Itakuwaje siku CCM itakapoondoka??

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Hakuna shaka kwamba ifikapo mwaka 2015 au kabla ya hapo kutatokea mabadiliko makubwa sana ya kiuongozi Tanzania!

Lakini taswira iliyopo ni kwamba mabadiliko hayo hayataihusisha CCM ambayo yenyewe ndiyo inayotakiwa kuondolewa ili mabadiliko "yatokee". Kwa maana nyingine ni labda CCM yenyewe ibadilike kabisa (over hauling party System), jambo linaloonekana kwamba haliwezekani kutokana na minyukano ya kimaslahi iliyomo ndani ya chama hicho.

kwa hiyo tunapozungumzia mabadiliko yatakayotokea 2015 au kabla ya hapo tunazungumzia wakati huo huo kuondoka kwa CCM. Ni lazima tujitayarishe kuipokea uongozi CCM na kuhimili athari za kuondoka kwake, ziwe ni athari chanya au athari hasi. Watu wanaotaka tuamini kwamba CCM ikiondoka madrakani kutakuwa hakuna athari ni watu wanaotaka kutudanyanya.

KANU ilipoondoka madarakani nchini Kenye aliacha athari kubwa sana ya ukabila. Wakati wote ilipokuwa madarakani KANU haikushughulika kabisa na tatizo la ukabila nchini mwao. Hata USSR iliposambaratika athari za mfumo wa Kikomunisti inaonekana mpaka sasa. CCM kwa kukaa kwake madarakani kwa zaidi ya miaka 35 ni lazima mfumo wake uache madhara makubwa sana kwenye jamii yetu.

Sote tunakumbuka jinsi watu walivyovunja sheria (na bado wanavunja) bila kuchukuliwa hatua kwa sababu tu sehemu zao wanazofanyia shughuli wametundika bendera za CCM au wao wenyewe waliichangia CCM. Mali ngapi za umma ambazo zimechukuliwa na CCM zitarudishwa.

Ukiangalia kwa makini utaona baada ya kuondoka kwa CCM kuna kazi ya kufanya. Kuna kazi ya kubadilisha mfumo mzima wa jinsi ya kuendesha mambo na kila raia awajibike na kuepusha chama kutawala serikali. Watu wote walipe kodi na wanaokabiddhiwa jukumu la kuchunga kodi na kupanga matumizi yake ni lazima wahahakishe wanatimiza wajibu wao.
 
Itakuwa shangwe na vigelegele kwa wapenda maendeleo na haki na vilio na kushaga memo kwa wachumia tumbo (Wakuu wa Mikoa na wilaya, Mabalozi, Wenye vyeo vya kugawiwa na Rais hata kama huna sifa)
 
Itakuwa shangwe na vigelegele kwa wapenda maendeleo na haki na vilio na kushaga memo kwa wachumia tumbo (Wakuu wa Mikoa na wilaya, Mabalozi, Wenye vyeo vya kugawiwa na Rais hata kama huna sifa)
Hiyo ni athari moja uliyoiona ongeza na makatibu tarafa kwenye List yako. Lakini hawa wakiondoka watawekwa wengine ambao si wa CCM au tunabadili mfumo kwenye mchakato wa kuandika katiba mpya?
 
Thread yako naitunza nita muonesha Rais atakaekuwa madarakani kwa tiketi ya CDM Ii ayafanyie kazi mawazo yako tusiwe kama USSSR na Kanu pia kuta kuwa na shangwe kuu nchini Tanzania kwani wakati tulio usubiri kwa takribani miaka 27 utakuwa umewadia
 
Hiyo ni athari moja uliyoiona ongeza na makatibu tarafa kwenye List yako. Lakini hawa wakiondoka watawekwa wengine ambao si wa CCM au tunabadili mfumo kwenye mchakato wa kuandika katiba mpya?
Katika mchakato wa Katiba mpya mimi napendekeza kama wakuu wa mikoa na wilaya wanatakiwa basi Wachaguliwe na wananchi wa mikoa hiyo na wawe wanakaa katika mikoa au wilaya hizo.
 
Katika mchakato wa Katiba mpya mimi napendekeza kama wakuu wa mikoa na wilaya wanatakiwa basi Wachaguliwe na wananchi wa mikoa hiyo na wawe wanakaa katika mikoa au wilaya hizo.
Na kama wakuu wa wilaya na Mikoa watachaguliwa na wananchi, jee sifa za kuwa wilaya au mkoa ziwe hizi sasa au tutafute nyingine na ziweje?
 
Hakika itakuwa shangwe isiyoelezeka maana watanzania watakuwa wamepata ukombozi wa kweli.

Ccm ni kichefuchefu kweli ni bora kuitapika ili tuondokane na adha hii.-chafu kabisa.
 
Kazi wala si kuiondoa CCM
kazi ni kundesha nchi better baada ya CCM kuondoka
tazama Kenya na Zambia
wapinzani walichukua nchi na wakashindwa na wao kubadili mambo
 
ccm wakifikiria hapo ndio huwa wanachanganyikiwa. 'eti tuwe wapinzani? Si aibu hii?' hakika nawaambia, heri kuwa poromoted kuliko kuwa demoted! Ccm wakijua fika mwanzo wao wa kuwa wapinzani umekaribia tusishangae kusikia siku jeshi limekabidhiwa nchi kwa kisingizio cha hali ya hatari. Hiyo ndio mbinu ya mwisho ya ccm kwa kuwa wanategemea siasa kuishi
 
nabii si lazima awe mzee,,,,,,.......jeshi litakabidhiwa nchi kwa kisingizio cha hali ya hatari///////heri mie kimyaaaa,
 
Back
Top Bottom