jaman mwenye kujua maana ya n maneno hayo anifahamishe maana mara nyingi nimekuwa nikiyasikia mahala fula fulan hasa kwenye mkusanyko wa watu weng kama mkutano n.k sa huwa sielew anakuwa amemaanisha nin mtu akiongea hvyo

Neno itifaki asili yake ni kukubaliana (makubaliano ya pande mbili au zaidi).
Hivyo usemaji wa mtu kuwa "itifaki imezingatiwa" ina maana makubaliano yamezingatiwa, au kilichofanyika au kusemwa kimo ndani ya makubaliano n.k.

Kidogo inakubalika lakini haikidhi kiu ya muuliza swali
Itifaki= utaratibu wa jinsi ya kuendesha shughuli fulani kutokana na utaratibu uliowekwa.
mathalani katika shughuli za mikutano ni kiongozi gani anatakiwa kuingia kwanza kisha nani afuatie na nani awe wa mwisho kuingia katika sehemu ya mkutano, je mwenyeji wa mkutano anatakiwa kukaa upande gani na mgeni mwalikwa anatakiwa kukaa upande gani, kama ni shughuli ya kitaifa ni wimbo gani wa taifa unatakiwa uanze je ni wa Rais mwenyeji au Rais mgeni?, na baada ya mkutano nani anatakiwa kutoka kwanza na nani awe wa mwisho. mambo kama haya au utaratibu kama huu ndo huitwa ITIFAKI au protocol
Mimi nimeona wanasiasa wakiwa wavivu wa kuwatambua waheshimiwa wote kwa kutaja mlolongo wa majina wanapoanza hotuba zao, huminya kwa kusema itifaki imezingatiwa. Sijui kama ni matumizi sahihi ya usemi huo.
Itifaki= utaratibu wa jinsi ya kuendesha shughuli fulani kutokana na utaratibu uliowekwa.
mathalani katika shughuli za mikutano ni kiongozi gani anatakiwa kuingia kwanza kisha nani afuatie na nani awe wa mwisho kuingia katika sehemu ya mkutano,
Umerudi kule kule kwenye asili ya neno itifaki!
Kabla ya kufikia hatua hii ina maana kuna makubaliano ambayo yalifanyika kwanza ndio ukawekwa huo utaratibu.
Na mifano yako yote mingine uliyotaja inarudi kwenye asili ya neno itifaki ambayo ni makubaliano.
Kikawaida utaratibu huwekwa baada ya aina fulani ya makubaliano.
*Ningefurahi sana kama katika tafsiri yako ungewafahamisha wasomaji wako asili ya neno lenyewe hivyo wakati wanaposoma tafsiri yako huwa wanajua umetokea wapi.
Ni katika neno hili itifaki ndipo lilipochimbuka neno mawafikiano.
Kwa lugha ya kigeni ni..."all protocols observed"..Maranyingi hutumika kwenye majukwaa ya kisiasa (wakati wa utambulisho) ikimaanisha utaratibu wote wa utambulisho (esp kwenye upande wa ranking/vyeo) umefuatwa...hivyo ndo navyoelewa mimi...otherwise subiri waje wenyewe
Itifaki imezigatiwa maana yake hasa CCM ni: Posho ipo, chakula kipo na mkipitisha hoja yenye dalili ya rushwa hapo ndo utasikia neno itifaki imezigatiwa huku kila mmoja akiombea kikao kiishe mapema wakapige pasu.