheka. Kama kila mtu angesema kule alikopitia mpaka hapa alipofika angeweza kutengeneza movie ya Episode kama 5.
Wapo wengine ambao wao hawajawahi kujua mapenzi ya baba na mama kwenye maisha yao. Wengine walipitia katika mazingira magumu sana. Wengine wame experience malezi ya upande mmoja hajui baba anafananaje, Wengine wamekulia familia za wazazi wote wawili lakini ameshuhudia mapambano ya ndondi ya baba na mama kila siku.
Usione ukadhani kuwa kila aliyejenga nyumba ni jasho lake mwenyewe la kazi halali, Usione ukadhani leo watu wanaendesha magari ukadhani kachanga changa mshahara. Tumekuzwa na kufanikiwa katika njia tofauti.
Miongoni mwetu wapo waliokuwa kabla ya wakati. Kuna waliopoteza Bikira zao[Wakike na Kiume] Katika umri mdogo pengine kwa kubakwa ama kwa kushiriki mapenzi ya mdada wa kazi. Lakini miongoni mwetu wapo waliokuwa kimajukumu kabbla ya wakati. Kuna wengine kati yetu walilazimika wao kuacha masomo ya shule ya msingi ama Sekondari ili wawezr kuwasomesha wadogo zao. Fedha walizopata walilazimika kutunza mama zao na wadogo zao kwa kujinyima sana. Majukumu yalisababisha wengine ku-sacrifice kwa ajili ya kusaidia familia zao.
Shukuru Mungu wewe ambaye umekulia familua ambayo imejawa Upendo, Familia ambayo mnalazimishwa kula mayai na sausage, Shukuru Mungu ulikuwa unalazimishwa kulala Mchana ama sivyo utanyimwa Maziwa. Wengine hata huo mlo mmoja haukuwepo wala muda wa kunywa maziwa. Amekulua uji wa mtama na Mabumunda Sembuse wewe Sausage.
Wengine mazingira tuliokulia hata hapa tulipo kuongea Sentence moja ya kiingereza ni Muujiza, Wenginetu ukichunguza familia ya Upande wa Baba na Mama peke yako ndo angalau unajua Sentence ya Kiingereza, Pekr yako ndo umesoma kamshahara kaki kadogo kila mtu anakatolea macho.
Usione mtu ukadhani maisha yake yanafanana na yako, Wengine wamezaliwa katika mkondo wa mafanikio angalau Mama alikuwa Mwalimu na Baba Bwana Shamba ukirudi nyumbani unapata muda wa kusoma, Angalau baba alikuwa anakuhimiza kusoma sababu anajya umuhimu wa kusoma, Wengine walikuwa walikuwa analazimishwa kuchota maji na kuwa waganga wa kienyeji.
Ndio maana hata hatua zake za maendeleo hazifanani na wale waliozaliwa kwenye mikondo ya mafanikio kwenye maisha ya vizazi vijavyo.
Wikiendi njema