Itakuwa kazi kumzuia Lowassa kuingia Ikulu

Bintiwangara

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
551
287
Kwa ufupi

Kabla ya kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa amekuwa mbunge wa jimbo la Monduli kwa zaidi ya miaka ishirini, huku akishika nyadhifa mbalimbali serikalini, ikiwamo Uwaziri kwa awamu kadhaa na Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.

Mkongwe huyu wa siasa, amejiunga na chama hicho kikuu cha upinzani baada ya kushindwa katika kura za maono za kumtafuta rais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

By Joster Mwangulumbi, Mwananchi Makala iliyokuwa na kichwa cha habari "Kwa nini Lowassa anaweza kuwa rais" iliwakuna wengi, lakini kama ilivyotarajiwa iliwaudhi wengine na walionyesha hasira zao kwa kutuma ujumbe mchafu.

Badala ya kupinga hoja kwa hoja, mmoja alituma ujumbe: "…shame on you"; mwingine akasema, "Nasikitishwa kwamba hata wewe umenunuliwa"; halafu yupo aliyesema, "Nilidhani uandishi wa habari ni taaluma kumbe wako wajinga"; yupo aliyeandika, "…huna akili, mjinga wewe…" na mwingine kwa raha zake ameniandikia, "Lowassa atakuongoza wewe na mkeo."

Uelewa wao umewaongoza kuandika hivyo. Makala ile haikulenga kumpigia debe Edward Ngoyayi Lowassa, bali ulikuwa uchambuzi wa hali ya hewa ya kisiasa nchini na kwa kuwa niligundua mikakati ya chini kwa chini, nilikusudia kudokeza kuwa waziri mkuu huyo wa zamani alikuwa mbioni kuhama CCM na huenda Watanzania wakamuunga mkono bila kujali ana kashfa. Walioielewa makala ile wameendelea kupongeza baada ya kuona kada huyo wa CCM katua Chadema.

Historia inasemaje?

Wanasiasa wanaotoswa katika vyama "kwa madai hawafai" wakihamia upinzani hujipatia umaarufu na baadhi hushinda chaguzi. Na leo nitafafanua zaidi juu ya wanasiasa waliotoswa na wakashinda au kuvitikisa vyama tawala ili kusisitiza hoja yangu "Kwa nini Lowassa anaweza kuwa rais wa Tanzania."

Fungua macho na akili. Kuanzia mwishoni mwa mwaka 2010 Tunisia ilitumbukia kwenye machafuko ya kisiasa yaliyotawala hadi mwaka 2011 wakati wa maandamano ya vurugu yaliyouondoa madarakani uongozi wa Rais Zine El Abidine Ben Ali kutokana na sababu kadhaa. Baada ya vurugu kutulia, walifanyia marekebisho katiba na Bunge la Katiba lilimchagua Moncef Marzouki kuwa rais wa mpito.

Hata hivyo, ulipofanyika uchaguzi mkuu Desemba 2014, bado Watunisia walimhitaji na kumchagua, kwa kishindo, Mohamed Béji Caïd Essebsi aliyekuwa waziri mkuu katika serikali ya muda iliyoondolewa madarakani. Caïd Essebsi alikaribishwa kuongoza muungano wa vyama vya siasa chini ya chama chake cha Nidaa Tounes.

Kwa nini vyama vya siasa?

Lengo la chama cha siasa ni kushika dola na lengo la mwanasiasa yeyote duniani ni kushika madaraka ndiyo maana baadhi hupigania urais na wengine ubunge na udiwani. Mwanasiasa akikosa nafasi katika chama kimoja, kwa sababu ya mizengwe, huhamia chama kingine na kushinda japokuwa wengine hushindwa.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa, msomi na mwandishi yeyote anayelaani mwanasiasa kuhamia chama kingine atakuwa anaongozwa na msimamo wa kiitikadi. Hata hivyo, ni kweli kwamba katika kuhama vyama, baadhi ya wanasiasa hufifia na kupotea lakini wengine huibuka kuwa gumzo.


Hadi mwaka 1985 Maalim Seif Sharrif Hamad alikuwa kipenzi ndani ya CCM na mwanasiasa madhubuti. Uamuzi wake wa kuwania urais wa Zanzibar kupambana na Idrid Abdul Wakil uliwachefua CCM. Wakamfitinisha. Januari 1988 alitemwa kwenye Baraza la Mapinduzi na akavuliwa cheo cha Waziri Kiongozi. Mei 1988 akafukuzwa uanachama wa CCM pamoja na wenzake sita kutoka Baraza la Wawakilishi. Mei 1989 alitiwa mbaroni na akafunguliwa kesi kwa madai ya kukutwa na nyaraka za siri za Serikali. Tangu mwaka 1989 hadi 1991 alikuwa kizuizini.

