Itoshe tuu kusema ndoa inahitaji....

Itoshe tuu kusema ndoa inahitaji....

socket

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2014
Posts
305
Reaction score
435
Ukiona mtu yuko kwenye ndoa miaka zaidi ya mitatu basi..

Itoshe tuu kusema ndoa inahitaji uvumilivu

Ndoa ikikosa uvumilivu ni kama vile mikono na miguu kwenye gari vishindwe kuelewana, mikono inazungusha stearing kukata kona na miguu inakanyaga mafuta.

Kwenye ndoa inabidi ujifanye mjinga ili kumuepuka mpumbafu..

Unatoka kazini umechelewa ukitafuta riziki mke anakuuliza kwann umechelewa akihisi ulikuwa na mwanamke mwingine..

Kwenye ndoa mume/mke anaweza kuwa na matumizi yasiyo ya lazima kipindi ambacho wewe unahitaji kubana matumizi au hauna hela..

Kwenye ndoa mke anaweza kukutaka umgegede wakati ambao anajua kabisa uko na stress na hata hisia hauna [emoji4][emoji4] nyie ndoa ni vichekesho..

Kwenye ndoa mnaweza mkagombana na mkasameheana na kesho mke/mme akarudia jambo lilelile.. Ndoa ni kuvumiliana..

Nishauri vijana ambao hamjaingia kwenye ndoa, hakikisha huyo mpenzi wako unampenda na umeridhika nae, usioe kwasasabu anatuliza nyege zako, usiolewe kwasababu ukiwa na shida ndogo ndogo anakusaidia.

Vyote vinapita na vina majira hivyo hakikisha vikipita na akabaki yeye basi utampenda..

Miaka 8 kwenye ndoa
 
Mke nyumbani anaweza akaandaa chakula kuanzia asubuhi mpaka usiku kwa ajili yako bila wewe kujua na wala yeye kukuambia...
Wewe unatoka kazini na marafiki mnapitia sehemu unakula unashiba..
Ukifika nyumbani itakubidi ule tuu
 
Umeongea yote ya msingi lakini umesahau umuhimu wa kumshirikisha Mungu.

All in all ndoa siyo kitu kinachotisha Ila vijana ndiyo wanaofanya ionekane hivyo,mimi leo ukiniuliza kipi bora kati ya kuishi bila ndoa au kuishi ndani ya ndoa nitakuwa na jibu tofauti na ambalo ningekupa miaka kumi iliyopita.
 
There comes a moment unagundua NDOA siyo kuwa tu na MKE mwenye Degrees na mtafutaji Hela....
 
Vyote vinapita na vina majira hivyo hakikisha vikipita na akabaki yeye basi utampenda..
Hapa ndo pana changamoto sana.
Je unaemuoa/olewa nae asipokua hivyo alivyo leo (kiafya/kimaumbile) je utampenda??
 
1687900357487.jpg
 
Ukitaka Ndoa uimudu

1. Mume sharti ampende Mkewe kwà upendo wa kiMungu ( God love )

2. Mke anatakiwa kumpenda mumewe kwà upendo usiokua na strings attached ( unconditional love ) ...bila kutegemea Malipo.

The greatest commandment ni

LOVE ONE ANOTHER.
 
Back
Top Bottom