Ndugu zangu Watanzania,
Natambua na kuelewa ya kuwa Ni kweli huwezi kuungwa mkono na kila mtu, ni kweli huwezi kupendwa na kila mtu,ni kweli huwezi kukubalika kwa kila mtu ,ni kweli huwezi kuwafurahisha watu wote,ni kweli huwezi kuwaridhisha mioyo yao watu wote. Hata ungewafanyia wema gani wanadamu bado huwezi kukata kiu ya kila mtu na kukosa lawama au maneno.
Hata ungewaunganishia watu mabomba yenye kutoa maziwa na asali majumbani mwao bado hutapendwa na kila mtu na badala yake wengine watasema hujawapa sukari ,huku wengine wakisema shombo ya maziwa inaleta sana nzi majumbani mwao na hivyo kutishia mlipuko wa kipindupindu. Hata ungewabeba watu mgongoni wapo watakaokulaumu na kukulalamikia ya kuwa unawafunga sana na mbeleko hadi kuwaumiza migongo yao.
Hivyo ni ukweli kuwa mwanadamu hana jema na hivyo ni bora utende wema uende zako pasipo kusubiri shukurani kutoka kwa watu. Maana mwanadamu hana shukurani hata siku moja.
Embu fikiria ndugu zangu kwa akili yako timamu unaweza vipi mnyima kura ya ndio Rais Samia Mama aliyegusa Maisha ya kila mtanzania na kuleta matokeo chanya? Unamnyima vipi Kura kiongozi Aina ya Rais Samia aliyeleta mapinduzi katika kila secta. Kumbukeni ni Rais Samia amekamilisha mradi wa bwawa la mwalimu Nyerere lenye kutoa megawati 2115.
Ni Rais Samia ameongeza kima cha chini kwa watumishi wa umma kufikia Laki Tano kwa mwezi, ni Rais Samia Amekamilisha ujenzi wa Daraja lenye urefu wa zaidi ya KM 3 Mkoani Mwanza, Ni Rais Samia amejenga reli ya SGR na kuzindua usafiri huo,Ni Rais Samia imeipeleka kileleni Tanzania katika Diplomasia na heshima kimataifa imepaa, ni Rais Samia ameongeza idadi ya watalii kufikia millioni mbili kwa Mwaka.
Ni Rais Samia Ameboresha huduma za Afya na hivyo kufanya hata wageni zaidi ya Elfu 12 kutibiwa Nchini,Ni Rais Samia Ametoa ajira za ualimu zaidi ya Elfu 89 ,Ni Rais Samia Amepunguza bei ya mbolea kutoka laki moja na 20 kwa mbolea ya DAP hadi elfu 70 baada ya kutoa Mabilioni ya Ruzuku,ni Rais Samia amefungua fursa za watu wanaoanza biashara kufanya bure bila kudaiwa mapato mpaka biashara isimame vizuri.
Ni Rais alifungulia vyombo vyote vya habari vilivyokuwa vimefungiwa na kupokonywa lessen zao, ni Rais Samia anayewapa Elfu kumi kumi wanafunzi wa vyuo kama pesa ya kujikimu, ni Rais Samia anayetoa Elimu bure hadi kidato cha sita kwa kutoa zaidi ya Billion 33 kila mwezi,Ni Rais Samia amewalipa madeni yao watumishi wote wa umma waliyokuwa wanadai kwa miaka mingi.
Ni Rais Samia Amepaisha Bei za mazao mbalimbali hapa nchini kuanzia kahawa hadi Korosho. Ndio sababu mapato ya korosho yamepaa zaidi ya mara Nne kufikia Trilioni 1.6. kutoka Billioni 452. Hii ni kwa kauli yake ya kilimo ni Biashara pamoja na kuweka mikakati mbalimbali ikiwepo ya kutafuta wawekezaji pamoja na wanunuzi kutoka maeneo mbalimbali Duniani ikiwepo India.
Sasa Unaanzia wapi kumnyima Kura Mama Yetu Mpendwa? Kama siyo kujitafutia laana na Mikosi unakuwa unataka nini ewe mtanzania? Nini ambacho tulitaka na hakijafanywa au kuanza kutekelezwa au kuwekwa katika mikakati ya utekelezaji? Sauti ya nani haijasikilizwa masikioni Kwa Rais Samia Mama yetu Mpendwa? Nani kaporwa mali zake au kufungiwa biashara yake au kuchotewa na kufungiwa akaunti yake ya Benki kwa uonevu?
Mnataka nini kwa Mama huyu Mwenye Moyo wa upendo ,huruma ,ukarimu ,upole ,ucha Mungu , unyenyekevu na Usikivu? Mnataka awafanyie nini watanzania wenzangu cha zaidi mpate kuridhika? Mnataka nini Jamani ndugu zanguni? Mnataka nini cha ziada? Afanye nini Mama yetu kwetu sisi watanzania wenzangu ili mpate kusema asante? Kwanini tusimshukuru Mungu aliyempatia kibali cha uongozi Rais wetu kipenzi?
Watanzania wenzangu ni lazima mfahamu ya kuwa Hakuna Malaika atashuka kutuongoza sisi. Na Rais Samia Siyo Malaika . Ni binadamu Aliyeumbwa kwa Mfano wa Mungu. Kiukweli kama huna upofu wa akili na macho utakili na kukubali bila unafiki ya kuwa katika Ubinadamu wake Rais Samia amefanya kazi kubwa sana inayohitaji pongezi na shukurani kwake.
Natamani kuendelea kuandika zaidi na zaidi bila kuchoka. Maana naona Itakuwa ni aibu ,fedheha na chukizo mbele za Mwenyezi Mungu kwa mtanzania mwenye akili Timamu na anayejitambua kumnyima kura ya ndio Rais wetu Mpendwa katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwishoni Mwa Mwaka huu. Ila kwa hakika Ipo Siku wenye chuki binafsi na Rais Samia watatoka hadharani huku wakibubujikwa machozi ya majuto kumuomba msamaha Rais wetu Mpendwa Mama Samia na kumpongeza kwa kazi tukuka aliyofanya na anayoendelea nayo kuifanya.
View attachment 3400571
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.