Ilipofika fursa ya kuanzisha vyama vingi "aliasisi" Chama cha Wananchi (CUF). Je, ‘amekufa' kisiasa au ameimarika zaidi?

Kenya ilikuaje?

Mwaka 2008 yalizuka machafuko yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 1000 na wengine kwa maelfu walikosa makazi nchini Kenya. Waliodaiwa kuchochea vurugu za kisiasa ni Uhuru Kenyata aliyekuwa mshirika wa Rais Mwai Kibaki na William Ruto aliyekuwa mshirika wa Raila Odinga.

Kenyatta na Ruto ni miongoni mwa watu waliofikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC). Kesi dhidi ya Kenyatta ni kama ‘imetupwa' baada ya mashahidi wengi kujitoa lakini Ruto pamoja na mwandishi wa habari Joseph arap Sang wana kesi ya kujibu.

Kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2013 Kenyatta na Ruto walielemewa na shutuma za kuhusishwa na machafuko kwamba hawafai lakini Wakenya walipuuza wakawachagua Kenyatta kuwa rais na Ruto kuwa makamu wake kupitia muungano wa Jubilee.

Kuelekea uchaguzi mkuu wa rais nchini Afrika Kusini, iliibuliwa kashfa ya ufisadi katika ukarabati wa makazi ya Rais Jacob Zuma yaliyoko Nkandla. Upinzani ulijenga hoja na katika kampeni ulishawishi wananchi kutoipigia kura ANC ya Zuma kwa sababu ya walichoita "Kashfa ya Nkandla." Wananchi hawakuelewa ‘mahubiri ya ufisadi' dhidi ya Zuma bado walimpigia kura nyingi akarudi madarakani.

Nchini Marekani, tajiri mkubwa aliyewahi kuwa meya mara tatu katika jiji la New York, Marekani, Michael Bloomberg alijiwekea historia kwa kushika wadhifa huo kupitia vyama vitatu tofauti. Kila alipofanyiwa mizengwe alihama chama. Hadi mwaka 2001 Bloomberg alikuwa Democrat, alipofanyiwa mizengwe alihamia chama cha Republican. Mwaka 2007 alijiondoa kwenye chama hicho akawania umeya wa jiji hilo akiwa mgombea huru na akashinda.

Kilichombeba Bloomberg kokote alikokwenda ni mtaji wa wapigakura siyo chama. Hata waliowahi kuwa wanadiplomasia maarufu Condoleezza Rice na Hillary Clinton wamekuwa na historia ya kuhama vyama.

Halafu kuna aliyewahi kuwa seneta wa Connecticut, Joe Lieberman. Kwa miaka mingi amekuwa Democrat. Mwaka 2006 alijitoa akawa huru lakini mwaka 2008 alimfanyia kampeni mgombea urais kupitia Republican, John McCain. Alipoulizwa kwa nini aliamua kuhama vyama alijibu, "Chama cha Democrat hakikuwa tena kile chama nilichojiunga kikiwa na taswira ya Rais John Kennedy."

Mtazamo mpya wa Lowassa

Majibu ya Lieberman ni sawa na ya Lowassa anayesema "Hii si CCM anayoijua" na ndiyo kiini cha kuondoka na kujiunga na Ukawa. Je, atashinda katika mazingira anayofuatwa fuatwa na kashfa ya Richmond? Jibu ni ndiyo.

Kashfa ya Richmond iliibuliwa na wapinzani wake wa kisiasa ndani ya CCM ikasababisha akajiuzulu mwaka 2008. Waliotaka kuitumia kashfa hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 walishindwa, mbunge huyo mwenye nguvu katika jimbo lake la Monduli na mkoa wa Arusha kwa ujumla, alishinda kwa kishindo.

Rais Kikwete alisema ilikuwa ajali ya kisiasa na mwaka 2010 alimpigia debe akisema ni mtu safi. Hata Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana alipopita Monduli alimsifu Lowassa hukua akidai Lazaro Nyalandu anazurura.

Si hivyo tu, mwaka 2012 bado alichaguliwa kwa kishindo kuingia NEC na ameendelea kuwa na ushawishi mkubwa nchini. Kama kashfa hiyo haikumzuia kushika vyeo ndani ya CCM, itakuwaje na nguvu nje ya chama hicho tawala?

Lowassa amekuwa maarufu katika kipindi chote cha maisha yake na kazi alizofanya, hakika zinamtangaza. Wakati CCM itakuwa inahangaika kumnadi, kwa wananchi, mgombea wake John Magufuli, upande wa pili Lowassa atakusanya mamilioni ya wanachama wa Ukawa pamoja na wafuasi waliokuwa wanamuunga mkono tangu akiwa CCM.

Mbunge huyo wa Monduli si chaguo langu, nimewahi kuandika hivyo katika magazeti mengine niliyofanyia kazi. Sijageuka jiwe. Ninachoeleza "mimi na wewe" tunaompinga, tufungue macho na akili zetu tujiulize CCM ndiyo yenye Serikali na Serikali ya CCM ndiyo yenye Takukuru, polisi na vyombo vingine vya uchunguzi, imeshindwa nini kumfungulia kesi katika kipindi cha miaka saba ambayo hakuwa madarakani?

Sababu moja kubwa ni kwamba bado Serikali ilikuwa inasimamia msimamo wa Takukuru iliyochunguza sakata hilo na kueleza hakukuwa na rushwa.

Je, Serikali ilifanya uchunguzi mwingine au ilibaki kuamini ripoti ileile ya Takukuru kuwa hakukuwa na rushwa katika zabuni ya Richmond? Ikiwa hawakumshitaki awali itakuwa kazi kumchukulia hatua leo ili kumzuia asiingie ikulu. Tafakari!


Chanzo: Mwananchi
 
Goli la mkono...



DSC_1069.jpg


DSC_0250.jpg



DSC_0196.jpg


DSC_0302.jpg


DSC_0341.jpg


DSC_1076.jpg



Watu wa lowassa!
 
tumesahau alikua mwenyekiti wa kamati ya bunge ya kimataifa
 
KIM KARDASH

Uzuri wa lowasa anakubalika, ndani ya CCM, ndani ya Ukawa, Nje ya CCM, na nje ya Ukawa... LAZIMA AWE RAISI
 
Last edited by a moderator:
Mwaka wa mageuzi ukifika, huwa yanakuja bila kuzuilika. CCM tekelezeni ahadi zenu, picha hizo hazisaidii.
 
Kama kuna MTANZANIA asiyependa mabadiliko hapa nchini....basi hana budi kupimwa akili zake kama kweli zipo sawa sawa....maana kila MTANZANIA ni shahidi wa mateso tuliyopitia tukiwa chini ya CCM na bado tunaendelea kuyapitia....otherwise uwe ni mnufaika wa mfumo nyonyaji wa CCM.....VIVA UKAWA...
VIVA LOWASA..
WANANCHI TULIOJERUHIWA NA CCM TUNATAKA MABADILIKO.....HATA LINGEWEKWA JIWE DHIDI YA CCM NINGECHAGUA JIWE.....
PEOPLEEEEEEEEESSSSS
POWERRRRRRRRRRRRRR...
 
Mwandishi anamaanisha kuwa jamaa

anawezafunguliwa kesi kabla ya

uchaguzi Kisha UKAWA ikabaki 'YATIMA'
 
Kama kuna MTANZANIA asiyependa mabadiliko hapa nchini....basi hana budi kupimwa akili zake kama kweli zipo sawa sawa....maana kila MTANZANIA ni shahidi wa mateso tuliyopitia tukiwa chini ya CCM na bado tunaendelea kuyapitia....otherwise uwe ni mnufaika wa mfumo nyonyaji wa CCM.....VIVA UKAWA...
VIVA LOWASA..
WANANCHI TULIOJERUHIWA NA CCM TUNATAKA MABADILIKO.....HATA LINGEWEKWA JIWE DHIDI YA CCM NINGECHAGUA JIWE.....
PEOPLEEEEEEEEESSSSS
POWERRRRRRRRRRRRRR...

Vile vile ni vyema watanzania tukajikumbusha unabii wa Mwalimu Nyerere alioutoa mwaka 1995.

Unabii na 1 Mwalimu Nyerere alisema upinzani wa kweli wa vyama vya siasa nchini utatokea kutoka ndani ya CCM pale ambapo chama hicho kitaanza kumeguka.

Unabii no 2 Mwalimu alisema kuwa wananchi watakapoona hawawezi tena kuyapata mabadiliko ndani ya CCM watalazimika kuyatafuta nje ya CCM.

Kama yupo mtanzania ambaye pamoja na matukio makubwa ya kisiasa yanayotokea nchini hivi sasa ataendelea kuufanya moyo wake mgumu na kukana kwa nguvu zake zote kuwa unabii wa Mwalimu hauwezi kutimia mwaka huu basi hakika mtu huyo atakuwa ameamua kujitia 'uartificial' uziwi na upofu!
 
Lowasa hatutampa kura kwa sababu ya usafi wake ambao hatuujui, wala si kwa mbamba na uwezo na sifa zozote zinazoweze kulilnganishwa na zile za Dr. Slaa na walioko UKAWA.

Tunampa kura kwa sababu kuu mbili. 1. KIKUBWA NA UWEZO WAKE WA KUIMALIZA CCM. 2.Yuko UKAWa ambako hata akitaka kufanya maloloso ya ccm hatapata nafasi kwa kuwa mfumo utamdhibiti.

Maneno mengi wala hayahitajiki!.
 
Vile vile ni vyema watanzania tukajikumbusha unabii wa Mwalimu Nyerere alioutoa mwaka 1995.

Unabii na 1 Mwalimu Nyerere alisema upinzani wa kweli wa vyama vya siasa nchini utatokea kutoka ndani ya CCM pale ambapo chama hicho kitaanza kumeguka.

Unabii no 2 Mwalimu alisema kuwa wananchi watakapoona hawawezi tena kuyapata mabadiliko ndani ya CCM watalazimika kuyatafuta nje ya CCM.

Kama yupo mtanzania ambaye pamoja na matukio makubwa ya kisiasa yanayotokea nchini hivi sasa ataendelea kuufanya moyo wake mgumu na kukana kwa nguvu zake zote kuwa unabii wa Mwalimu hauwezi kutimia mwaka huu basi hakika mtu huyo atakuwa ameamua kujitia 'uartificial' uziwi na upofu!

Ni mwendawazimu pekee ndiye asiyejua kuwa huu ni wakati wa MABADILIKO.....
WATANZANIA TUMEKUWA NA DAIMA TUTAKUWA WAMOJA....
SINA SABABU ZA MSINGI ZA KUIPIGIA KURA CCM......
 
Lowasa hatutampa kura kwa sababu ya usafi wake ambao hatuujui, wala si kwa mbamba na uwezo na sifa zozote zinazoweze kulilnganishwa na zile za Dr. Slaa na walioko UKAWA.

Tunampa kura kwa sababu kuu mbili. 1. KIKUBWA NA UWEZO WAKE WA KUIMALIZA CCM. 2.Yuko UKAWa ambako hata akitaka kufanya maloloso ya ccm hatapata nafasi kwa kuwa mfumo utamdhibiti.

Maneno mengi wala hayahitajiki!.

Mfumo wa cdm msafi ni upi?
Mfumo huu ambao Zito alivojaribu kuhoji matumizi mabaya mkamtafutia visababu na kumtimua?

Mfumo gani mtu mmoja anauza chama kwa 10b na wengine mnabaki "ewala baba"

Mfumo huu huu uliomchosha Dr, Padri Slaa akaamua kukaa pembeni.

Mfumo huohuo nasikia prof nae anaukacha,

Wewe unauongelea mfumo upi ,,au unatiririka tu.
 

Attachments

  • 1438830654343.jpg
    1438830654343.jpg
    28.4 KB · Views: 503
Magufuli yupo kwenye tafakuri nzito. Anawazia umati ule wameukodi, CCM wanamtumia kama mbuzi wa kafara.
Anawaza kua yeye ndio atakua mgombea wa kwanza kushindwa katika mbio za Urais ndani ya CCM.....anatia huruma!
 

Attachments

  • 1438831836857.jpg
    1438831836857.jpg
    21.3 KB · Views: 397
Ngoja wapite hapa wendawazimu wasioweza kutafakari yanayoandikwa...

Patajaa mapovu hapa...
Kutomfungulia mashtaka sio kwamba hana makosa ni kwa kuwa serikali ilikuwa inamkingia kifua , sasa kwa kuwa kawa kapi na kutemwa na CCM ngoja tu atapelekwa keko akanyee debe
 
Back
Top Bottom